Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilayani Ulanga inawashikilia watu wanne wanaodaiwa kukutwa na mamilioni ya fedha zinazoaminika kuwa zililengwa kugawiwa kwa Wajumbe Wapigakura za maoni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Ulanga.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa vijana hao ni mawakala wa kugawa fedha waliokuwa wakitumika na mmoja wa wagombea ubunge wenye nguvu kifedha katika jimbo hilo.
Watu hao walikamatwa usiku wa kuamkia tarehe 04 Agosti 2025 siku ya Uchaguzi wa Kura za Maoni katika Kata ya Mwaya tarafa ya Mwaya majira ya Saa 7 Usiku.
Watia nia katika jimbo hilo walikuwa Abdallah Kirungu, Christina Mpete na Mbunge anayetetea kiti chake, Salim Alaudin Hasham. Wengine ni Oswald Matefu, Thabiti Dokodoko na Andrew Magombana.
Hata hivyo mchuano mkali ulikuwa kati ya mfanyabiashara mkubwa wa madini ambaye ameongoza kura za maoni, Salim na Mwanadiplomasia Kirungu.
Taarifa kutoka Kidogo cha Polisi cha Mwaya, Wilayani Ulanga, waliokamatwa wametajwa kuwa ni Kenethi Msoromoko ambaye alikutwa na shilingi 1,936,000 na majina na namna za simu za wajumbe waliopaswa kutumiwa pesa hizo.
Mwingine ni James Fimbo ambaye taarifa zinaeleza alikutwa na fedha nyingi zaidi pamoja na majina na namba za simu za wapigakura za maoni.
Kabla ya kukimbizwa kituo Kidogo cha Polisi Mwaya, watuhumiwa hao walipigwa na watu wenye hasira na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao kama vibaka.
Inaelezwa kuwa, vijana wengine wanne walikamatwa baada ya Takukuru kufanya mahojiano na watuhumiwa wawili wa mwanzo ambao ni Kenethi na James.
Kamanda TAKUKURU Wilaya ya Ulanga, Joseph Kayombo alipoulizwa alisema mwenye mamlaka ya kuzungumzia matukio hayo kwenye taasisi hiyo ni Kamanda Takukuru mkoa Morogoro.
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, Pili Mwakasege alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo alisema ni mapema mno kwa taasisi yake kutoa taarifa za matukio ya rushwa mkoani Morogoro kwani nyingi bado zinafanyiwa kazi.
“Kuna matukio na taarifa nyingi za malalamiko ya rushwa, sasa kukamata au kuwahoji baadhi ya watu sio mwisho kwani zingine zina ukweli na zingine ni tuhuma tu,” alisema Kamanda huyo TAKUKURU.
Hata hivyo aliongeza kuwa baada ya kukusanya taarifa zote na kuzifanyia kazi, wanazipeleka Makao Makuu ya TAKUKURU kwa hatua zaidi hivyo aliomba muda zaidi ya kumalizia kazi hiyo.
Kule Jimbo la Kisarawe mkoani PWANI, Mbunge anaemaliza muda wake ndugu Selemani Jaffo akituhumiwa kuhonga na kutoa rushwa, watu kadhaa wamekamatwa wengine ni viongozi wa Jumuiya ya wazazi wakiwa na kura feki, na pia viongozi wa chama kunavideo zinawaonyesha wakigawa fedha.