Wadai kuchangishwa Sh 10,000 kila mtu ili wasihamishwe Hifadhi ya Ngorongoro

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Baadhi ya wananchi wanaoishi eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wamesema 'kiburi' walichonacho viongozi wa vijiji, wazee wa mila wa jamii ya wafugaji wa Kimasai na baadhi ya wanasiasa, kinatokana na kuachangisha fedha wakazi ili kwenda kuwatetea wasiondolewe hifadhini.

Wamesema viongozi hao huwachangisha wanawake Sh. 2,000 na wanaume Sh. 10,000. Madai hayo yalifichuliwa juzi na wawakilishi wa wananchi wanaotaka kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Akizungumzia michango hiyo, mwakilishi wa wananchi wa Kata ya Endulen, Foibe Lukumay alisema: "Mikutano kila siku na kuchangishwa hao hao wanachangishwa. Hata mimi nimechanga kwa sababu ni mwanakijiji.

"Kwanini nisichange kama tukiambiwa na viongozi wenzetu wa mila kwa ajili ya kwenda kutetewa. Wanawake wa Kimasai hawana nguvu na hawana haki kwa mume, kusema kwamba mimi nitaondoka wewe ubaki, haiwezekani.

Tunachangishwa ili viongozi waondoke kwenda kutusaidia, hasa Malaigwanani (wazee wa mila), kufika hata kwa mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan."

Foibe, ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Endulen alisema wanawake lazima watoe mchango huo kwa sababu wako chini ya wanaume.

Aidha, kwa sasa katika Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha, baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na masuala ya utoaji elimu ya kujitambua, kujikwamua kiuchumi na haki za jamii za kifugaji, yanatajwa kufanya kampeni za chini kwa chini kushawishi wananchi wasiondoke kwenye makazi yao wanayodai ni ya asili.

Mwanaharakati na Mkazi wa Kitongoji cha lrmuli, Kijiji cha Oloirobi, Kata ya Ngorongoro Paulo Mama sita, alisema: "Ninavyoona mimi ni kama wanafaidika kupitia mchakato huu. Ile kwenda kushawishi wao wanapata fedha kwa wafadhili, hawajui wanamuumiza yule mtu wa hali ya chini, kwa sababu yule hajasoma, hawezi kuona vitu kwa mapana zaidi yeye."

Alisema wananchi wanaotaka kuhama kwa hiari Ngorongoro, wanasumbuliwa, hivyo wanashindwa kutoa maamuzi ambayo ni sahihi.

Hivyo, aliiomba Serikali iyachunguze mashirika nayo pamoja na baadhi ya watu binafsi wanaotumia ushawishi wao kuvuruga zoezi hilo.

Kiongozi wa Mila wa Jamii ya Kifugaji ya Kimasai (Laigwanani), Matengwai Ole Tauwo, Mkazi wa Kijiji na Kata ya Aleilai alisema:

"Nimeona Ngorongoro hakuna kitu cha kutawala, hakuna miliki ya ardhi, hakuna ruhusa ya kuvuna miti au kufanya maende leo yoyote ya kiuchumi. Ukitaka kwenda kwenye maeneo yenye maji ya kunywesha ng'ombe au mbuzi lazima utoe taarifa na ukitaka kupitisha pikipiki hairuhusiwi. Sasa kwa nini nikae Ngorongoro."

Mkazi wa Ngereiyani, Kijiji cha Osinoni, Kata ya Kakesio, alisikitishwa na kauli za Lukas Tiamasi, baadhi ya wanaharakati wanaotoa elimu ya ushawishi kwa wananchi ili wasihame.


Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom