Wafanyabiashara wanaanza kurudi tena upinzani

Wafanyabiashara wanaanza kurudi tena upinzani

Maneno ya kusema lowassa ni fisadi kwa sasa ni out of fashion.maana toka ameanza kusemwa sio leo,rais wa serikali ya 4 aliliskia,rais wa awamu ya tano amelisikia nae na vyombo vyote vya dola wamesika.mbona hawamkamati ili ashitakiwe kwa ufisadi aliofanya?tuna polisi wasomi,wanasheria wa waserikali wasomi,takukuru wasomi na rais msomi wote wako kimya,sembuse wewe?
Haya maswali kawaulize viongozi wa chadema.
 
Tatizo la nchi ni kuaminisha watu kwamba wewe ukiwa maskini basi wewe ni Mzalendo.......


Tena hili raisi maghu analipigia kampeni Sana kutuambia watu masikini ndiyo wazalendo, mfano mmoja Ni kuwaambia atashusha mishahara ili watu waishi kama mashetani, lakini hatuambii atapandisha mishahara ya kima cha chini ili tuishi kama malaika
 
Mimi ni UKAWA lakini kwa hili hapana! Hakuna sukari mitaani na wafanyabiashara wameweka millions of kgs of sugar in godowns, Is this acceptable. Think if it were you, would you accept that?
hiyo sukari mbona wanaikamata lakini tunaambiwa haina shida na wanaiachia?
na sio sukari tu, sera za huyu jamaa ni majanga kiuchumi, mambo ya bei elekezi, kuhamishia pesa b.o.t, kuingilia biashara za watu hovyo sio vizuri
 
Bussiness + Politics = 0
uko sawa, na ndo maana hata Mwl alishaonya kuhusu wanasiasa / watumishi wa serikali kujingiza kwenye biashara. Always businessmen are after super profit,
 
Lowassa alianza kuwahi kiti cha mbele mapema kwenye chumba cha wapinzani!

Kwa sasa anapata protection yote ya CHADEMA!

Kwa sasa ukilitamka jina la Lowassa, walinzi wanaibuka haraka kutoka ndani ya shimo ili kumtetea kwa kutumia hoja za nguvu!

Ajabu sana.. Walimwita fisadi papa kwa miaka nane..
 
Kwa sasa anapata protection yote ya CHADEMA!

Acheni porojo..CHADEMA haina dola haiwezi kuwa na Protection..Acheni Maigizo....Mpelekeni Lowasa Mahakamani...ili awajibishwe.....Hamwezi kuongoza katika misingi hii ya makamera
 
Unapokuwa na kikosi cha aina hii cha kukulinda na kukutetea kwa hoja za nguvu haina maana kuwa wewe ni mtawala wa nchi!

From here;
1.jpg


To here;
mbowe_Red%2BBrigade.jpg

DSC_0037.jpg

Hawa kwa sasa ndiyo walinzi wa Lowassa!

Lowassa is finished!
Kwa mtazamo huyo Tanzania itapataje maendeleo ya kiuchumi? Kisayansi? Kisiasa? Hopeless!!!!!!
 
Lowassa alianza kuwahi kiti cha mbele mapema kwenye chumba cha wapinzani!

Kwa sasa anapata protection yote ya CHADEMA!

Kwa sasa ukilitamka jina la Lowassa, walinzi wanaibuka haraka kutoka ndani ya shimo ili kumtetea kwa kutumia hoja za nguvu!
Ni kweli, ila tumpe tahadhari kuwa ubeo hlikuwa ungo. Yaliyomkuta Dr Slaa huenda naye yakamkuta. Ajue yumo kwenye chama chenye wanafiki wote wa Tanzania, hao huwa hawachelewi kusema wamebadili gia angani.
 
Kwani Lowassa kuwahi na kukaa kiti cha mbele cha nyumba ya CHADEMA ina maana He's still alive?

Nimesema, mtu yoyote akilitaja jina la Lowassa, walinzi wake wanakuja mbio kumtetea kwa kutumia hoja za nguvu. Are you the one?

Lowassa is finished!
Huna lolote mchumia tumbo mkubwa we ! Mtu aliyekwisha alipata wapi uwezo wa kumshawishi Maalim seif ajitoe kwenye uchaguzi ( kama ule uzi wako wa kizushi uliouweka hapa ? ) , huku kwetu Tandika mwembeyanga kuna msemo wetu kwenye vigodoro kwamba " UKIWA MUONGO USIWE MSAHAULIFU "
 
Tushauliza mara chungu nzima hapa kuhusu uthibitisho wa ufisadi wa Lowassa lakini hakuna anayekuja na majibu ya kueleweka kwahiyo hoja yako ya ufisadi haina mashiko
Uliwauliza kina Mbowe waliposema pale mwembeyanga?
 
Naona Mada Inazungumzia Wafanyabiashara,Kilicho Ndani Yake Sasa...Ahahaha!
Lowasa Sijuhi Ana Nini Huyu!
 
Unapokuwa na kikosi cha aina hii cha kukulinda na kukutetea kwa hoja za nguvu haina maana kuwa wewe ni mtawala wa nchi!

From here;
1.jpg


To here;
mbowe_Red%2BBrigade.jpg

DSC_0037.jpg

Hawa kwa sasa ndiyo walinzi wa Lowassa!

Lowassa is finished!

Tunajua anawaumiza vichwa sana ,kila linapokuja suala la kisiasa hasa likiuzungumzia upinzani lazima Lumumba7 mumshambulie Mzee wa watu utafikiri ni yeye pekee ndie alihama CCM na kuhamia Upinzani..Jengeni hoja acheni hadithi za Abunuwasi kila siku Lowasa hatuoni mkimfikisha mahakamani lakini haishi midomoni kwenu,hamna mambo ya kufanya kwani?
 
Naona kama vile bado sana ....Maaana topic inaongelea wafanyabiashara wa sukari lakini MTU anachangia kwa la Lowasa.......au lowasa nae muuza sukari
?????
 
Wanaomtetea Lowassa wana mamlaka gani ktk hii Nchi?

Kama CHADEMA wamefikia hatua ya kutoa protection kwa Lowassa na ikawezekana kama ulivyosema basi CCM si chama tawala tena bali CHADEMA ndiyo watawala.

Mimi wala sihangaiki kumtete kwa sababu hajawahi kupatikana na hatia. Naona nyie wapinzani wake mnapenda kumsemasema tu kwenye corridor za Lumumba wakati mna mamlaka ya kumkamata na kumfikisha mahakamani lakini hamfanyi hivyo. Tutawaamini vipi?
 
Naona kama vile bado sana ....Maaana topic inaongelea wafanyabiashara wa sukari lakini MTU anachangia kwa la Lowasa.......au lowasa nae muuza sukari
?????

Kuna watu siku hizi wasipomtaja lowassa hawapati usingizi. Wanatembelea nyota yake kila mahali.
 
Lowassa ni Icon ya ufisadi ni lazima atajwe ilivyo kwa Nyerere Icon ya uzalendo. Hivyo ni makosa kuacha kumtaja Lowassa popote unapojadili janga la ufisadi. Anasubiri Mahakama ya Mafisadi.
 
Back
Top Bottom