Prodigal Son
JF-Expert Member
- Dec 9, 2009
- 1,067
- 700
Wafanyabiashara wa kitanzania mnawaandaa watotowenu kuendeleza biashara zenu baada ya nyie kutangulia mbele ya haki?
Hili ni swala lakujadiliwa, kwani wafanyabiashara wengi ambao wamefanikiwa ila kinachosikitisha wanapoitwa mbele ya haki wengi biashara zao hazichukui muda zinakufa. Kwa kulijandili hili nawagawanya wafanyabiashara wakitanzaania kwenye makundi matatu
KUNDI LA KWANZA: Wale wafanyabiashara ambao wamefanikiwa wengine tena saana tu lakini hawana FORMAL eduacation. Kwenye hili kundi hili watu walijihitahidi na wengi walianza na biashara ndogondogo na kwa sasa wengi wana mabiashara makubwa na wengine wameenda mbali mpaka wamefungua biashara nje ya Tanzania.Wamejitahidi saana kwani ukiangalia background zao cha kusikitisha baadhi ya wafanyabiashara waliopo ndani ya hili kundi hawajali kuwaendeleza watoto wao kwa kuwapa elimu na ujuzi wakuendesha hizo biashara. Kuna baadhi wapo ndani ya hili kundi hata wake zao wenyewe hawajui biashara waume zao wanazofanya. (Mfano kuna mjasiriamali wa maduka kariakoo alipata ajali watoto bado wadogo mke alipoulizwa kuhusu mali za mume alikuwa anajua duka moja tu wakati mumewe alikuwa anamaduka matano na magorofa zaidi ya matatu).Ikumbukwe wengi waliopo ndani ya hili kundi wana mitaji mikubwa kiasi kwamba wangekuwa na elimu au kuwatumia Wataalamu wa biashara wangeweza kupanua biashara zai na kujikita kwenye kilimo, utalii, madini nk.kutakana na assert wanazomiliki wanaweza pata mikopo mikubwa saana ndani ya mabenki yetu ya kibiashara. Pia
KUNDI LA PILI: Hili linajumuisha Wanasiasa, Wasomi, na waliokuwa waajiriwa wa serekali ambao walihamua kuachana na kazi zao na kuhamua kuingia kwenye biashara. Linajumuisha waliokuwa ma CEO wa mashirika ya Umma yaliouzwa/kufa/na yaliyonunuliwa na wafanyakazi. Hili kundi bado ni dogo saana na wanajitahidi na kikubwa baadhi wanawaandaa watoto wao kwa kuwapa elimu na malezi mazuri kwa ajili ya kuja kusimamia biashara zao baada ya wao kuzeeka au kuitwa mbele yahaki. Kwakuwa hili kundi wanafanya biashara kisomi wanachangamkia fursa mbalimbali na wantoa ushindani mkubwa kwa wafnayabiashara wa kundi la TATU.
KUNDI LA TATU: Hili kundi linajumuisha wafanyabiashara Waasia/ wahindi ( naomba nisionekane mbaguzi). Ndani ya hili kundi wafanyabiashara wengi wamefanikiwa na wameridhi mitaji na biashara kutoka kwa Baba/babu zao. Mfano R M, Muhamed Dewgi na wengine lukuki.Hawa walipata upendeleo mkubwa saana tangu enzi za mkoloni na waliweza kutumia opportunities zilizokuwepo kwa uzuri kabisa. Jambo la uzuri kwao hawakuwekeza tu kwenye biashara ila waliwekeza na kwa watoto wao, waliwaandaa watoto wao ipasavyo kwa kuwapatia shule nzuri Ulaya na Marekani na kwa kiasi kikubwa watoto wao walipomaliza elimu pamoja na mbinu nyingine zikiwemo mbinu chafu kupanua biashara za wazazi wao na kuanzisha ma group of companies( mfano mzuri ni Sumaria, Muhamed enterprises etc). Hili kundi linasifika kwa kusaidiana na kupeana mbinu mbalimbali za kuendeleza biashara zao. Na ni wanyanyasaji wakubwa wa wafanyakazi na ni ngumu saana kufanya kazi kwao na kuweza kujiendeleza.
Hitimisho nini kifanyike kuondoa tatizo hili. Je tunaweza jenga biashara endelevu hata mwanzilishi wake kama hayupo biashara inabakia kuwepo na kuendelea? Hawa wajasiriamali ambao wameanzia mbali na kupata mafanikio makubwa lakini wanapokufa wanaondoka na biashara zao wasaidiweje tatizo ni mfumo au ni nini????.Je serekali inalitambua hili? Na taasisi kama Business school ya UDSM kitengo chake cha ujasiriamali wameshaliona hili????? Nini Jukumu la wafanyabiashara waliopo kwenye kundi la pili na la Tatu kuwasaidia wanzao wa kundi la kwanza???
Naamini wadau mkitoa mawazo yenu yanaweza yakatoa changamoto kwa hili tatizo