wafanyabiashara twendeni south sudan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wafanyabiashara twendeni south sudan

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by rosemarie, Jul 6, 2011.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  kuna nafasi nzuri za kibiashara nchini south sudan ambayo ni taifa jipya kabisa africa,
  nashauri watanzania tusilale twendeni tukaangalie uwezekano wa kuwekeza
  tumesikia taarifa kutoka bbc wakenya wanajaribu kufunga opportunity zote za nchi zingine
  bora kujaribu kuliko kufa maskini!!
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  sudan kusini inahitaji sana raslimali watu,tunaomba serikali ifanye jitihada za kupeleka watu wetu hasa vijana wasomi waliojazana barabarani
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  rosemarie

  je hali ya usalama ikoje huko .... bado kuna UN peace keepers ...?

  nafikiri bidhaa za vyakula inaweza kuwa biashara nzuri huko

  jana nilikuwa border ya Tanzania na Kenya, Tarakea aka Last ..... nimeona Fuso tano za vitunguu maji packed in mesh bags of 10kg vikivuka kuelekea kenya

  duh nimechoka kabisa .... hawa wakenya kiboko

  anyways ..... good idea mkuu
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  bbc wameongea na waziri wao wamesema wanaitaji watu wengi kufanya kazi mbalimbali,tutumie fursa hiyo kupeleka watu wetu,nafikiri usalama upo kwa sababu un wapo pale na marekani wana watu wao pale
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0

  kwa hiyo kinachohitajika hapa ni human resource na siyo kwenda kuwekeza na kufanya biashara...?

  je wanayo makampuni na viwanda vya kutosha kuajiri watu kutoka nje... yaani private sector ya ka nchi kapya kama haka inahitaji kuajiri watu kutoka nje ya nchi ... mimi nafikiri wanahitaji wawekezaji
   
 6. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wazo zuri lakini .. bado usalama haujatulia kule... kuna vita baridi ya wenyewe kwa wenyewe
   
 7. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kweli wadau nimesikia bbc wanaongelea hizo habari, kuna baadhi ya Watanzania wapo huko wamefungua maduka na jamaa zetu Wamasai wameishafika huko, bahati nzuri kiswahili kinatumika, wapemba wameishaanza kwenda
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Un na marekani watamwaga hela nyingi sana kule,nafikiri lazima kutakuwa na chance kubwa tuu za kutengeneza fedha,
  lakini nafikiri wanaitajika watu wenye roho ngumu wasiokubali kushindwa
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  wamewekeza kwenye maduka?? Maduka ya vitu gani?
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Maduka ya vifaa vya ujenzi, maduka ya vyakula pamoja nguo
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  tukumbuke kuna mafuta,usafiri unahitajika,malori,mabasi,wajenzi,computers,mafundi mbalimbali,mashirika ya kijamii,nafikiri na nafasi nyingi za kufanya biashara,
   
 12. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Nice idea mkuu, anayepanga kwenda kuangalia mazingira tujuzane wakuu.
  Thanx.
   
 13. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  hapa ndo ilipo tofauti ya Mkenya na Mtanganyika, wakati wewe unahimiza watu twende sasa wakenya walikuwa huku tangu hata hawajakubaliana kuhusu amani. Kuna opportunity nyingi saana na wakenya wanazishikilia karibu zote, ila ukumbuke kuna na challenge nyingi saana. mfano hawa wadinka wanafikiri wana haki ya kila kitu, ni kitu cha kawaida mtu kwenda hotelini anaagiza anachotaka na baadae anakataa kulipa ukiwauliza wanakumabia wanakula faida ya uhuru wao

  pia kuna swala la sheria, jeshi na hata polisi hawakona displine kabisa ukitofautiana na polisi au mjeshi anawweza kukulima risasi mara moja, Pia kama unataka kuwekeza unatakiwa uwe na mbia kutoka south sudan, japo kiafrica hili sio issue kubwa

  wakenya wengi wameajiriwa na mashirika ya misaada, wengine kampuni za kikenya kama KCB, na wanasaidiana kweli, wakenya wengine wamehamua kujinunulia maeneo makubwa saana ya Ardhi kwani huu udongo unarutuba kweli

  Kwa watanzania badala ya kujenga hizi hoteli sinza na kwingineko wangeweza kuzijenga JUBA na wangerudisha pesa zao very soon. Tatizo la watanzania wengi tunaogopa kuchukua maamuzi magumu, na hatujishughulishi kusaka taarifa, ndo maana tunapitiwa na hizi opportunities. nimesikia CRDB wanataka kufungua tawi BURUNDI hawa jamaa wangeenda SOUTH sudan naamini wangepata faida kweli,kama KCB ya kenya inavyo vuna pesa huku,
   
 14. Kishaju

  Kishaju Senior Member

  #14
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 106
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Ndugu kama kweli kuna watanzania ambao wako serious na wanataka kufanya biashara Juba tuwasiliane. Uwezi kuamini kazi zote za biashara zinafanywa na wageni kuna waganda, wa-ethiopia, wa-ertriea na wakenya wengi...kwa muda wote niliokaa hapa juba yapata mwaka mmoja nimeonana na mtanzania mmoja tu anayefanya biashara wengine waliopo ni kwenye UN na mashirikia mengine (NGOs). Karibu bar-maids wote ni kutoka kenya na uganda...vihoteli mshezi ambavyo kwa Dar unalipa 4,000 hadi 10,000 hapa waweza tozwa karibia dola 100 au zaidi kwa siku. Yale mahoteli ninayoyaona sinza yakiwa hapa una uhakika wa kupata hadi dola 150 kwa siku kwa kila chumba na unaweza ukakatu hakuna siku chumba kinakuwa wazi.

  Hivyo kama kuna yoyote yuko interested an-PM tuongee zaidi....

  Maeneo ambayo naona yanapotential kubwa ni haya
  a) Biashara ya usafirishaji toka ndani na within South Sudan.
  b) Biashara ya mazao kama mahindi, mchele, vitunguu na mafuta ya kupikia.
  c) Kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji- hapa watu hawalimi sana
  d) Biashara ya vituo vya mafuta
  e) Biashara ya garage - hasa kufanya matengenezo ya magari yaliyopata ajari
  f) Biashara ya mahoteli na kumbi za starehe - kwa mfano ukianzisha sehemu nzuri na kubwa ukaweka runinga kubwa nyingi na ACs kwa ajili ya kuangalia mechi za UK etc basi hapo waweza pata pesa kibao.
  e) Biashara ya appartments - hapa nyumba zina uhaba mkubwa sana kwa kweli especially for international staff. Nyumba uwezi pata chini ya dola 2,500 au 3,000 na hakuna quality kabisa. Ukiweza wekeza kwenye apartment nzuri kwa mfano 4 units of 2 bedrooms, kitchen, sebule etc unaweza pata pesa nzuri.

  Changamoto kubwa ninayoiona ni upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kwa gharama nafuu....

  Haya ndugu zangu, kama unajiona kwamba uko tayari kufanya utafiti wa kuwekeza juba na sehemu zingine za South Sudan tuwasiliane basi.
   
Loading...