Wadau wa habari wamshukia Dkt. Abbas, wadai hakumuelewa Rais Samia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,230
2,000
Wakati Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbas akidai Rais Samia Suluhu Hassan alivyotamka vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe hakumaanisha magazeti yaliyofungiwa, wadau mbalimbali wamemshukia kwamba hakuielewa kauli ya kiongozi mkuu huyo wa nchi.

Dk Abbas alitoa kauli hiyo jana Jumanne Aprili 6, 2021 wakati akihojiwa na televisheni ya Wasafi saa chache baada ya Samia kuagiza vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa katika hafla ya kuwaapisha makatibu wakuu na manaibu wao iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“...,lakini ni kusimamia vyombo vyetu vya habari ndani, nasikia kuna vyombo vya habari mlivifungia fungia sijui vi televisheni vya mkononi vifungilieni lakini wafuate sheria na miongozo ya serikali. Tusiwape mdomo wa kusema tunabinya uhuru wa vyombo vya habari lakini mhakikishe kila mliyempa ruhusa ya kuendesha chombo cha habari anafuata sheria za serikali na kanuni ziwe wazi kosa hili adhabu yake hii..., tusifungie tu kibabe tuhakikishe wanafuata kanuni,” alisema Samia.

Wakati wadau wakimshukia Dk Abbas, jana taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya rais Ikulu ilieleza kuwa kiongozi mkuu huyo wa nchi ameagiza vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe na kutakiwa kuzingatia sheria.

Katika mahojiano hayo, Dk Abbas alisema agizo hilo liligusa vyombo vya habari vya mtandaoni pekee na kwamba magazeti hayahusiki akisisitiza kuwa iwapo rais ataagiza magazeti yaliyofungiwa yafunguliwe watalifanyia kazi hilo.

“Rais alizungumzia kuhusu vyombo vya habari vya mtandaoni na unafahamu kuwa amefanya mageuzi kule TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) kwa hiyo tutakwenda kuangalia ni vyombo vipi vilifungiwa na kutokana na sababu zipi kisha tutachukua hatua kama alivyoelekeza Rais.”

“..., kwa hiyo tutalifanyia kazi hilo lakini kama kuna maelekezo mengine sisi ni watekelezaji tunatekeleza. Rais amesisitiza vyombo vya habari kuendelea kuzingatia maadili na sheria za nchi lakini kwa hili agizo alilolitoa tunakwenda kuchukua hatua mara moja,” amesema.

Muda mfupi baada ya kauli hiyo wadau hao walitumia mitandao ya kijamii ya Twitter na Instagram kumshukia Dk Abbas wakidai kuwa katibu mkuu huyo ndio hakuelewa alichokieleza Samia.

Katibu mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema, “uamuzi wa Dk Hassan Abbas kulipa tafsiri finyu agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kufunguliwa kwa vyombo vya habari akidai hajaagizwa kufungulia magazeti ni online Tvs tu ni dalili kuwa kichwani kwake bado anaishi zama za...,”

“Katika muktadha ambao Rais Samia alikuwa anazungumzia uhuru wa vyombo vya habari Dk Abbas alipaswa kuchukulia Online Tv kuwa ni mfano tu wa vyombo vingi vya habari vilivyofungiwa.”

Deodatus Balile ambaye pia ni mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ameandika, “Dk Hassan Abbas sijakusikia vizuri. Unasema Rais hakuagiza mfungulie Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima?”

“Isikilize tena hotuba ya mama au unataka kuwa wa kwanza kuzinguana, Asante sana Mheshimiwa Rais, Mama Samia kuagiza vyombo vya habari vifunguliwe.”

Katibu wa jukwaa hilo, Neville Meena amesema Dk Abbas bado ana hamu ya kuendelea kufungia magazeti kwa kutafsiri maelekezo ya Rais Samia.

“Eti amri yake inahusu kufunguliwa kwa online tv tu, ndugu yetu huyu hajifunzi,” amesisitiza Meena.

Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema amesema, “ni kweli uhuru wa vyombo vya habari ni haki yetu na sio kwa hisani ya watawala, lakini pia dhamira ya mtu sio haki yetu. Hivyo tunapoona dalili za dhamira njema kwa mtu ni vyema tukatambua kwa sauti kuu kwani roho nzuri Tanzania imekuwa bidhaa adimu kati ya mwaka 2015 hadi 2020.”
 
haszu

JF-Expert Member
Oct 10, 2017
747
1,000
Mambo 3 :
1. bado anahisi yuko katika ule utawala wa mabavu na sifa za kijinga
2: anahasira kutolewa kua msemaji mkuu
3: anakiburi na anamdharau Mama
 
  • Thanks
Reactions: Lee

captain 21

JF-Expert Member
Mar 27, 2021
209
500

Ngoja tuendelee kuusoma mchezo..
 
3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
3,299
2,000
Naona anapigwa kila upande huyu Dr yaani ina maana watu woote hawakumuelewa Rais isipokuwa yeye tu eti ni online tv tu zilizoruhusiwa..
 
Lee

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
37,263
2,000
Ata mimi na darasa la saba c nilimuelewa mama vizuri ...iweje huyu
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
52,280
2,000
Rais Samia anavyosema hataki serikali iwe na shutuma kuwa inabinya vyombo vya habari intention yake ni kufungulia vyombo vyooote vilivyofungwa kibabe including news paper ili serikali isiwe kwenye kashfa ya kuonea vyombo vya habari.

Sasa huyu Abbas anajiita mwanasheria alafu anatafsiri kauli ya mkuu wa nchi kama kasuku pori. Pambaf.
 
Biggs

JF-Expert Member
May 3, 2014
482
500
Wakati Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbas akidai Rais Samia Suluhu Hassan alivyotamka vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe hakumaanisha magazeti yaliyofungiwa, wadau mbalimbali wamemshukia kwamba hakuielewa kauli ya kiongozi mkuu huyo wa nchi.

Dk Abbas alitoa kauli hiyo jana Jumanne Aprili 6, 2021 wakati akihojiwa na televisheni ya Wasafi saa chache baada ya Samia kuagiza vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa katika hafla ya kuwaapisha makatibu wakuu na manaibu wao iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“...,lakini ni kusimamia vyombo vyetu vya habari ndani, nasikia kuna vyombo vya habari mlivifungia fungia sijui vi televisheni vya mkononi vifungilieni lakini wafuate sheria na miongozo ya serikali. Tusiwape mdomo wa kusema tunabinya uhuru wa vyombo vya habari lakini mhakikishe kila mliyempa ruhusa ya kuendesha chombo cha habari anafuata sheria za serikali na kanuni ziwe wazi kosa hili adhabu yake hii..., tusifungie tu kibabe tuhakikishe wanafuata kanuni,” alisema Samia.

Wakati wadau wakimshukia Dk Abbas, jana taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya rais Ikulu ilieleza kuwa kiongozi mkuu huyo wa nchi ameagiza vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe na kutakiwa kuzingatia sheria.

Katika mahojiano hayo, Dk Abbas alisema agizo hilo liligusa vyombo vya habari vya mtandaoni pekee na kwamba magazeti hayahusiki akisisitiza kuwa iwapo rais ataagiza magazeti yaliyofungiwa yafunguliwe watalifanyia kazi hilo.

“Rais alizungumzia kuhusu vyombo vya habari vya mtandaoni na unafahamu kuwa amefanya mageuzi kule TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) kwa hiyo tutakwenda kuangalia ni vyombo vipi vilifungiwa na kutokana na sababu zipi kisha tutachukua hatua kama alivyoelekeza Rais.”

“..., kwa hiyo tutalifanyia kazi hilo lakini kama kuna maelekezo mengine sisi ni watekelezaji tunatekeleza. Rais amesisitiza vyombo vya habari kuendelea kuzingatia maadili na sheria za nchi lakini kwa hili agizo alilolitoa tunakwenda kuchukua hatua mara moja,” amesema.

Muda mfupi baada ya kauli hiyo wadau hao walitumia mitandao ya kijamii ya Twitter na Instagram kumshukia Dk Abbas wakidai kuwa katibu mkuu huyo ndio hakuelewa alichokieleza Samia.

Katibu mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema, “uamuzi wa Dk Hassan Abbas kulipa tafsiri finyu agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kufunguliwa kwa vyombo vya habari akidai hajaagizwa kufungulia magazeti ni online Tvs tu ni dalili kuwa kichwani kwake bado anaishi zama za...,”

“Katika muktadha ambao Rais Samia alikuwa anazungumzia uhuru wa vyombo vya habari Dk Abbas alipaswa kuchukulia Online Tv kuwa ni mfano tu wa vyombo vingi vya habari vilivyofungiwa.”

Deodatus Balile ambaye pia ni mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ameandika, “Dk Hassan Abbas sijakusikia vizuri. Unasema Rais hakuagiza mfungulie Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima?”

“Isikilize tena hotuba ya mama au unataka kuwa wa kwanza kuzinguana, Asante sana Mheshimiwa Rais, Mama Samia kuagiza vyombo vya habari vifunguliwe.”

Katibu wa jukwaa hilo, Neville Meena amesema Dk Abbas bado ana hamu ya kuendelea kufungia magazeti kwa kutafsiri maelekezo ya Rais Samia.

“Eti amri yake inahusu kufunguliwa kwa online tv tu, ndugu yetu huyu hajifunzi,” amesisitiza Meena.

Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema amesema, “ni kweli uhuru wa vyombo vya habari ni haki yetu na sio kwa hisani ya watawala, lakini pia dhamira ya mtu sio haki yetu. Hivyo tunapoona dalili za dhamira njema kwa mtu ni vyema tukatambua kwa sauti kuu kwani roho nzuri Tanzania imekuwa bidhaa adimu kati ya mwaka 2015 hadi 2020.”
Maelezo yalikuwa straight forward na yanaeleweka.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
9,720
2,000
Abbas ni tatizo kubwa sana kwa upande wa uhuru wa vyombo vya habari, hakupaswa kuendelea kukikali hicho kiti chake alipo kwa sasa labda falsafa ya mchawi mpe mwanao amlee imetumika.
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,383
2,000
Kuoneawa ni kuonewa tu..., Issue hapa sio online wala offline issue ni kila aliyeonewa afunguliwe...., na sababu tumeona hapo nyuma tulikuwa waonevu basi hatuna budi kuachia wote tufungue kurasa mpya...

Na si hivyo tu sheria zirudiwe na zieleweke sio tu mtu kukosea matamshi ya lugha anapewa kesi ya uhujumu uchumi na chombo kufungiwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom