Nisehemu gani na mkoa gani na mtaa gani maduka yamefungwa? kama wameona ni vyema kufunga wafunge....
Rais wa Ghana[emoji13] [emoji13]Wanaotaka kufunga maduka wasipate shida, waniambie niwasaidie kuyafunga, watayafungua 2025 nikitoka, by rais Wa Ghana. Nahisi hili lingekuwa miongoni mwa majibu
Rais wa Ghana[emoji13] [emoji13]
Nisehemu gani na mkoa gani na mtaa gani maduka yamefungwa? kama wameona ni vyema kufunga wafunge....
Wasitishie wafunge tu kimya kimya watu wataona ila kama wamekutuma waambie salamu zimefika
Hahaha hayo yangekuwa majib ya Nana Ado baada ya kuapishwaWanaotaka kufunga maduka wasipate shida, waniambie niwasaidie kuyafunga, watayafungua 2025 nikitoka, by rais Wa Ghana. Nahisi hili lingekuwa miongoni mwa majibu
tegeta kiwalanikuelekea wapi?
basi nitaukuta hukotegeta kiwalani
Mbona huyu jamaa anasita kuelezea madhara wamachinga walioleta kwa walipa kodi.kama Rais angepata fursa ya kujibu hili tishio la wafanyabiashara unahisi angewajibuje ukirejelea majibu kwa mbunge wa wale waathirika wa tetemeko aliyeomba kupunguziwa bei za vifaa vya ujenzi?
Hapa kasi tu!
========
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja, amesema wataendelea kufunga biashara, kama maeneo ya wafanyabiashara hayataboreshwa ili kuwavutia.
Minja alisema hayo jana kwenye mahojiano maalumu na kituo kimoja cha redio, kuhusu kufungwa kwa biashara Dar es Salaam. Alisema awali wakati Serikali inaingia madarakani, ilijipambanua kuwa itahakikisha watu wanalipa kodi, ili kukuza uchumi wa nchi.
Minja alisema walikubali mpango huo wa Serikali kutokana na malengo yake mazuri kwa wafanyabiashara ya kuleta ushindani kwenye biashara.
"Baada ya hapo, kuliibuka mfumuko wa kodi bandarini kutokana na mahesabu ya upitishaji mizigo,” alisema.
Alifafanua kuwa hakukuwa na kodi mpya, bali kilichofanyika ni kwa wenye mzigo bandarini kuongezwa thamani ambapo mwenye mzigo wa Sh milioni 30, alijikuta ukibambikiwa Sh milioni 200.
"Na hii si kodi mpya, bali ni yale mahesabu ya ushuru wa forodha," alisema na kuongeza kuwa baada ya kubaini hilo, walitembelea nchi mbalimbali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutafuta mbinu za kudhibiti ubambikiwaji wa thamani za mizigo.
Alitaja nchi walizotembelea kuwa ni Kenya na Uganda, ambako walikuta kodi zikikatwa kulingana na thamani halisi ya mzigo na hakukuwa na ubambikizaji.
Minja alisema kama uchumi wa nchi unakua, anaiomba Serikali ihakikishe ukuaji huo unamgusa mwananchi wa kawaida, ili kuondokana na malalamiko.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi kwa mwishoni mwa mwaka jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema pamoja na uchumi kukua kwa asilimia 7.2, baadhi ya wafanyabiashara walifunga karibu maduka 2,000.
Kwa mujibu wa Dk Mpango, utafiti uliofanyika Dar es Salaam na Arusha kati ya Agosti na Oktoba mwaka jana, ilibainika katika wilaya ya Ilala wafanyabiashara wakifunga maduka 1,076.
Dk Mpango alisema kwa Kinondoni biashara 443 zilifungwa na kufuatiwa na Temeke, ambako biashara 222 zilifungwa huku Arusha, wafanyabiashara 131 wakifunga biashara zao.
Alitaja aina ya biashara zilizofungwa kwa wingi kuwa ni za sekta ya ujenzi na biashara ya jumla na rejareja na chache zikiwa kwenye huduma za usafiri.
Chanzo: Jambo leo
Mkuu kati ya hayo 2000 hebu tutajie makampuni 10 tu na sababu za kufunga biashara zao.makampuni zaidi ya 2000 yamefunga milango yake ya biashara yaani yamefilisika ....[bankruptcy ]hii ni hatari kubwa kwa nchi ambayo inataka kujenga viwanda .........hao walaji watapata wapi pesa ......kama biashara zinafungwa ..hayo makampuni ni yale ambayo yako rasmi ...kuna maelfu ya biashara nyingine ambazo sio rasmi yameadhirika ...kwa mpango huuu hiyo kodi itatoka wapii>>????
Nani anamkomoa nani na kwanini?Jelous people never win visas vibaya sisi sote wamoja tukifa tunaoza ya nini kukomoana?
Wafunge tu kwa sab wakati wanafungua hawakumshirikisha mtu zaidi ya familia zao.Ni sehemu gani na mkoa gani na mtaa gani maduka yamefungwa? Kama wameona ni vyema kufunga wafunge....
Hizo shughuli zingine si biashara pia au wataenda kufungua makanisa?Mkuu wanaenda kwenye shughuli nyingine kwani wanaokula ni wenye maduka pekee?
Wigo wa kodi ni mpana sana na biashara ni kama daladala wengine wanafunga wengine wanafungua. Wengi wa hao wanaofunga hawakuwa wanalipa kodi hivyo serikali mapato yako vile vile tena yanaongezeka sab wigo umezidi kupanuliwa kwa mfano maduka mengi yanatumia efd mahotel yote siku hizi ukienda na mchepuko unapata efd makampuni ya huduma za kuzoa takataka wanatoa risiti za efd baadhi ya daladala wanatoa risiti za efd hebu angalia wigo huo.makampuni zaidi ya 2000 yamefunga milango yake ya biashara yaani yamefilisika ....[bankruptcy ]hii ni hatari kubwa kwa nchi ambayo inataka kujenga viwanda .........hao walaji watapata wapi pesa ......kama biashara zinafungwa ..hayo makampuni ni yale ambayo yako rasmi ...kuna maelfu ya biashara nyingine ambazo sio rasmi yameadhirika ...kwa mpango huuu hiyo kodi itatoka wapii>>????