Wafahamu kwa uchache "Madada Poa" wa Barabarani

Wafahamu kwa uchache "Madada Poa" wa Barabarani

Nusratt

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
1,707
Reaction score
4,192
Habari za jioni wapendwa wana Jf (JamiiAfrica )
Natumaini mko salama na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku.

Lengo la kuleta uzi huu usiku huu ni kuona kwa namna gani hii biashara ya ukahaba ilivyo enea na jinsi inavyofanyika.

Hii biashara nina uzoefu nayo kwa muda wa miaka 15.
Najua A to Z kuhusu hii kazi.
Na kama kuna kitu nitakuwa nimekiruka katika simulizi hii, basi ni ruksa kuongezea.

Ukahaba ni nini?
Ukahaba ni aina ya kazi ya ngono inayohusisha kushiriki ngono ili kupata malipo.

Kahaba ni nani?
Kahaba ni mtendaji ngono anayepokea malipo baada ya tendo.

Sasa basi, tumeshaona na kufahamu maana ya ukahaba na kahaba.

Tuje kwenye mada husika.
Wapo watoa huduma wengi wa ngono katika hii dunia.
Kuanzia watoto, rika maalum, vijana, watu wazima mpaka wazee na wote hawa hutoa huduma kulingana na mapatano yao.

Wapo wanaotoa huduma ya ngono kwa lengo la kupata pesa, mitaji, nyumba, gari, biashara, nguo, viatu, lifti, vyakula n.k

Na katika makundi haya ya watoa huduma wapo pia aina mbali mbali za watoa huduma.
Kuna wamama wa nyumbani, wafanyakazi wa maofisini, walimu, wanafunzi, wafanyabiashara n.k wote hao hutoa hii huduma kulingana na mazingira aliyopo.

Leo nitazungumzia kundi moja tu la watoa huduma hii ya ngono, wenyewe wanajiita "watu wa road" au kiufupi wale wanaosimama barabarani katika kujiuza.

Kundi hili la wanaosimama barabarani kwanza jamii nyingi inaona ni kama vile wamepinda na maisha au tuseme ni kama wametoa maisha yao sadaka/rehani kwa lolote lile litakalokuja mbele yao.

Imagine umesimama road na anakuja mteja mwenye gari unaongea nae bei kisha unaondoka nae, humjui huyo mteja na wala hujui kama ni mwema au lah!

Kisha mnamaliza mambo yenu huko na unarudi salama 'kijiweni', ni Mungu tu anakulinda.

Zipo kesi nyingi sana za wadada wa road kupotea au kuuliwa na wateja wao huko walikopelekwa.
Na pia wapo wadada waliowaua wateja wao hukohuko walikopelekwa na wateja wao.
Kwahiyo hapa ni kama wanaviziana.

Siri ya "wadada wa road"
Wadada wengi wa road ni lazima wawe wavutaji wakubwa wa sigara au bangi. Piga ua ukikuta mdada wa road havuti sigara huyo bado mgeni.

Unywaji wa pombe pia ni kipaumbele cha wadada wengi wa road bila kusahau pombe kali.

Wanawake wa road ndio kundi la madadapoa linaloongoza kwa kurogana, hii hutokana na kurundikana sehemu moja hivo ni lazima 'uroge' ili uvutie wateja.

Pia ndio kundi linaloongoza kwa kuwaibia wateja wao.
Piga ua galagaza, ukienda kwa wadada wa road jipange kisawasawa.
Nenda na pesa kamilli ya huduma.
Ni lazima ulizwe vibaya mno.

Pia usisahau ndilo kundi la madadapoa linaloongoza kwa kuwa na maambukizi ya Ukimwi na magonjwa hatari ya ngono kutokana na aidha kupasuka kwa condom wakati wa tendo au kufanya ngono peku kwa ahadi ya kuongezewa pesa zaidi

Ndio kundi linaloongoza kwa kufanya ngono za bei rahisi.
Si ajabu kukuta mdada hajapata hata pesa ya nauli tangu kaingia road usiku, hvo akija wa alfajiri wa 2000 au 1500 hawezi kataa.

Pia kundi hili ndilo huongoza kwa uchafuzi wa mazingira kwa kusambaza hovyo mipira ya kiume iliyotumika mitaani. Kwani hawana sehemu maalumu ya kufanyia kazi popote pale hupatana na kuingia kazini na wakimaliza huacha uchafu wao hapo

Pia vilevile usisahau ndio kundi linaloongoza kwa kulea ving'asti hasa bodaboda ili kupata unafuu wa usafiri pale wanapokuja kukimbizwa aidha na askari au mgambo usiku.

Ndio kundi linaloongoza kwa kuvaa nusu utupu.
Nadhani mshawahi jionea.

Pia vilevile majimaji ya kiume (shahawa) huuzwa kwa wahitaji kwa ajili ya mambo yao ya ushirikina.
Baada ya tendo, mipira ya kiume yenye manii ni biashara nzuri sana.
Siku hz wanaume wengi huomba kuondoka na mipira yao baada ya tendo.

Ni nadra sana kwa dada wa road kwenda site yake ya kazi bila silaha mkobani au kwenye maziwa.
Visu vidogo, nyembe, bisibisi au hata unga wa pilipili hutumika sana kama silaha pale anapotokea mteja mkorofi au mteja mwizi.

Pia usisahau kundi hili la road ndilo huongoza kwa kutembea na madawa ya usingizi.
Naweza paka mgongoni ukiniinamia tu, umeisha.
Hii ndio ipo kwa sasa.

Ngoja niwape siri, usidhani wale wanaume woote wanaotufuata tunafanya nao ngono hapana.
Wengi huishia kumwaga kwenye mapaja au mkononi.

Usijaribu na usithubutu kumnyonya kahaba yeyote sehemu yake ya mwili, utalia.
Fanya kilichokupeleka pale.
Ukimaliza, nawa au oga kisha ruhusu aondoke au wewe uondoke.

Usimdhulumu dadapoa ujira wake kama mlivyokubaliana.
Mlipe kadri ya makubaliano yenu.
Na usikubali akufute sehemu za siri na kitambaa, mwambie atumie tishu.
Hili somo la kwanini tishu na si kitambaa ni la siku ingine.

La mwisho, pia ndio kundi la dadapoa ambao wengi wapo 'kazini'
Nadhani umenielewa ninaposema kazini.
Usidhani wale wote ni dada poa bali wengine huja kwa 'msimu' na kuondoka baada ya kumaliza jambo lao.

Ila la mwisho kabisa, hii biashara ya ukahaba ipo tangu karne na karne.
Na iko chini ya milki za watu na maisha yao.
Kuizua ni ngumu sana.
Cha umuhimu ni kutulia na ndoa yako.

Fanya ngono salama.
UKIMWI upo na Unaua.
Tumia kondomu kiufasaha.

Niliposahau mnikumbushe.

Wabillahi Tawfiq
Alamsiki.

KIKWAGIZO
Screenshot_20250510_172056_WhatsApp.jpg
 
Pia vilevile majimaji ya kiume (shahawa) huuzwa kwa wahitaji kwa ajili ya mambo yao ya ushirikina.
Baada ya tendo, mipira ya kiume yenye manii ni biashara nzuri sana.
Siku hz wanaume wengi huomba kuondoka na mipira yao baada ya tendo.
Hii inajulikana sio wanaojiuza tu hata michepuko inafanya hii kitu kwa hio hakuna kwa kuponea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom