NingaR
JF-Expert Member
- Apr 15, 2012
- 2,759
- 590
Nimemaliza kidato cha 6 mwaka huu nikichukua mchepuo wa pgm na kupata div iii-13 yaani physics-e, mathematics-d, geography-d na gs-s, pia o-level chemistry sikuifanyia mtihani kutokana na sababu zilizo kua nje ya uwezo wangu lakini niliisoma kama masomo mengine, sasa nataka kusomea civil engineering chuoni tatizo linakuja katika vyuo vingi hapa nchini wanataka o-level angalau niwe na c ya chemistry lakini chuo cha St. Joseph wanataka any two principals in physics, mathematics na chemistry, nimejaribu kuwatumia email kuulizia kama naweza pata admission lakini bado hawajanijibu, Siolazima kusoma St. Joseph hata vyuo vingine pia itasaidia sana. Wadau wa elimu hapa jf naombeni mnipe mwangaza kwa hili nifanyaje ili niweze kutimiza ndoto zangu za kupunguza tatizo la miundombinu hapa nchini kwetu kwani ndio sababu kubwa ya mimi kutaka kusomea civil engineering, akhsanteni na mungu awabariki na kuwaongoza