Wadau naombeni Msaada please. Nimepatwa na Janga

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,700
Reaction score
14,639
Ni week sasa nipo jiji la Mwanza kwa mapumziko ya mwisho wa Mwaka. Nina sehemu nimeweka kakibanda na ufugaji na mapumziko pia.

Leo nmeamka asubuhi mmoja ya Mbwa wangu kapoteza ghafla uwezo wa kuona. Mbwa wapo wawili.hawakugombana na huwa hawana tabia ya kugombana.

Hajaumia popote pale ila haoni kabisa ingawa macho yapo wazi. Jana usiku amefunguliwa alikuwa Ok kabisa. Leo asubuhi nmeamka nifanye mazoezi namwambia kuingia ndani anazunguka tu akijigonga. Nlishangaa.baadaye nimegundua haoni.

Hata nikipitisha mkono mbele yake haoni. Zaidi zaidi anaonekana kunusa.nimepata mawasiliano na daktari wa mifugo nimemweleza anasema hajui tatizo nini.

Nimekosa raha,sina amani nataka kumsaidia huyu Mbwa maana ni mbwa mwema kabisa.very friendly kwangu na hatari kwa maadui. Huyu kijana ambaye hukaa hapa anahusisha jambo hili na imani za kishirikina.mimi sielewi hayo mambo.

Naombeni msaada namsaidia vipi mbwa wangu. Na huku niliko Madaktari wa mifugo wachache maybe niende town. But daktari mmoja huyu ndo amenambia hajui tatizo ni nini.maana macho yanaonekana hayana ugonjwa wowote na hayadhurika.ameshindwa la kufanya.

huyu bwana mdogo anakomaa tu kuwa ni mama jirani ndo tatizo.ashawahi sema yeye hapendi mbwa. Na jana alikuja kama bundi. nami nlisikia mimi sauti ya bundi but i didnt give a damn . Sasa bwana mdogo anakazia hapo hapo. Nimeshapoteza mbwa kama wanne hapa toka nimeanza fuga.

Jirani mama huyu hapendi mbwa ingawa hawafiki kwake coz hapa kuna fance. Pia mbwa ashasaidia zaidi ya mara nne kumwonesha kijana Nyoka. So its possible ni nyoka. Ingawa kijana hakubali kabisa
 
Niliwai kusikia mbwa akiwa mkali wachawi hawasogei maana ana uwezo wa kuwaona.

kwa hiyo wakiona hivyo humuwinda kwa jinsi ya kibinadamu Mkuu ili asiwazuie...
hapo itakuwa walimlushia vitu machoni...
 
Ni week sasa nipo jiji la Mwanza kwa mapumziko ya mwisho wa Mwaka. Nina sehemu nimeweka kakibanda na ufugaji na mapumziko pia.

Leo nmeamka asubuhi mmoja ya Mbwa wangu kapoteza ghafla uwezo wa kuona. Mbwa wapo wawili.hawakugombana na huwa hawana tabia ya kugombana.

Hajaumia popote pale ila haoni kabisa ingawa macho yapo wazi. Jana usiku amefunguliwa alikuwa Ok kabisa. Leo asubuhi nmeamka nifanye mazoezi namwambia kuingia ndani anazunguka tu akijigonga. Nlishangaa.baadaye nimegundua haoni.

Hata nikipitisha mkono mbele yake haoni. Zaidi zaidi anaonekana kunusa.nimepata mawasiliano na daktari wa mifugo nimemweleza anasema hajui tatizo nini.

Nimekosa raha,sina amani nataka kumsaidia huyu Mbwa maana ni mbwa mwema kabisa.very friendly kwangu na hatari kwa maadui. Huyu kijana ambaye hukaa hapa anahusisha jambo hili na imani za kishirikina.mimi sielewi hayo mambo.

Naombeni msaada namsaidia vipi mbwa wangu. Na huku niliko Madaktari wa mifugo wachache maybe niende town. But daktari mmoja huyu ndo amenambia hajui tatizo ni nini.maana macho yanaonekana hayana ugonjwa wowote na hayadhurika.ameshindwa la kufanya.
Wanga nuksi sana
 
kuna nyoka anaitwa spitting cobra ana uwezo wa kurusha sumu umbali wa mita 6 na hakosi target yake ya machoni.husababisha temporary blind au forever blindness inategemea na idadi ya sumu imempata vipi.mapema ungemuwahi kwa maji safi umsafishe macho kisha umtie dawa za macho za antibiotic
 
Atakuwa ametemewa mate na nyoka tu .mbwa wangu aliwahi kupata shida kama hii ila baada ya siku kadhaa akapona
Macho yake yamekuwa ya Blue. Sasa hivi nikiwa mbali kidogo ananiona nikisogea hanioni.
 
kuna nyoka anaitwa spitting cobra ana uwezo wa kurusha sumu umbali wa mita 6 na hakosi target yake ya machoni.husababisha temporary blind au forever blindness inategemea na idadi ya sumu imempata vipi.mapema ungemuwahi kwa maji safi umsafishe macho kisha umtie dawa za macho za antibiotic
Ngoja nifanye hivyo nione.
 
GuDume pole sana kapten.
Hapo nyoka kamtemea mate, atakaa sawa ndani ya wiki tu.

Hii ni ishara kwamba maeneo karibu na hapo kuna nyoka au alipita na biashara zake akakumbana na mbwa akaamua kujihami.
 
Kumuosha kwa maji anaweza kuwa amechelewa ila nafikiri bora amuache tu kwa sasa. Atakaa sawa
 
Macho yake yamekuwa ya Blue. Sasa hivi nikiwa mbali kidogo ananiona nikisogea hanioni.
Soon atakuwa poa kama vipi chukua sabuni au zile dawa zao kumuosha ili bacteria wasiunge humo tatizo likawa kubwa .
 
Hapana itasaidia kama maji yatakuwa na sabuni kuuwa bacteria wanaoweza kuingia kwenye macho ,kwa sasa tongotongo najua zitakuwa kibao
Kumuosha kwa maji anaweza kuwa amechelewa ila nafikiri bora amuache tu kwa sasa. Atakaa sawa
 
GuDume pole sana kapten.
Hapo nyoka kamtemea mate, atakaa sawa ndani ya wiki tu.

Hii ni ishara kwamba maeneo karibu na hapo kuna nyoka au alipita na biashara zake akakumbana na mbwa akaamua kujihami.
But huyo nyoka ndo atakuwa amekuja kwenye anga za huyu jamaa yangu. Huyu mbwa hatoki kwenye gate isipokuwa jioni anatolewa akajisaidie na asubuhi haraka anarudi. Leo hata nje ya gate imebidi apelekwe. Sasa inabid kuanzisha MSAKO WA HAYAWANI HUYU. huyu bwana mdogo anakomaa tu kuwa ni mama jirani ndo tatizo.ashawahi sema yeye hapendi mbwa. Na jana alikuja kama bundi. Nlisikia mimi sauti ya bundi but i didnt give a damn . Sasa bwana mdogo anakazia hapo hapo aiseee...
 
Inaonekana nduguyo anapenda hizo imani sana.
 
Back
Top Bottom