Waelewe Watu kupitia Miti

Joe Navarro

JF-Expert Member
Aug 22, 2022
1,475
3,063
AINA 3 ZA WATU KATIKA MAISHA YAKO..

1. Watu Majani
2. Watu Tawi
3. Watu Mizizi

Watu Majani:
Hawa ni watu ambao wanakuja katika maisha yako kwa msimu tu. Huwezi kuwategemea kwa sababu ni dhaifu. Wanakuja kuchukua tu wanachotaka, lakini upepo ukija wataondoka nao.

Unatakiwa kuwa makini na hawa watu maana wanakupenda mambo yakiwa sawa ila yakienda kombo huenda na wao huenda na pepo zinazo vuma.

Watu Tawi:
Wana nguvu, lakini unahitaji kuwa mwangalifu nao pia. Wanaachana nawe wakati maisha yanapokuwa magumu ( Unapokuwa na ukame au kukaukiwa ) na hawawezi kuhimili unayopitia kwa muda wote. Wanaweza kukaa na wewe katika baadhi ya misimu, lakini wataenda zao pale hali inapokuwa ngumu zaidi.

Watu Mizizi:
Watu hawa ni muhimu sana kwa sababu hawafanyi mambo ili waonekane. Wanakuunga mkono hata ukipitia wakati mgumu watakunywesha maji na hawaguswi na msimamo wako wanakupenda hivyo hivyo...

Sio watu wote unaokutana nao au ni marafiki zako, watabaki na wewe.
Ni aina ya mizizi tu ya watu itabaki bila kujali msimu na mara nyingi huwa wachache zaifi.

Je, ulishafahamu Aina za marafiki ulionao Sasa hata wale wapya ?


Usisahau Kulima na Bashe
FB_IMG_16898943886235437.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom