Wadhamini Kikwete 14,069; Slaa 1.3 million | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadhamini Kikwete 14,069; Slaa 1.3 million

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Freetown, Aug 8, 2010.

 1. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Haya ni maneno ya Makamba wakati Kikwete akirudisha form ya kugombea uraisi
  Kwa miaka mitano umeonesha umahiri mkubwa, na nataka kukuambia kazi ya kukurudisha Ikulu ina wenyewe. Nawaambia wenzangu Rais wa Jamhuri ya Muungano ni Jakaya,” alisema na kuongeza kuwa uthibitisho mwingine ni wadhamini 14,069 aliowapata wakati alitakiwa kuwa nao 2,500 tu.
   
 2. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Slaa kapata wadhamini 1,300,000 taarifa za habari za vyombo makini
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Makamba, Katibu Mkuu wa CCM! Kazi kwel kwel
   
 4. senator

  senator JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ikifika wakati wa kupiga kura sijui kama zitafika hiyo number ya wadhamini aliopata...
   
 5. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hesabu kamili ni hii:-
  Dk. Slaa ambaye hadi jana asubuhi alikuwa ameshadhaminiwa na Watanzania 1,397,757 kutoka mikoa 20 Tanzania Bara na Visiwani, alikuwa akitokea Zanzibar alikokwenda kutafuta wadhamini, akiwa ameambatana na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ambapo aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere majira ya saa 6:50 mchana na baadaye kuhutubia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika viwanja vya Jangwani.
   
 6. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nadhani suala la awadhamini sio la kulipa kipaumbele sana, inawezekana timu ya CCM ilitafuta wadhamini bila kuweka kichwani mwao kuwa idadi itakuja kulinganishwa mahali au na ya chama kingine, Otherwise nashawishika mgombea wa CCM angeenda kutafuta wadhamini yeye mwenyewe na kuhutubua mikutano kama Mgombea wa CHADEMA hali ingekuwa tofauti kidogo.
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  CCM wanazipigia mahesabu hizo 1.3m waziibe, umesahau kura za wadhamini wa CCJ zilivyoyeyuka, lakini mwaka huu kazi itakuwa pevu hata kuiba lazima wajiandae kwa lolote ikiwa ni pamoja na majeshi.
   
 8. senator

  senator JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  This time mkwere anataka kushinda kwa kishindo zaidi so watafanya fitina zote ili Lengo lao litimie..wasimamizi wengi wa vyama vya upinzani njaa kali inakuwa rahis sana kupigwa bao kwa cent kidogo tu...Ndo mana 2005 baada ya kampeni ndefu ya Mbowe na kutumia helikopta akaishia kuw watatu na kusema anaona watanzania hawakumwelewa...Ngoja tuone kwa slaa itakuwaje
   
 9. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Asilimia 60% au zaidi ya watanzania hawana elimu ya kupambanua mambo, mimi nawewe tuliye bahatika kupataa mwanga kidogo kama huu nijukumu letu kuhakikisha tunawajuza haya mambo, hata kama ccm wataiba lakini tutakuwa tumetimiza waajibu wetu kama watu tuliotumwa na sehemu zetu vijijini kuwapelekea neema ya uelewa.

  Najua ccm watatumia gharama yeyote ile warudi lakini kazi ipo mwaka huu, lazima ziwatoke kweli kweli. Nabado watu wengi watapiga kura mwaka huu, walioamua kupiga kura wote ni kwa sababu wamechoka na hizi tabia chafu za kujineemesha kama kwamba wao ndo wenye nchi pekee yao.
   
 10. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,pamoja na ukweli kwamba JK na mafisadi wake watafanya kila jitihada kung'ang'ania madarakani,jambo la faraja ni kwamba USHIRIKA WA WACHAWI HAUDUMU.This time,and perhaps for the first time ever,CCM inakumbana na mgombea makini.Hilo linawapa hofu na tayari kuna dalili za kupanick kwa namna flani.Lakini habari njema zaidi ni possibility ya wao kwa wao kufanyiana ufisadi.Wengi tunakumbuka namna fedha za EPA zilivyoibiwa kwa minajili ya kumsaidia JK lakini mafisadi wakapiga panga la haja.Kilichomsaidia JK ni sapoti ya Mkapa ambaye wakati huo alikuwa rais (hakufanya hivyo kwa mapenzi yake bali shinikizo).Sasa,kwa kipindi hiki JK ana kazi mbili kubwa:moja,kuhakikisha anashinda uchaguzi na kubaki madarakani,na pili,anatengeneza mazingira ya kumnusuru pindi "kura zisipotosha".Wanaweza kuchangishan fedha za kutosha lakini zikaishia mifukoni mwa mafisadi,ambao nao wanahangaishwa na mambo mawili:kuhakikisha JK anabaki madarakini ili azidi kuwalinda na pia wanajijengea mazingira ya "kujinusuru" pindi upepo ukienda vibaya.

