Wadada Msipende kula pesa za wanaume ambao hamna future nao. Zitakugharimu!

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,619
2,997
Inaaminika kuwa ni ujanja kula Hela ya mtu na kukimbia na kutangaza kuwa sio taipu yangu, mshamba, kajipendekeza etc.

Spiritually ( kiroho) mtu akikupa kitu chake, ukapokea, tayari umejiunganisha naye chochote atakachotamka dhidi yako kitakupata, akikulaani, laana hiyo itakupata, hujaolewa/ Mwanaume hujaoa jichunguze wanaume/ wanawake uliokula Hela zao Kwa madharau wamekulaani bila wewe kujua.

Epuka utumwa Kwa wanaume au Wanawake Kwa kutosheka na ulivyonavyo,acha kujifunga mguu mwenyewe na kuomba watumishi wakuombee!

Kuna Dada kutoka Dodoma, Mwimbaji wa nyimbo za injili, alinieleza shida zake,alisema anahitaji nauli kuja Dar es salaam.

Nikamtumia Hela,niliona kweli ana kipaji na Mtumishi wa Mungu,kumbe alikuwa tapeli, sikumsikia baada ya kupokea ule mwamala, imepita miaka miatatu kaanza kunitafuta, nilishamsahau,kajieleza,anataka mawasiliano namimi! Nikagundua ni Hela zile zinasumbua nafsi yake!

Elimu ya Bure,Mwanadada/ mwana kaka,kaa Mbali na utumwa wa pesa za watu Ili kuishi maisha ya Utulivu mbele ya safari.
 
Usitutishe wewe tutakula na hamna kitu utafanya
 
Hata mimi nimewahi kumtongoza mdada mmoja hivi kumbe alikuwa na mtu wake mimi sijui,akawa ananiomba hela nampa,kila akiniomba hela namtumia baadae ghafla akakata mawasiliano baada ya chenga nyingi za kukwepa kwenda faragha,sh Kama laki moja na nusu mdada alichukua ila kwa awamu

Baadae nami nikapotezea baada ya kukata mawasiliano nikasikia ameolewa na jamaa,basi maisha yakaendelea,baada ya mwaka mmoja mume wake akamkimbia kwa sababu ya ugumu wa maisha na mwanamke alikuwa mjamzito ikabidi mdada arudi kwa wazazi
Ghafla nakutana na missed call,kupiga akajitambulisha,nikasema poa tupo,baada ya siku kadhaa akatuma sms anaomba nisimkaushie pia nimpende Kama zamani
Nikamwambia "Nikamwambia si ulijifanya mjanja kula hela yangu na kunipiga chengaa ukaona wewe mjanja,wewe pambana na hali yako haupo moyoni tena"
Hakujibu sms akakaa kimya Kama mwezi akanitafuta tena akiniomba tuwe marafiki tu wakawaida nikasema haina shida,kesho yake jioni akatuma bonge la sms akiniomba nirudishe moyo wangu nimpende anajutia kosa mwishoni akaniomba niwe karibu na yeye kipindi hiki kigumu cha ujauzito na pia nimsaidie matumizi na fedha ya kwenda kujifungua

Niliguna tu,hata sikujibu sms, akawa akituma sms sijibu,akipiga simu sijibu akaamua kuacha na mtaani hakutaka tukutane uso kwa uso, nikasikia ameenda kuishi kwa dada yake,
Wanawake bwana wanajisahau sana
 
Wanazingua sana Hawa viumbe,wakila Hela zako hawakusahau maisha yao yoote,hasa ukitenda wema akalipa ubaya.
Mimi Kuna Dada mwingine,alinitapeli Hela Kwa kuuza vitu mtandaoni,karibia 400,000 nilimsihi arudishe Hela kwakuwa vitu nilimrudishia,akagoma.nikafuta namba yake nikaendelea na maisha,nikamuonya kuwa unajiharibia watu wa kukusaidia siku ukiwa na shida.imepita miaka miwili,ananitafuta,miezi minne aonane na Mimi anashida,mumewe kamtelekeza na Watoto! Usile Hela za watu,zinakutia utumwa na kukufanya urudi ulikokula Hela zao
 
Na kuna watu anaweza kukukopesha hata 10m, lakini wala hakusumbui kukudai muda ukifika... Ukimtapeli wala haangaiki na wewe, wapo watu wa hivi tena wengi tu

ila ukae ukijua pesa yako utakayokuwa unaipata haikai, inapotea potea hovyo, unakuwa mtu wa kulalama kila siku
 
Kweli Mkuu,Kuna watu niliwahi kuwakopesha,kuwasaidia,Mimi sikumbuki,ila nikionana nao wamechoka,wananieleza nilivyowakopesha,hata sijui ni lini na kiasi gani.nafuu anayekudai Kuliko anayekaa kimyaa.
 
Principle ni moja tu...

Toa pesa kwa mtu ukiwa na nia nyeupe ya kumsaidia...
Kwako unakuwa huna hatia,ila mpokeaji anakosa amani.anajiona ana deni.sio tabia nzuri kuombaomba Hela, kwakuwa unafungua mlango wa uhalali kwako.chochote utakachomuomba ukikwama hawezi kukataa kukupa
 
Back
Top Bottom