Wadada njooni niwape mpya, wakaka msahihishe panapohitaji usahihi

Cryspina

JF-Expert Member
May 1, 2020
298
392
Habari ya jumapili.

Jana tukiwa dinner na gurls, pamoja na rafiki wengine wa kiume,tulijikuta tumeingia katika mjadala juu ya maswala ya wanawake kuomba pesa wanaume na wanaume kutokupenda kuombwa hela, pamoja na swala zima la kujitambua kifikra, finance, kutafuta mali, kujenga Wealth, na kuwa set of plans and goals.

Ulikuwa ni mjadala very open and nashukuru hawa rafiki zetu wa kiume ambao wote wanafamilia na wameoa wana mafanikio na ndoa zao walikuwa wawazi sana katika kujadili na ikasaidia kupata kitu kipya. Zifuatazo ni baadhi ya hoja ambazo walizitoa wanaume hawa, na walisema yafuatayo:

1. Wanaume huwa hawaoni haja au ulazima wa kuta pesa kwa mwanamke ambaye hajawa rasmi kwao yaani ambaye sie mke wake na mama wa watoto wake. Wanasema mwanaume husikia wepesi kutoa pesa yake akijua inakwenda kwa mwanamke anaemlelea watoto wake ambayo ni damu yake. Hapo atajitoa bila shida labda awe hana na mambo ni magumu kiuchumi.

2. Wanawake huwa tukiulizwa katika mahusiano kabla ya ndoa, ukitoa sex, ni kitu gani ambacho tunaoffer kwenye mahusiano kama mchango wetu kama wanawake huwa tunakosa majibu sababu ya uelewa mdogo wa majukumu yetu.

3. Mabinti wengi wanaoingia katika mahusiano huwa wanakwenda na mtazamo ule ule kama wa viongozi wa inchi za Africa wakienda ulaya.

Kuomba misaada na kujiweka rehani ili kutumika kwa malengo ya kufadhiliwa baadae kama mtu dhaifu badala ya kuingia kama kiumbe active anaye tafuta mwenza wa kumpa sapoti ya kujenga maisha yao wawili.

Ndio maana wanawake wengi baada ya muda kidogo wa ndoa mawazo huwazia mume afe sisi tubakie na mali na uhuru wa kutumia kama zetu pekee yetu. Ni wanaume wachache sana huwaza mke afe waishi huru na mali. Wanaume wengi huhitaji wake zao maisha yao yote. (ladies someni mara mbili hii hoja).

4. Wanaume wamepunguza kujitoa kwa wanawake sababu ya hofu ya kuonekana wajinga kugawa pesa waliyopata kwa shida kirahisi kwa mwanamke anayemlaghai kujipatia pesa.

Wazia mdada anampigia mwanaume na kuongea nae kumuomba pesa akimlilia shida as if yeye ndie kimbilio la mwisho na hakuna msaada mwingine ile hali akitoka kwa mkaka huyu ananyanyua simu anapigia wakaka wengine watano kuomba kiasi kile kile.

5. Pesa imekuwa ngumu sana miaka hii na mojawapo ya kisababishi ni kushuka kwa nguvu ya manunuzi kutokana na kushuka kwa kipato. Nimeambiwa kushuka kwa kipato kuna changiwa sana na matumizi holela ya pesa kwa vitu ambavyo havina longterm impact. Naambiwa wadada bajeti zetu ni 80% liabilities katika uchumi wa couple au ndoa changa. (ntaomba michango sana kwenye hii hoja). Hii inawafanya wanaume kuanza kuwa wazito kushare kipato chao na wanawake sababu pesa huenda kusipojulikana.

6. Wanawake wengi hatuna family financial capacity ya kujua efforts zetu zinahitajika wapi na kwa wakati gani.

Na ndio maana si ajabu sana kukuta couple ambayo mwanaume ana mshahara wa laki 6, 7,8,9, 1 milioni na zaidi, pia mke ana kazi yenye mshahara wa level hizo hizo ila wanashindwa kufanya maendeleo na kuishia kulipa kodi, kusomesha watoto na kusaidia ndugu na jamaa huku humo ndani ugomvi mara kwa mara.

Ukifuatilia unakuta mojawapo ya chanzo ni hofu kwa mwanamke kuwa hataki kuweka pesa zake rehani sababu zinamuuma ila anataka za mumewe ziwe rehani.