  Tunaweza kupata ahueni kutoka kwenye mwenendo wa kura za maoni ndani ya CCM ambapo yayumkinika kuhitimisha kuwa ya RUSHWA ya msimu huu ni ya KIHISTORIA.Japo Dkt Slaa ana muda mfupi kujitengenezea mazingira ya ushindi mkubwa,JK naye ana kazi ya ziada ya kutuliza mzuka wa walioangushwa ndani ya CCM...hususan wale waliomwaga mamilioni yao ya kifisadi na kuambulia patupu.Je hatuwezi kubashiri kuwa baada ya CCM kupitisha majina ya wagombea wake kukatokea kizaazaa cha aina yake?

  Wakati jukumu kubwa la JK na wapambe wake lingepaswa kuwa ni kumdhibiti Slaa tu,limejitokeza jambo jingine la dharura la kuwadhibiti "wahanga" wa process ya uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya CCM.Na kwa udhaifu wa JK,hasira za kushindwa za watu kama Malecela,kutanguliza maslahi binafsi kwa mafisadi wenye sauti ndani ya CCM,kuna uwezekano mkubwa wa Dkt Slaa kufanya vizuri kwenye uchaguzi huo.

  By the way,lolote linawezekana katika siasa.
   
 11. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Unasahau ukweli kuwwa Kikwete wa 2005 si wa 2010. Amechuja sana
   
 12. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Acheni kudanganyana, hata Dr.Slaa mwenyewe anamkubali JK. Tatizo la watanzania ni kusukumwa na matukio lakini si uhalisia, we have seen since Mrema, for sure people must change their altitudes towards political analysis otherwise we will remaim bleming because of our fault. JK hatashinda kwenye vyombo vya habari, kwa wananchi the guy is going to become the winner for 2010. Na si kweli Tz hajawahi tokea mgombea makini kama Dr. Slaa, issue ni aina ya watu wanaoshiriki uchaguzi.
   
 13. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kachuja sana kwa riferensi ya gani? kachuja sana kwa group lipi? je amechuja kwa wapiga kura wote tz? au baadhi ya watu? tukishapata hakika hii may be utasaidia kujua mchujo huo una impact gani kwa uchaguzi wa 2010?
  mix with yours
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  WADHAMINI 1.3M SI HABA........gawanya kwa mbili utapata idadi ya kura....!
   
 15. a

  ally mkali Member

  #15
  Aug 8, 2010
  Joined: Sep 27, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Idadi ya wadhamini si oni kama ni issue ya msingi. Ushauri wangu wa msingi kwa uma wa tanzania tumpigie kura dr. Slaa kwa wingi sana pamoja na wabunge wengi wa upinzani ili bunge letu liweze kuwa la ukweli na hakika d. Slaa this time hatoweza kumuangusha raisi kikwete lakini tukiwa na wabunge wengi wa upinzani ndani ya bunge hali ya wenyewe ccm kufanya maamuzi yakutuumiza watanzania hayata kuwepo. Tusiwe washabiki kamwe haito tusaidia., tufanye kweli
   
 16. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Asante kwa ujumbe wako. [FONT=&quot]WAPINZANI WANAPASWA KUELEWA kuwa wakati huu ni wa Dk. Slaa katika kambi yao. Ingawa ni haki ya kikatiba kwa wapinzani wengine kugombea urais, bado wanapaswa pia kuelewa ukweli huu. Mimi ningeshauri wamuunge mkono Slaaa kama kweli wanaliona hilo. KWA UPANDE WA CCM WAKAE CHONJO MAANA MAMBO HAYATAKUWA KAMA WALIVYOZOEA SIKU ZA NYUMA. mechi haitakuwa sawa na Taifa Stars dhidi ya Brazil bali kati ya Ujerumani na Hispani sijui kama wanaweza kumruhusu Pweza atabiri matokeo![/FONT]
   
 17. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  PWEZA KESHAITABIRIA CHADEMA KUIBUKA KIDEDEA..............!azim dewji alitoa dau kama vitu kama hivi vinaweza kutoa ushindi!
   
 18. M

  Mutu JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hayo ndio mahesabu gani bwana mahesabu .......?
  mbona unatia aibu accept the reality .
   
 19. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Idadi ya wadhamini sio jambo la kujivunia, suala muhimu ni kura atakazozipata mgombea mwezi October.
   
 20. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Hatutakuwa wakweli kama tutataka kufanya kama vile udhamini wa Dr Slaa wa zaidi ya watanzania milioni 1 haina maana. Kw ahili Chadema imeshweka historia na itakumbukwa kwa vizazi vijavyo regardless of the final results. Vivyo hivyo kwa mikutano yake mikubwa katika mikoa mbalimbali iliyovuta maelfu ya wananchi. Kama CCM itaendelea kubeza matukio haya basi watajikuta kama Hillary Clinton Marekani ambaye alijiamini kupindukia na alikuja kushtukia too late kwamba mwenzake ameshampita. Ila kutokana na arrogance ya Kikwete camp, sidhani kama mtakuwa tayari kushauriwa kwa hiyo hata wenye uwezo wa kuwapa ushauri wa maana watakaa pembeni au wataenda kuishauri kambi ya upinzani...
  :wave:
   
Loading...