Mbunge aishauri Serikali jinsi ya kudhibiti Watoto wanaochezea Kondomu Mwanza

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,538
8,548
Mbunge wa Ilemela (CCM), Dk Angelina Mabula ameitaka Serikali kujenga uzio katika Shule ya Msingi Kitangili iliyopo mkoani Mwanza ili kuokoa maisha ya watoto wanaochezea kondomu katika uwanja wa mpira.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Jumanne Aprili 23, 2024, Dk Mabula amesema eneo hilo lenye shule mbili nyakati za usiku limekuwa likitumiwa na dada poa na lipo katika uwanja wa CCM wa Kirumba.

“Ni lini Serikali itaweka uzio ili kuokoa maisha ya watoto ambao wanachezea mipira (kondomu), “amehoji Dk Mabula.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala Bora na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Zainab Katimba amemkumbusha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela kwenda katika shule hiyo na kufanya tathmini.

“Kama alivyozungumza mheshimiwa mbunge kuna kila sababu ya halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kutenga fedha ili kunusuru na kutengeneza mazingira bora ya wanafunzi hao,” amesema.
 
Kinachofanyikaga maeneo hayo ni zaidi ya Ufirauni,,,, hatua za haraka inabidi zichukuliwe kuwanusuru hao watoto.
Na uke mawenge uzuiwe kwenye mikesha ya mawenge maccm hapo ndio yanapofanya ufirauni wao asubuhi unakuta condom za kutosha.
 
Huyo mbunge aliwaona lini wanafanya huo mchezo?
Baada ya kuzungumza mambo muhimu yeye anazungumzia majani.
Majani hataathiri zaidi ya matawi na mashina.
 
Tuache watoto wacheze, Michezo ni Afya tena hasa wanavyotumia condom.
Screenshot_20240208_205614_Chrome.jpg
 
Ila wasukuma bna...sasa vitoto vidogo vimeanza nusa nusa condoms alafu wakija pewa nchi wanakuwa wehu kumbe uwehu wameanza muda mrefu...
 
Mbunge wa Ilemela (CCM), Dk Angelina Mabula ameitaka Serikali kujenga uzio katika Shule ya Msingi Kitangili iliyopo mkoani Mwanza ili kuokoa maisha ya watoto wanaochezea kondomu katika uwanja wa mpira.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Jumanne Aprili 23, 2024, Dk Mabula amesema eneo hilo lenye shule mbili nyakati za usiku limekuwa likitumiwa na dada poa na lipo katika uwanja wa CCM wa Kirumba.

“Ni lini Serikali itaweka uzio ili kuokoa maisha ya watoto ambao wanachezea mipira (kondomu), “amehoji Dk Mabula.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala Bora na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Zainab Katimba amemkumbusha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela kwenda katika shule hiyo na kufanya tathmini.

“Kama alivyozungumza mheshimiwa mbunge kuna kila sababu ya halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kutenga fedha ili kunusuru na kutengeneza mazingira bora ya wanafunzi hao,” amesema.
Hilo eneo lipo karibu na kituo cha polisi, cha kushangaza polisi wanawasarandia msimu WA sikukuu peke ake,
Wadada wanaojiuza wengine wamepanga hapo Anntonnio logde.

Polisi wa Kirumba washenzi sana.
 
Duuuh napajua watu wanafanya mapenzi kama wanyama hakuna Cha kitanda wao ni kuinamiahana tu dadek. Anyway serikali itume polisi wakamate hao wauzaje na wateja wao
 
Back
Top Bottom