KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,153
- Thread starter
- #21
Last edited by a moderator:
Meje na cindy wanamchuano mkali ambao umezaa biff kwa sasa kati yao,lakini hilo biff linakuzwa na koffi olomide:koffi anamchukia sana meje 30 kwa kuwa meje aliwahi kuwa kwenye moja ya bendi ya koffi kama underground pale,sasa koffi kama kawaida yake akawa anataka kumtumia au inawezekana alimtumia lakini meje baadae inaonekana hakukubali kutumiwa na koffi hali iliyopelekea aachane na koffi,kitu kinachoelezwa kumchukiza koffi ambae kwa hasira ndio akaamua kumtoa cindy ambae walikua pamoja kwenye bendi ya koffi kama ma underground,meje ndio akaamua kujiunga na tshala muana.Lakini inaonekana bado hajakubali na inasemekana amekua akihangaika kumtafutia meje kashfa mbalimbali kwa kutumia waandishi wa habari na wapiga picha ili wachafue meje 30 na cindy azidi kupanda chati kwa kuwa anajua meje ana kipaji zaidi ya cindy,kwa wafuatiliaji wa haya mambo watakumbuka kuna picha za utupu za meje akiwa stejini huko uganda ambapo ukisearch kwenye google kwa kutumia jina la mege 30 utaziona,inasemekana hizo picha ni kazi ya watu waliolipwa na koffi kuzichakachua kwa kutumia photo shop ili kumdhalilisha meje,na kwa kweli sio picha nzuri kabisa kuzitizama,zinatia aibu kwa mwanamke.
nimekuwa mshabiki mkubwa wa Cindy lakini thread hii imenifanya nifunguke juu ya binti Meje 30...............Sema hili la koffi kumkwarua natia shaka kidogo.
meje trante ana full packagez kwangu kuanzia uzuri, style ya nywele na sauti. Napenda sana anavyofit anapoimba na Tshela Mwana haswa ktk kibao cha grand petre mere huwa nasuuzika sana. Cindy Sio Nzuri Kwa sauti ila Koffi huwa anampandisha anapolalamika nyuma ya sauti ya Cindy na wimbo ulionikuna ni ule wa L'amour n'existe Pas
Wakuu Kizimkazimkuu,The Romantic na Hadj Drogba nafurahi kusoma comment zenu jinsi mnavyowachambua mabinti hawa......... hebu tuangalie upande wa pili tena wa Muziki huu kwa kizazi kipya wa Kongo kwa upande wa wanaume tuwajadili wakina Fally,Ferre Golla na wengineo ambao wametoka kwenye Band za wakongwe................Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa huu Muziki hasa rhumba na kwa kweli napenda sana muziki wa Ferre Golla na ningependa kuona mkimchambua kama mlivyofanya kwa Cindy na Meje 30........Kuanzia alipokuwa Wenge Musica
Kiufupia ferre alijiunga na wenge original mwishoni kwa kuletwa na werrason,ndio maana utaona hata jb mpiana na wenzake walipoamua kujiondoa wenge musica 4x4 tout terrain kwenda kuasisi wenge musica bcbg miongoni mwa wanamuziki wachace waliobaki na kina werra mmojawapo alikua ni ferre,yeye alikua ni kijana mtiifu kwa werrason japo baadae sana walikuja kutofautiana na ferre kuanzisha bendi yake ambapo kabla ya kuanzisha bendi yake alikimbilia paris ambapo mkewe anaishi huko ni raia,ferre pia kwa sasa anayo "makaratasi" ya kuishi ulaya(france)ambayo aliyapata through huyo mwanadada.Baada ya kuwa huko ferre alifuatwa na wanamuziki wenzake kina Bill clinton waliojitoa wenge musica maison mere ya werrason ambae wakati huu bendi alibaki nayo peke yake ikawa yake baada ya kufanya fitna zilizowaondoa waanzilishi wenzie ADOLPHE DOMINGUEZ na le foundee DIDIER MASELA.FERRE GOLA alipofuatwa na kina BILL CLINTON hakusita kujiunga nao kuanzisha bendi chini ya meneja SIMON SIPE(Jamaa hatari sana huyu kwa kuua bendi,ipo story yake) na baada ya ferre kukubaliana nao wakasaini contract ya miaka kuni na SIPE ambapo SIPE akapendekeza bendi iitwe LE MAQUIS DE MAISON MERRE ili kuwachanganya mashabiki wajue kabisa hawa vijana wametoka wenge maison merre ya werra!
Story ndefu nimejaribu kuifupisha angalau upate picha kwanza...hapa chini kuna video ya ferre akiwa na WENGE ORIGINAL kabla kina mpiana hawajaondoka lakini ndio wakiwa mbioni kuondoka maana hata ukitizama utaona katika show hii ya mwisho mwisho ya wenge original wakiwa pamoja hapo Abidjan walipiga mara mbili,ya kwanza walipanda wote waliokuja kuwa wenge maison halafu iko nyingine siku hiyo hiyo walipanda wote waliokuja kuwa bcbg hapa namaanisha jb,blaize bula etc,kasoro tutu caludji(repa)yeye alipiga kazi na wote siku hiyo japo baadae walipogawanyika aliondoka na jb mpiana kuunda bcbg.Pia Alain mpela na Aimeli Lyase Demingongo nao walishiriki hapo japo baadae waliondoka na jb mpiana.
ferre wa pili kulia baada ya Adolphe Dominguez mwenye kanzu na pama..