Wadada na waume za watu

Wadada na waume za watu

Spirit

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2013
Posts
457
Reaction score
383
Habari wapendwa,

Wadada leo naomba tujikumbushe kitu kidogo hapa :- Ni kuhusu kuchagua watu wa kuwa nao kwenye mahusiano mf: -kumezuka wimbi la wasichana kupenda kutembea na waume za watu kisa wapate pesa za kujikimu kimaisha kwa upande wangu mimi naona tunakosea sana hiyo tabia na kwanza utachelewa sana maisha kwa kupenda vya dezo mwisho wa siku vitakutokea puani wewe msichana mdogo umeng'ang'ana na mizee isiyojiheshimu kisa anakupa hela na bora hata iwe hela sasa 50000 huoni kama ni dharau?

Yani kakuona jalala la kumwagia taka mwili wake puu! Kwanini wadada tusijikite katika kutafuta maisha? Mume wa mtu akikutongoza ujue kakuona wewe ni dastibini zile za barabarani ambazo kila mpita njia anatupia taka na kwenda zake, yani limtu na mauchafu yake wewe unalikubali maana hakuna malengo yoyote kawashwa huko kaona aje kwako ni bora utulie upate wako asiye na mke ukipenda vya dezo utatumika hadi utakuwa unatembea upande upande.

Tuacheni jamani.
 
hahahahahahah skuiz nazana hata fisi haifiki 50000 ? 😵 watu wanakubali hata 30000 wewe fisi waliona halina maana ? asee
 
eti kutembea upande ? okey ujumbe mzuri sana wakukusikia na wasikie tu ... kukubali kupewa elfu hamsini ni upungufu wa mipango...... me huwa nasema tembea na mume wa mtu jua unataka nini kwake kama ni pesa iwe ya maana na hakikisha hatesi familia yake kwa ajili yako ukiweza hii principle basi utakuwa ni wale washindi wachache ........... ila pia uzinzi ni dhambi na jiandae pia kuja kuliwa mumeo incase ukiolewa malipo ni hapa hapa duniani...... huwa nawauliza hivi ukija kusikia mumeo anatembea na demu mwingine utajisikiaje HUWA MNAJIBU KWA UJASIRI HAWEZI NA MIMI NAJUA NJIA ZOTE ZA KUMBANA , MY DEAR KEEP IN MIND UKILA VYA WENZIO NA VYAKO TUTAVILA TU RAFIKI.. kila la heri
 
Dada naona unawapeperushia watu viwanja vyao vya mazoezi!!
hao wadada wa ivyo wanaitwa viwanja vya mazoezi ukitoka mazoezi unaenda kwenye mechi sasa kwa mkeo!!
Unaweza ukamuita ni jini mkata kamba mvunja ndoa za watu
 
Habari wapendwa. Wadada leo naomba tujikumbushe kitu kidogo hapa :- Ni kuhusu kuchagua watu wa kuwa nao kwenye mahusiano mf: -kumezuka wimbi la wasichana kupenda kutembea na waume za watu kisa wapate pesa za kujikimu kimaisha kwa upande wangu mimi naona tunakosea sana hiyo tabia na kwanza utachelewa sana maisha kwa kupenda vya dezo mwisho wa siku vitakutokea puani wewe msichana mdogo umeng'ang'ana na mizee isiyojiheshimu kisa anakupa hela na bora hata iwe hela sasa 50000 huoni kama ni dharau? Yani kakuona jalala la kumwagia taka mwili zake puu!! Kwanini wadada tusijikite katika kutafuta maisha? Mme wa mtu akikutongoza ujue kakuona wewe ni dastibini zile za barabarani ambazo kila mtu anatupia uchafu maana hakuna malengo yoyote kawashwa huko kaona aje kwako ni bora utulie upate wako asiye na mke ukipenda vya dezo utatumika hadi utakuwa unatembea upande upande tuacheni jamani

Mimi wala sijaoa bado...tutembee tu
 
Back
Top Bottom