Wafanyabiashara Matapeli mitandaoni hubadili Usernames baada ya kupiga tukio

Wafanyabiashara Matapeli mitandaoni hubadili Usernames baada ya kupiga tukio

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,217
Reaction score
3,796
Moja ya ishara kubwa ya kurasa za utapeli mtandaoni ambayo watu wengi hawaistukii ni tabia ya kubadilisha majina ya akaunti zao mara kwa mara.

Matapeli wakishawadhulumu watu na jina lao kuanza kuchafuka mtandaoni, hawafuti akaunti; badala yake, wanabadilisha tu jina la ukurasa, picha ya wasifu (profile picture), na maelezo ya juu (bio) ili kuwawinda wahanga wapya bila kushtukiwa.

Nenda kwenye ukurasa wa duka husika.

1. Bonyeza vidoti vitatu (...) vilivyopo juu kulia mwa ukurasa.

2. Chagua "About This Account" (Kuhusu Akaunti Hii).

3. Bofya "Former Usernames" (Majina ya Awali). Ukikuta ukurasa umebadilisha majina mara tano au sita ndani ya miezi michache, Shtuka

Ushauri wa bure: Biashara makini inayojenga chapa (brand) thabiti haibadili jina kila kukicha. Ukiona jina linacheza kama kinyonga, mfuko wako upo hatarini!

Stori fupi.........
Kuna rafiki yangu alikuwa anahitaji Laptop, nikamshauri asinunue online bali aende kwenye duka husika ili aweze kupata nafasi ya kuona na kupewa maelekezo ya aina ya Laptop inayomfaa kulingana na budget yake pamoja na matumizi.

Jamaa akaona haina nma hata online anaweza ku-purchase nakufanyiwa delivery, kiufupi ni aina ya watu wasiopenda kutembea. Akasearch Instagram akakutana na page inauza laptops na ina followers kibao ikawa kigezo cha yeye kujenga imani nayo.

Akawacheki then wakakubaliana cha ajabu akaambiwa atume hela ili afanyiwe delivery kitu ambacho ni red flag ya kwanza, jamaa bila kuchelewa akatuma red-flag ya pili namba haina hata jina la duka maana sikuzi for trust issue wafanyabiashara husajili line kwa majina ya duka ili mteja anapofanya transaction anaona ndo duka lenyewe.

Baada ya malipo majamaa hawakupatikana tena akisearch lile jina halipo
na tayari hela imeenda.
 
Ukiona jina la mtu binafsi kwenye namba ya malipo ujue unajipeleka mwenyewe kutapeliwa.
 
Back
Top Bottom