Wafanyabiashara wa Tanzania wazuiwa kutoa mahindi nje ya Zambia, Wafunga mpaka wa Tunduma

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,621
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mahindi kutoka Mikoa mbalimbali wamefunga mpaka wa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma mkoani Songwe kwa zaidi ya masaa mawili, kwa kuegesha magari yao, wakishinikiza serikali ya Tanzania kukaa meza moja na serikali ya Zambia, ili iwapatiwe mahindi yao zaidi ya tani 1,200 ambayo wamedai kununua kwa njia halali lakini yameshikiliwa kwa zaidi ya miezi mitano ,licha ya kuwa na vibali halali vya kununulia na kusafirishia mazao hayo kutoka nchini humo.

Akielezea tukio hilo na hatua zilizochukuliwa na serikali,, Mkuu wa wilaya ya Momba Bw. Fakii Lulandala ,amesema tayari serikali ya Zambia imewataka wafanyabiashara hao ambao wamenunua kihalali kuuza mahindi hayo ndani ya Zambia na si vinginevyo, huku akiwataka kuwa watulivu kwa kipindi hiki wakati suala hilo linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu.

1684913541878.png

Chanzo: ITV
 
Isije ikawa ni yale Wafanyabiashara wanayosema: Kuwa tozo huwa zinawafanya wapeleke bidhaa nchi za Jirani, halafu wanageuza na bidhaa hizo tena ili kukwepa kodi/tozo. Haya.

Ninasubiri kusikia mengine kwa shauku ndeeefu.
 
Back
Top Bottom