YALIYOJIRI SHEREHE YA MIAKA 32 YA QUARTIER LATIN INTERNATIONAL YA KOFFI OLOMIDE

The August

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
1,080
2,024
KOFFI OLOMIDE": Kabla hata Group "QUARTIER LATIN" halijaanzishwa rasmi, nilikua nikifahamika Inchini kote kama "L'ETUDIANT LE PLUS CELEBRE DU ZAIRE" / MWANAFUNZI ALIE MAARUFU SANA INCHINI ZAIRE, hilo hutokana na kipaji changu cha utunzi wa nyimbo.

Kipindi kile nilikua nikipokea mialiko mbalimbali ilinapate kuwaburudisha Watu kwenye sherehe zao "harusi,B'Day,msibani... Walikua wakizipenda sana Nyimbo zangu.

Endapo napata mualiko, nilikua nikiomba msaada kwa baadhi ya Wanamuziki ambao tayar ni ma Stars ili waje kunisaidia kuimba kwenye Shughuli yangu.

Kuna kipindi fulani nilipata mualiko wa kwenda Congo Brazzaville, sahari hiyo,niliwashirikisha Wanamuziki akina "DJUNA DJANANA","DINDO YOGO","ROXY TSHIMPAKA", tukaongozana nao kufanya SHOO, Watu walijazana hadi ukuta wa ukumbi ukavunjika.

Haikua jambo rahisi kuwapata Wanamuziki na kuwashawishi wakusaidie kuimba, wakati mwengine imetokea wanazo shughui zao,hawawezi kuziacha kwa ajili yako.

Mda ulifikia nirudi Chuo,nililazimika kuondoka Jijini "KINSHASA" kwenda Ulaya "PARIS". Wakati walikizo ndo nikarudi tena kama kawaida "KINSHASA".

Nikiwa "KINSHASA" nikafaanikiwa kupata tenda yakudumbwiza kwenye Ukumbi wa bar moja ilioka KIMPWANZA. kama kawaida nilihitaji msaada wa Wanamuziki ili tushirikiane kwa pamoja.

Safari hii nikamwendea Ndugu yangu "BEN NYAMABO", ndie aliekua Kiongozi na Mmiliki wa Group "CHOC STARS" Group lililo bobea Magwiji wa Muziki, hapa ntawataja :"DEBABA","GENERAL DEFAO","CARLYTO"...
Bila kusita akanikubalia, siku ya Shoo akaja na Group nzima vikiwemo vyombo, vifaa vyao,walinzi, pia na wauza Ticket. yaai Mimi nimekuja na Nyimbo zangu pekee.

Kwakweli Watu walikua wengi sana,na SHOO ilikua nzuri, baada ya SHOO kumalizika, nikaona "BEN NYAMABO" kanijia sehemu nilipokua nikisimama, na kanigea bahasha iliokuwepo na hela, nikazihesabu, wala sijaridhika na kiasi nilichopewa.

Nikamuuliza mbona pesa zaonekana kama ndogo kuliko nilivyo tarajia wakati Watu walijitokeza kwa wingi?, kajitetea kwakusema kwamba, ukiondoa malipo ya Wanamuziki wa Group,kulikuwepo pia gharama za Walinzi,pesa za kukodisha ukumbi, na mlolongo wa mambo mengine yaliyo takiwa kutekelezwa.

Kwakua kipindi kile nilikua sitegemei sana pesa za Muziki,sijapendelea kuendelea na maongezi hayo, tukaagana nikaingia zangu ndani ya gari na kuondoka.

Nikiwa njiani wakati narudi nyumbani, mawazo mengi yakawa yananikuna kichwa, huku nikifikiria laiti ningekua na Group langu binafsi, kwa siku ya leo hii, ningekua na mahesabu mengine.

Nikageuza gari nakwenda moja kwa moja kumuona Mzee wangu "VERON" ndie kwanza Mtu ambae kanifunza kusakata Gita. tukajaribu kujadiliana kuhusu wazo la kuanzisha group, kanipa muelekeo wake, kwakweli Mzee VERON kawa nguzo kubwa kwangu.

Tarehe 26-11-1986, Group "QUARTIER LATIN" liliibuka rasmi, uzinduzi ulikua kwenye maeneo ya PHENIX HOTEL. na tokea tarehe hiyo hadi leo hii Group bado lipo juu sana.

Yapo mabaya na mazuri yaliyo jitokeza kwenye Group, ntaanza na mabaya, hakuna kilicho nisikitisha saana kama kitendo walicho nifanyia Vijana wangu wakati wame jiondoa na kwenda kuunda Group "QUARTIER LATIN ACADEMIA".

Yaani tulikuwa dhiarani Jijini Dar-Es-Salaam kwa ajili ya SHOO, siku ya SHOO, nafika uwanjani, nawakuta Ma dancers pekee wakiwa Stejini, nikauliza Vijana wengine wako wapi? jibu nikwamba bado hawajafika, nikasema sio kawaida nipande jukwaani na hawa Vijana hawapo.wenda kunatatizo limetoea.

Tukaongozana na "CHEZ NTEMBA" ndie aliekua Producer kipindi kile, hadi hotelini walipofikia Vijana.
Hotelini hapo tukaambiwa tayar wamesha ondoka na kuelekea Airport kwa safari ya kurudi Paris.

Nikapigwa na mshangao, kwanini wanatenda jambo kama hilo?
Nikwa mara ya kwanza katika historia ya Muziki wa Congo,Wanamuziki wanakimbia wakiwa AFRICA. kwakawaida wengi hukimbilia wakati wapo Ulaya.

Basi nikalazimika kufanya Shoo hiyo ili kuheshimu mkataba, kwa bahati nzuri,Jijini Dar-Es-Salaam palikuwepo na Vijana wa KiCongo ambao walikua wanazijua vizuri Nyimbo zangu wakasaidia kuziba pengu.

Jambo njema, ntasema ujio wa "FALLY IPUPA", kwakweli linapokujia jambo baya, basi wewe watakiwa shukuru tuu, jua njema laja. kwa leo hii "FALLY" kaliletea sifa na fahari sio tuu Inchi ya Congo bali bara nzima la Africa.

SHOO SIKU YA SHEREHE ILIKUAJE ?

SHOO ntasema imeanza rasmi pale tuu "CINDY LE COEUR" kapanda stejini !

"CINDY" kapendeza sana,kanenepa kidogo, kavalia nguo za rangi ya "Black and white" ilio mkaa vizuri, huku akibadirisha kabisa mtindo wa nywele, yeye ambae kazoeleka kua kichwa upara au mwenye nywele fupi, kaweka Wig na katokeleza vizuri.

"CINDY" kasakata dansi ile mbaya kwa mshangao wa wengi, yeye ambae zoezi la usakataji rumba huaga ngumu kwake, kweli kila kitu mazoezi, siku hiyo kajitahidi sana.

Baada ya dansi,"CINDY" kachukua Mic, nakutoa salaam kwa Umati wa Watu ulio jitokeza nakujazana kwa wingi kuhudhuria sherehe hiyo kwenye viwanja vya FIKIN.

Kama ilivyo kawaida yake, "CINDY" kaimba kwa umaridadi Nyimbo tatu. kaanza na Wimbo "IKEA" uliopo kwenye Album "BORO EZANGA KOMBO" ya Mwaka 2008. kaunganisha na Wimbo "RAVISSE" Album "EFFRAKATA" Mwaka 2002, kaja kumalizia na Wimbo "MOLOUNGE" Album "MOLOUNGE" Mwaka 2013.

Pindi tuu kamaliza "CINDY" kashangiliwa kwa nguvu huku mashabiki wakiomba arudilie tena kuimba.

Mzee mzima "KOFFI OLOMIDE" kapanda jukwaani na miondoko ya "ELENGI MOKO MOPAO MOKONZI". Dahh Umati ukishangilia kwa furaha !!!

Mzee "AGBADA QUADRA KORA" kawaambia Watu walio jitokeza kwa wingi maneno haya :"NAZALAKA MPO BINO BOZALI" / UWEPO WANGU NIKWAKUA NYINYI MPO, BILA NYINYI MIMI SICHOCHOTE.

Bila kuchelewa ikapigwa "SEBENE" Tata mobimba, "MOPAO MOKONZI" kajiweka katikati ya Vijana wake huku akiongozana nao kusakata dansi sambamba nao.

punde kidogo ma dancers nao wakaingia, wakiongozwa na MAMY INTAZOMA wakifanya yao burudani saafi kabisa !!!

Kwenye Dakika ya 42 hivi, Muziki ulisimamihwa ili zoezi lakuwagea Wanamuziki zawadi ya Gari lianze, wakwanza kapewa funguo ya Gari ni Mpiga Solo Gita mahiri "VOLCAN" kwakufurahia zawadi yake, "VOLCAN" kacharaza "SEBENE" ya Wimbo "SELFIE" na baadae "KOFFI OLOMIDE" kamtangaza rasmi kama ndie "CHEF D'ORCHESTRE" / kiongozi wa Wanamuziki.

Wapili kupewa zawadi ya Gari ni Kijana mwimbaji machachari "OMBA LIPASA" kapewa Mic kwa shukran kaimba wimbo "PHARMACIEN" utunzi wa "FALLY IPUPA".

Watatu kapewa zawadi ya Gari ni "BOUMPA MYSTIC" Mpiga Rhythmic Gita wa siku nyingi tokea Mwaka 2002 yuko ndani ya Group.

Wainne Kapewa zawadi mpiga Ngoma "SUIRA MUNDELU"

Gari la Tano kapewa "LINDALALA Sprada" yeye ni Mwimbaji.

Gari la sita kapewa "ERIC TUTSI" Mwimbaji tokea Mwaka 1994.
Gari la Saba kapewa "BB JTROIS" Mwimbaji tokea Mwaka 2016.
Wengine walio pokea zawadi ya Gari ni : ROCKY BLANCHARD, FABRIZO,MUKUSA MBWA...

kwajumla Watu 17 walipokea zawadi ya Gari."WENGINE WALIPEWA ZAWADI YAO BAADA YA SHOO"

Baada ya zoezi la zawadi, Mzee "KOFFI OLOMIE" kawatambulisha Wanenguaji wapya 14 :

01. JENNIFER
02. LIPAMOTO
03. FANTOME
04. SARAH NOIRE
05. RACHEL MBUY
06. LINETTE BOFANGA
07. IDA MBOTO BAFANTA
08. JULIE IPUPA
09. LAMIGNONE MWANA
10. CARMENE NGALULA
11. MALANGINE
12. BENEDICT LOTALA
13. FRANCAISE MBUMBU
14. MYRADOR

SHOO imeendelea, "CINDY" na Ma Dancers wakicheza "Kalembelembe". walivyo maliza akapanda Stejini "GIBSON BUTUKONDOLO" Mwanamuziki wa zamani wa Group, yeye kajiunga na Group Quartier Latin tokea Mwaka 1999,nakajiondoa Mwaka 2008. kaimba wimbo wake "BA LOBIENS"Album"DANGER DE MORT".

Baada ya Saa nzima na dakika 11, "FALLY IPUPA" kapanda Stejini, Umati wa Watu ukashangilia, "KOFFI OLOMIDE" wakati kamkaribisha Jukwaani kawataka Watu wampokee kwa shangwe "MWANA NANGAI YA LIBOSO" / MWANAGU WA KWANZA. tamko hilo halijawafurahisha wengi, iweje "FALLY IPUPA" awe Mtoto wa kwanza wa Group wakati kalikuta tayar Group limeshasimama tena sana! au kwakua ndie alie na mafaanikio dhahiri?

"FALLY IPUPA" kaliwasha jukwaa, pindi tuu kapewa MIC, kaimba wimbo wake "PHARMACIEN". Sebene lilipigwa zikikumbushiwa zilizo pendwa, huku Rapa "APOCALYPSE" akionyesha cheche zake kama zamani.

Muziki ulisitishwa tena, "KOFFI OLOMIDE" akawaita Wanamuziki wote wazamani wapande Stejini.
Walikuwepo :
APOCALYPSE "RAPA"
CNN ALIGATOR "RAPA",
CHAMPION NDJIKAPELA "DRUM"
PASE KOSE "NGOMA"
BINDA BASS "BASS GITA"
FELLY TYSON "SOLO GITA"
GABBANA "MWIMBAJI"
SUZUKI LUSUBU "MWIMBAJI"
GIBSON BUTUKONDOLO "MWIMBAJI"
WILLY BULA "MWIMBAJI"

Wakiwa wote Stejini ikapigwa "NDOMBOLO YA SOLO", "GIBSON BUTUKONDOLO" ndie kaonekana mwenye kuchangamka kuwazidi wote.

"WILLY BULA" yeye ni mdogo yake "BLAISE BULA", kajiunga "QUARTIER LATIN" tokea Mwaka 1988, na kajiondoa Mwaka 1997, kapewa Mic na "FALLY" ulipoimbwa Wimbo "PETIT NA LODON" Album "MAGIE" Mwaka 1994. ambao ndie kawa Mwimbaji kinara kwenye Wimbo huo.

"SUZUKI LUZUBU 4x4" : Mwimbaji asietambulishwa, mmoja kati ya Vijana walio acha alama kwenye Group, alipochukua Mic kakumbushia wimbo "NOBLESSE OBLIGE" Album "NOBLESSE OBLIGE" Mwaka 1993. "A muvila muyaya eeh eeh a muvila muyaya maweni eee Koffi Olomide"

Wimbo huu ukaunganishwa bila kuchelewa na Sebene ya Single "SKOL LONGITIMA".Watu wakaselebuka na Dansi "KISANOLA","BA MAMAN PESA SIMA PAPA BETA TONGA".
Mgeni rasmi wa Sherehe hiyo ni Msanii Mkogwe "JEAN GOUBAL" yeye ambae anao urafiki wa karibu sana na "KOFFFI OLOMIDE", kwa ukumbusho, ndie kafanikisha Kijana "OMBA LIPASA" apate kujiunga na Group "QUARTIER LATIN".

SHOO ya Sherehe imekamilika wakati wa kutangaza kura ya maoni iliowekwa mtandaoni Watu walitakiwa kuwachagua :

01. MWANAMUZIKI BORA WA GROUP QUARTIER LATIN TOKEA LIANZISHWE

02. MWIMBAJI BORA WAKIKE

03. MWIMBAJI BORA WAKIUME

04. DANSA BORA WAKIKE

KACHAGULIWA MWANAMUZIKI BORA : "FALLY IPUPA"

MWIMBAJI BORA WAKIKE : "CINDY LE COEUR"

MWIMBAJI BORA WA KIUME : "SIZUKI LUZUBU 4x4

DANSA BORA WAKIKE : "BIBICIA AUTOMATIQUE"

Baada ya kura "FALLY IPUPA" kayanena haya :
"NATOA SHUKRANI ZANGU KUONA MMENICHAGUA MIMI KAMA MWANAMUZIKI BORA WA GROUP "QUARTIER LATIN", BINAFSI NTASEMA WALA MIMI SIO MWANAMUZIKI BORA KUWAZIDI WOTE, GROUP QUARTIER LATIN NI FAMILIA KUBWA, MTU WAKWANZA ANAE STAHIKI KUPEWA SIFA SIMWENGINE BALI NI MWALIMU KIONGOZI WETU "KOFFI OLOMIDE MOPAO MOKONZI".

NATOA PIA HESHIMA YANGU KWA WALE WOTE WALIE NITANGULIA KWENYE GROUP LETU HILI PENDWA, HASA NAMSHUKURU KAKA YANGU "WILLY BULA", NAOMBA MPIGIENI MAKOFI KWA NGUVU.MSHANGILIENI PIA KAKA YANGU "SUZUKI 4x4",MPIGIENI PIA MAKOFI MPIGA GITA "FELLY TYSON"... HAWA NIKATI YA WATU WALIWEKA HISTORIA KWENYE GROUP.

Wimbo "ALIDOR" ndo ukafunga Sherehe Watu wote jukwaani.

Credit: LUBONJI WA LUBONJI
 
sioni kama ni shida... la muhimu ni content aliyomo ndani ya thread yake.
Hata sioni kama ni shida na sijasema kama ni shida.Kuwa mkongoman sio shida hata kidogo.Ukichukulia alichokiandika kinawahusu wakongoman!
 
Back
Top Bottom