7. Accountability kwetu kama wanawake ni jambo zito tunaogopa sana kuwajibika kwa mapungufu yetu na tunapenda kupata sababu ya kulaumu mtu, au watu wengine ili kupata utulivu wa hisia ila tunajua na sisi ni sehemu ya tatizo na hatupo tayari kujadili hilo.

Hii huanza katika mahusiano ya awali (boyfriend na girlfriend),ambapo binti kunapotokea tension ya uhusiano anakuwa mwepesi kukaa kimya na kuvunja mahusiano ili kupata nafasi ya kuanzisha mwingine.

Hii inatushape kuamini kuwa wanawake hatukose ila wanaume. Tunakua na hii tabia hadi umri wa ndoa na hapo ndipo tunachemka kuadjust tabia zetu, na tabia ikishakomaa kuiacha inataka ujasiri na kujishusha sana.

8. Wanawake wengi hatupendi kujua mipango ya mwanaume ikiwa hatua za awali na haijazaa matunda ila tunaka kuwa sehemu ya warithi wa matunda ya mipango hii ambayo mwanzo tuliona ni useless. Hii inawa discourage sana wanaume kuwa na ndoto kubwa na kuzisimamia zije kuwa kweli. Mama zao huwa nyuma kwa moyo wote ila sisi wanawake na matakwa yetu tumekuwa mstari wa mbele sana kuwa discourage tukiamini wanapoteza muda au hawajui walifanyalo.

9. Thamani ya mwanamke kwa mwanaume ni efforts zake na akili na focus anayompa kipindi cha utafutaji, thamani ya mwanaume kwa mwanamke ni uwezo wa kumhudumia na kumtunza. Nyakati hizi za kisasa zimekuja na vitu vipya vingi sana vya kututoa watoto wa kike katika hili eneo (kazi ya kuzimu). Leo mwanamke ataweka mwili wake, akili yake, mawazo yake rehani kwa yoyote atakae mpatia anachotaka.

Kwa hili tunawaumiza sana wanaume na wanashindwa wapi ni pa kushika ndio maana wengi wao akili zinakuja kutulia na kuwaza maisha wanapofikia miaka 38 huko kuendelea. Hii inachelewesha sana maendeleo ya kijamii na familia.

Kwa hili wadada hatuhitaji mganga kuliona au Nabii kutuambia kuwa sisi ndio kisababishi sababu ya utulivu kuwa zero kipindi cha usichana wetu.

Tunaweka sana miili yetu rehani kwasababu ambazo miaka 10 ijayo tunakuja jua tungeweza ziepuka. Hebu imagine kuna dada alilala na mume wa mtu, n hata kuingiliwa kinyume ili kununuliwa iPhone 7+ leo hiyo simu thamani haina tena yeye kashafanyiwa hayo atakuja mwambia nini mtoto wake hiyo story ikitoka nje na tunajua wanaume hawatunziani siri.

Mambo yalikuwa mengi sana kwakweli......
 
Ni mwiko kuipigia hesabu pesa ya mwanamke katika matumizi na majukumu ya kifamilia kama mume unacover bills zote muhimu hakikisha malazi, mavazi, chakula na ada za watoto shule unazilipa. Pia vijana msiogope sana kuingia kwenye ndoa mana changamoto na mapungufu ya ndoa hutofautiana baina ya ndoa moja na nyingine.
 
Mimi uyo

Wanaume huwa hawaoni haja au ulazima wa kutoa pesa kwa mwanamke ambaye hajawa rasmi kwao yaani ambaye sie mke wake na mama wa watoto wake.

Wanasema mwanaume husikia wepesi kutoa pesa yake akijua inakwenda kwa mwanamke anaemlelea watoto wake ambayo ni damu yake. Hapo atajitoa bila shida labda awe hana na mambo ni magumu kiuchumi.
 
Niliwai muuliza ili swali ex wangu mmoja, nikaishia kupigwa tofali (BLOCK)

"Wanawake huwa tukiulizwa katika mahusiano kabla ya ndoa, ukitoa sex, ni kitu gani ambacho tunaoffer kwenye mahusiano kama mchango wetu kama wanawake huwa tunakosa majibu sababu ya uelewa mdogo wa majukumu yetu."
 
Positive kabisa hzo hoja.

Nisababu ya wanawake wazuri wengi hawaolewi kwakua wanafikiria uzur wao tu bila kuwa na msaada kwa wenzi wao nakupelekea kukosa akili yakimaendelea na kuwaza competition waliyokuwa nayo kwa wanaume.

Mwanamke akiwa wakawaida anafocus sn kuwa msaada na akili kwa wenza wao inakuwa vzur kutumu sn.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom