wadada wa kizazi kipya DRC nani zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wadada wa kizazi kipya DRC nani zaidi?

Discussion in 'Entertainment' started by KIM KARDASH, Feb 3, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kuna watoto wawili ambao wamekua pamoja na kujifunza muziki pamoja na wametoka pamoja huko DRC,mmoja yuko chini Koffi Olomide ambae kwa sasa ni kama mke wake akiitwa Cindy Le Coeur na mwingine yuko chini ya mamaa mokonzi Tshala Muana akiitwa Meje 30,ambae mama Tshala anamuandaa kuwa mrithi wake,hapa kuna video zao ambapo wamejitahidi kunata na biti,je nani katisha?

  CINDY CHANTE KOFFI TITRE L'eau L'eau L'eau / DJOMEGABP  MEJE 30 CHANTE ABETI MASIKINI Titre Bade Dans face B / DJOMEGABP
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  huyo mke wa koffi anapiga makelele mwenzake anaimba!
   
 3. K

  KIFILI Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lol!sauti nyororo viuno nyoronyoro hayo ndio mambo yangu nikiwa napata moja baridi na shemeji yenu huku nasikiliza muziki wataratibu na sauti nyororo kama hizi,asante sana.
   
 4. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  ..Thank you for this post; hawa mabinti kwa sasa ndio kizazi kipya cha wanamuziki wa kike wa congo. binafsi nawakubali wote, meje 30 ana sauti nzuti na anafuata nyayo za Tshala Muana vizuri tu, na Cindy nae anatisha.....ingia google andika Cindy chante Koffi Zenith utaona show aliyofanya na Koffi Zenith, France was awesome! Tatizo critics wanasema Cindy anaimba nyimbo za Koffi ndio zinambeba wanampa changamoto atunge au aimbe nyimbo zake watu waone ubora wake
  na upload video zao wote wawili soon
   
 5. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  ...Hebu angalia hapa; unaweza kurudi hapa na kubadili kauli yako

  KOFFI OLOMIDE / CINDY proclamée meilleure chanteuse 2009 ZENITH ASPIRINE / Dj omegabp
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Hapa muangalie Meje 30 akiimba
  [Congo] Tshala Muana et MeJe 30 -- Doukou doukou


  halafu hapa muangalie Cindy Le Coeur akiimba Elixir..
  KOFFI OLOMIDE / CINDY 2009 ZENITH ELIXIR / DJ OMEGA BP
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini nyie mnabisha je mnajua walitokea wapi hawa watoto?hebu angalieni hii video kwa makini kama hamkulia na koffi kukabaka haka ka cindy,kwenye hii video mtawaona wote wawili wakiwa wadogo,cindy kulia kabisa na gauni ya rangi ya maziwa flani hivi,meje kushoto na blauzi nyeusi juu chini suruali white,katikati yao wenzao wengine wawili.Hapa walikua wanaimba kuhusu ukimwi na groupe yao ya mtaani enzi wakiwa makinda.kweli watu wanabadilikaga jamani lol,sasa hivi "walivyooga" huwezi amini kama ni wao!

  Cindy Le Coeur et Meje30 chantent Sida avec leur groupe Wassa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. T

  THE WHITE ELEPHANT Member

  #9
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa vipi wadau?

  Meje 30 Feat Fally Ipupa TSHOBO
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  sikilizeni hii fimbo ya Bakandja toka kwa Meje 30!naona hii inaweza kuwa ni fimbo ya ushindi kwa wapenzi wa meje au vipi?


  Mege 30 - Fimbo ya Bakandja
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. K

  KIFILI Member

  #11
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Najuta kutoifungua mapema hii thread leo,lol!cindy kwenye video ya kwanza nimeisikiliza vizuri sana kuna maneno anayasema kuhusu yeye na mumewe koffi ameyachomekea vizuri sana nimeyapenda naona mpaka washabiki wakaomba arudie,pale anapoimba hivi:

  "nzoto na ngai le coeur elengi na nga mopao,nzoto na ngai le coeur elengi na nga mokonzi,nzoto na ngai le coeur elengi na nga quadra kora man"
   
 12. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  ...Kim Kardash naona wewe namba moja yako ni Meje30; binafsi namkubali zaidi (lakini pengine niko biased kwa sababu naturaly nazimia wanawake wenye extra flesh).....
   
 13. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45

  ..kama ukisikiliza huu wimbo halafu ukasikiliza FM Academia wimbo wa Utamu wa vanilla utagundua Nyoshi na jamaa zake wanatuibia; Huu wimbo wa L'eau L'eau L'eau ni wa Koffi hapa Cindy kaurudia tu, kwa tafsiri ya moja kwa moja L'eau (kifaransa) ni maji lakini for sure Koffi hazungumzii maji ya bomba hasa kwa kuwa pia anataja utamu/raha (elengi)sasa jamaa wa FM Academia nao wanaimba utamu wa hivi hivi lakini kwa kiswahili na kuchomeka maneno yao machache.
   
