Wadada kwanini mnapenda kutumia neno 'my'?

Hilo neno ni pendwa mno na makundi yafuatayo.wanawake,mashoga, na viongozi wa CCM ngoja waje kutuambia kwanini wanalipenda
 
Imekuwa kawaida mabinti kuwaita vijana "MY" wakati wa kuchat, either WhatsApp, Facebook, Sms n.k. Sasa mi najiuliza hii sentesi nusu "My..." maana yake nini?
Ni maneno gani huwa yanaachwa bila kumaliziwa hapo mbele ya "My..."?

Sijui wengine mnajisikiaje kuitwa " My..., ila Binafsi huwa sipendi kabisa kuitwa "My" ovyo ovyo, maana unafanya nijiulize maswali mengi kichwani, My, nani sasa? My husband? My boyfriend? My love? Au my nini? Hili neno liko romantic kidogo hasa linapotamkwa kwa jinsia tofauti!

Sasa kwa nini wadada mnapenda kutuita "My..."?

Na kwa nini huwa mnaishia hapo My? Si muwe mnamalizia mfano my friend, au my babe n.k,

Na je wanaume wenzangu mnajisikiaje mnapoitwa na wadada My?
aisee dem akiniitaga my uwa cpend sana mkuuu
 
Back
Top Bottom