Wadada kwanini mnapenda kutumia neno 'my'?

Imekuwa kawaida mabinti kuwaita vijana "MY" wakati wa kuchat, either WhatsApp, Facebook, Sms n.k. Sasa mi najiuliza hii sentesi nusu "My..." maana yake nini?
Ni maneno gani huwa yanaachwa bila kumaliziwa hapo mbele ya "My..."?

Sijui wengine mnajisikiaje kuitwa " My..., ila Binafsi huwa sipendi kabisa kuitwa "My" ovyo ovyo, maana unafanya nijiulize maswali mengi kichwani, My, nani sasa? My husband? My boyfriend? My love? Au my nini? Hili neno liko romantic kidogo hasa linapotamkwa kwa jinsia tofauti!

Sasa kwa nini wadada mnapenda kutuita "My..."?

Na kwa nini huwa mnaishia hapo My? Si muwe mnamalizia mfano my friend, au my babe n.k,

Na je wanaume wenzangu mnajisikiaje
mnapoitwa na wadada My?
Mhh hili wenge .
Sema hao unaochat nao ndo wanakwita my
Ongea nao tu vzr utatumiwa msg za kiume
 
Mimi hilo neno lilisha nisumbuaga sana ila nilisha bata jibu.najibulake ni ukiona anakuita hivo ujue anahitaji uhusiano .ila wanambinu nyingi sana
 
Hili neno nalichukia sana ila nafikiri ni matamshi ya neno la kiingereza mine sasa sisi waswahili neno la mwisho lile huwa hatukisikii tukafikiri linatammkwa my... ila sipendi na wale wanaofupisha maneno P kuwa poa na K kama OKEY nayo siyapendi pia
 
linanikera sana

huwez amini na wanaume pia wanalitumia... hasa kwa lugha ya kiswahili....."wangu"
Kuna jamaa mmoja ananikera sana kila tukichat hakosi kuniita best

Mfano:: poa tu best sijui wewe

Hua natamani nimchane kua sipendi huu msemo wake
 
Back
Top Bottom