Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 6,319
- 11,893
Pengine ni karne iliyojaa mabadiliko ya kila namna kuanzia, kufikiri kwa mwanadamu, masuala ya kijamii, kiuchumi, na nyanja nyingine zote. Kwa kawaida mabadiliko katika dunia hayana budi kutokea. Mambo yamebadilika kwanini mnababaika?
Kipindi hiki cha mabadiliko makubwa kinawachanganya mabinti wengi sana, na kuwaweka katika hali ya mawazo na kuchanganyikiwa huku wakiwa na hasira kwa kila siku inayoongezeka. Fujo hizi mara nyingi huanza binti anapotimiza miaka 20 na kuanza kuhesabu kwenda mbele 21, 22, 23, 25, 29 na kuendelea.
Katika umri huu mabinti wengi hutamani sana kuolewa na kuona kuwa kuolewa ndicho kitu muhimu sana katika kipindi hiki na kusahau hata kufanya mambo mengine yanayoweza kuwakwamua kiuchumi na maendeleo mengine.
Ni katika kipindi hiki kilawanamke hutamani kusikia "nitakuoa" bila kujali kama ni uongo au ni kweli! Kama unabisha embu jiulize mpaka kuolewa kwako umekwisha ambiwa neno hili na watu wangapi? Au pengine bado kuolewa. Au Sisi wanaume tumewahi kudanganya kwa kauli hii wanawake wangapi na mwisho anayekuja kuolewa kweli ni mwingine.
Swala la msingi hapa ni kwamba wanawake acheni kubabaika katika umri huu wa 20's. Ndoa siyo suala la kulazimisha au pengine umri unakusukuma kuolewa pasi na kuangalia vitu vingine vya msingi unaamua bora tu liende maadam umri haukuruhusu tena kusubiri.
Ingawa suala hili siyo la kuingilia kati kama nifanyavyo kwakuwa kila mtu ana uhuru na maamuzi juu yake, lakini ni vyema kuwagutua ninyi mabinti kuwa mambo yamebadilika, umri wako usikubabaishe na kuwa mtu mwenye mawazo kila Mara! fanya mambo ya kukusaidia na kukuimarisha hata ukiingia katika mtego ukadanganywa mwisho ukabakia kuwa single mother maisha yataendele.
Unajua nikwanini zile daladala zinazotoka taifa siku ya mechi hata konda akisema nauli ni 2000 out of 400 watu wanapanda? Nikwasababu usiku unaingia na pengine hakuna usafiri mwingine. Huu ni mfano halisia wa dada zetu walivyo kwa sasa, wanapigana na umri huku wakifanya fujo ya kutaka kuolewa!
Anyway, suala la ndoa ni lakuja sio la kufanyia fujo, siyo suala la kukufanya uwe na mawazo muda wote huku sisi wanaume tukizidi kupiga hatua... Ambapo mwanamke unakuja kuolewa ndipo unanza moja kufanya mambo yako ya msingi..
Dada zangu, kuolewa kukukute unapambana. Kwenye karne hii "baharia" atapenda mwanamke wake aliye naye nyumbani anaonesha mafanikio hasa ya kiuchumi. Anyway, mtasema ni mtazamo wangu lakini ndivyo ilivyo, maisha yamebadilika sana.
Haya ni mawazo huru.
Hivyo makubaliano yeyote yanaruhusiwa.
Ukiwa na jambo la kusema niandikie.