 14. K

  KIFILI Member

  #14
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yap ni kweli cindy kaurudia,fm academia mbona wanatuibia mara nyingi mzee,wote tu hawa wa congo wa dar,wanachofanya ni kuzitafuta mapema cd za live concerts za hawa jamaa then wao fm na wengine wanazifanyia mazoezi na kurekodi fasta kabla hata wenyewe hawajaingia studio wakiwa bado wanazicheza tu live kwenye steji,ndio maana wasiofuatilia na kuujua muziki wa congo sawasawa sometimes wanakwambia eti wacongo ndio wanawaiga fm na wazaire wengini wa bongo!wizi mtupu.Mfano mzuri ni ule mtindo wa samaki ana vipande vingapi ambao kina nyoshi walikopi kutoka kwa jb mpiana na mtindo wake wa "LOPELEE" (mkia wa samaki),wao walichofanya ni kuingia studio na kurekodi haraka wakati jb bado anaupiga kwenye masteji,baadae alipokuja jb kuurekodi wasiojua wakadahni eti jb kawaiga jamaa na kuna watu mpaka leo huwabadilishi katika hilo,anayway ni kutokujua tu,hata sasa huu mtindo wa jb mpiana "mpunda" kuna bendi hapa bongo zimeshaanza kuufanyia mazoezi ili zirekodi,na mingine kama liboko,rotarota,biloko n.k.tunachezeshwa sana na kina nyoshi na kuamini ni yao kumbe wanaiga tu jb ndio yake na ataierekodi mwisho wa mwaka huu itakuwemo kwenye album ijayo baada ya hii ya sayons serieux iliyoko sokoni yenye mtindo wa "amataka na mpunda"

  ANGALIENI STYLE WANAZOCHEZA WENGE BCBG YA JB MPIANA HAPA HALAFU MNAOENDA FM ACADEMIA MNIAMBIE KAMA HAMJAONA KINACHOFANANA NA KINACHOONEKANA HAPA KWA JB MPIANA.

  http://www.youtube.com/watch?v=OSMDDOOFoNQ&feature=related
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa kaka namkubali sana Meje kuliko cindy.

  Kwa wale wapenzi wa viuno vya mutuashi kama mimi mnakikumbuka kiuno bora barani afrika enzi hizo toka kwa MAMAA MOKONZI TSHALA MUANA?Hiki hapa leo kinaletwa kwenu na Meje 30,usibabaishwe na mwili mkubwa subiri mambo,maana kuna pahali viatu vitawekwa pembeni....na kuacha kiuno kifanye kazi yake

  MEJE 30 & TSHALA MUANA 6 EN HD LIVE A PARIS / DJOMEGABP - YouTube
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Pia ni kweli kabisa Cindy anabebwa na nyimbo za koffi zaidi,angalau meje ameweza kuimba nyimbo zake mwenyewe na pia kushirikiana na watu kama Fally na akafanya uzuri tu pia hiyo fimbo ya bakandjaa nilikua sijaisikia lakini utaona ni wimbo mzuri sana ambapo ameshirikiana vizuri na mwalimu wake mamaa tshala muana.Pia kuna wimbo huu wa kampeni alimtungia rais kabila kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa congo.
  Meje30 CHANTE PRESIDENT JOSEPH KABANGE KABILA (clip exclusivite) - YouTube
   
 17. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45

  ..Nakusoma mkuu; seen this clip it is hot!
   
 18. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  ...Mkuu naona uko deep; kwa sasa ngoma ya kicongo nayoizimia ni Mpunda; JB ni bonge la entertainer!
   
 19. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kweli hii fimbo kaka,dada ana sauti nzuri sana sikumfahamu kabla thanx for this video,huyu dada viatu vya tshala muana vitamtosha tu hakuna shaka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu hakuna ngoma inayoitwa mpunda bali mpunda(farasi)ni style iliyoanzishwa na kutumiwa na jb mpiana na wenge bcbg yake katika albu ya mwisho iliyotoka mwaka jana katikati iitwayo sayon serieux kama alivyobainisha mdau hapo juu.Kiukweli hiyo style imewashika sana wacongo man,habari nzuri kwa wabongo hasa wale ma bcbgque(wapenzi wa bcbg)kuna taarifa za ujio wa jb mpiana tanzania muda si mrefu kutoka sasa kama mambo yataenda sawa.

  Hii hapa ni video ya jb mpiana na bendi yake huko Paris alipokwenda kuitambalisha mpunda kwa bana poto(watoto wa ulaya)

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...