Inakuaje unafika30 hujaolewa mwanamke? Unasoma.?? Unatafuta bil gate... Wala tusiwatetee ni wajinga. Unatakiwa ukidika 30 atlist unamtoto mmoja wa ndoa... Na mfie huko bali nyie vibibi mnaojiona watoto na kuwanza ndoto za mchana za kumpata kama mtu mengi... Hamuushi kujua kila aina za vilabu mjini...shenzi type... Huwezi sema umekosa wa kukuoa...endelea kula starehe hadi upate makunyanzi maana yashawaanza
Acha uongo wewe...jinsi ulivoandika unaonekana kabisa kwamba una msongo wa mawazo lini na we utaolewa japo kwa wiki afu uachike uendelee kula mipombe yako na kusema niliolewaga
I couldn't agree moreComparison is the thief of Joy....maisha ya kujilinganisha na fulani ndo maana wanakuwa na visirani....na wanatoa nafasi ya watu kuwaumiza kwa masengenyo....wanasema kill them with happiness. lakini wakiendelea kuwa watu wa kulalamika,wanyonge na kuona kama kutokuolewa ni aina fulani ya ulemavu au laana na kuwa desperate wataishi kwa taabu sana.
Ukweli utabaki kuwa kuna vitu haviko ndani ya uwezo wako,huwezi lazimisha mtu akuoe au aone unafaa kuwa mke,ukifanya hivyo una utumwa wa maisha,kufurahisha dunia kumbe ndani unaungua..kaa karibu na Mungu wako na mwambie mapenzi yako yatimizwe,unipe furaha kwa lile ninalodhani nalihitaji ila hujanijibu kwa kuwa sababu waijua wewe.
Usijiulize nilipanga? kwa ufupi ni machache sana unayopanga,hukupanga kuzaliwa,kuwa mwanamke,kuwa na elimu uliyonayo,kuwa na mafanikio uliyonayo au hata mapungufu....acha kupoteza muda na maswali usiyoweza pata majibu mazuri, labda ujiulize mienendo yangu na tabia zangu zinawavuta watu sahihi kwangu?
Ukimaliza muombe Mungu na urekebishe pale inapobidi the rest muachie Muumba wako aliyekujua hata kabla ya kutungwa tumboni kwa mama yako.
Last but not least....bado unaishi...subira na moyo wa shukrani kwa mazuri uliyonayo itakupa amani. Usiishi kuhesabu uliyokosa tu,tizama Mungu aliyokupa.
Nitampeleka makorora aka dunia hotel tukale uwono fest kilasi
Bomba sana katibu wangu......Ndiyo maana wewe ni jembe...
By the way, nimeambiwa kuwa mgeni wetu hajafikisha 30!! (Take note katibu, na wajulishe wajukuu wengine)!!
Bomba sana katibu wangu......Ndiyo maana wewe ni jembe...
By the way, nimeambiwa kuwa mgeni wetu hajafikisha 30!! (Take note katibu, na wajulishe wajukuu wengine)!!
He he he he he,bibi alinifundisha last time nilipokuwa hapo kuwa girls don't tell their AGE na ikibidi then minus 3 ndo useme ni miaka yako. Sababu hakunipa ila kwa kuwa bibi ana nia safi na mimi bila kuhoji natii ushauri wake....!! 😛opcorn:
Nitake nini mimi dunia hii,asante sana Babu DC hakuna kitu kizuri kama mwanaume anayeamini mikono yake ni salama na yuko tayari kutunza binadamu mwenzie kwenye mikono hiyo salama....wenye hela na wazuri wako wengi ila wenye mikono salama ni wachache sana dunia hii....happy!
Halafu umeona kuwa babu hajataja figure?
Kwa uzoefu wangu kutaja umri wa binti au mwanamama ni sawa na kumwambia kuwa huna hamu naye...
How can I do that to Michelle?
Babu DC!!
Hayo mabusara umeya-copy kutoka wapi mjukuu wanangu?
Rest assured, Katibu wetu na Tanga team ni watoto wazuri sana ambao wamewekewa mikono na Babu..
cc: Mwanyasi
Yaani imekua tabu watu hawali vikalika, hawasomi vkasomeka hawatulii makazini kisa kuwasema wadada wa watu.
Hivi jiulizeni kuna mtu anapenda kufika 30 bila kua na mahusiano ya kueleweka.
Hakika hayupo, na hii inatokana mara nyingi na kutojaaliwa maybe kutokutana na yule mwenye vigezo uvitakavyo. Ukizingatia husband material wachache sana siku hizi.
Na ndoa nyingi za vijana full kulazimishana lazima unioe dot com. Mara nying na mimba juu! Na kwa mwanamke mwerevu anayejitambua sidhani kama yuko tayari kuolewa na mtu baki tu eti kisa 30 inakarbia.
Jamani tukubali msingi wa ndoa ni upendo kama hawajaridhika na watu wa kuwapenda for life (katika magonjwa na afya).
Muwaache hakuwapanga iwe hivi inaniuma kuona mnawasakama hadi mnawa affect kisaikolojia. Imagne mume anayefaa humuoni bado jamii imekuandama.
Nilipanga mimi? Mnapelekea watu kuwa na visirani vya ajabu maofisini, nyumbani n.k let them live their lives, kama we umebahatika kuwa na happy family am happy 4 you.
Wadada wa watu muwaache
JS - kuzeeka siyo miaka tu uliyoishi duniani, lakini pia na maisha uliyoyaishi duniani...Kwamba tumezeeka sana si ndio?