Askofu Kakobe awaonya mitume na manabii juu ya huduma ya maombezi

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
BREAKING NEWS: ASKOFU KAKOBE AWAONYA HAWA
MITUME NA MANABII KUACHA KUJENGA
KANISA KWA MSINGI WA MAOMBEZI
Na mwandishi :Shujaa Charles Richard Mwaisemba (CRM)

Mapema katika ibada ya Jumapili iliyopita ya tarehe 7/10/2018 katika Kanisa la FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP{FGBF} ,Alisikika ASKOFU MKUU ZACHARY KAKOBE wa kanisa hilo akizionya na kuzishauri hizi huduma zote za Maombezi au Makanisa yanayojiita Makanisa ya Maombezi hasa zinazoongozwa na hawa MITUME NA MANABII na watumishi wengineo kuacha kujenga Kanisa kwa Misingi ya Maombezi ambapo alidai MAOMBEZI HUZAA KANISA DHAIFU.
Askofu Kakobe
ameeleza Kulianza kuongozeka kwa kasi kubwa Vuguvugu hili au wimbi hili la huduma za maombezi kila mahali na kila kona katika nchi yetu Mwaka 2003 mara baada Kongamano la kihistoria la wachungaji na Maaskofu wa madhehebu ya kipentekoste lenye zaidi ya wachungaji zaidi ya 12,000 ambalo ndipo alifundisha namna ya kuanzisha huduma hizi za maombezi ambazo zilikuwa ngeni sana katika nchi yetu na ndipo moto wa Vuguvugu hilo lilipoanza
Askofu Kakobe aliyaongea hayo kwa Mamlaka kubwa akisema kuwa ana haki na Mamlaka ya kuongelea juu ya huduma hizi za maombezi katika nchi yetu kwasababu yeye kama Baba au Mwanzilishi wa kwanza katika nchi hii kuanzisha huduma hizi za maombezi mapema katika kanisa lake kuanzia December 1991 ambazo zilikuwa ngeni sana katika Kanisa la Tanzania na ndizo zilifanya watu wengi kumuminika maelfu kwa maelfu kutoka kila mahali nchini hata kupelekea wengi kudhani labda anatumia nguvu za giza
Lakini Askofu Kakobe aliendelea kueleza Pamoja na kuanzisha Huduma hiyo ya Maombezi mwaka 1991 , lakini alisema Kanisa lake la FGBF halikuanzishwa kwa Msingi wa maombezi.Alieleza kuwa kanisa la FGBF lilianzishwa APRIL ,30 1989 likiwa na washirika 13 ambapo liliendesha ibada zake Kwa kuwajenga watu kwa mafundisho ya ndani sana ya usafi na utakatifu,na walikuwa wakichambua maandiko , mstari kwa mstari, aya kwa aya na sura kwa sura kwa masafa marefu sana ambapo hapo baadae kidogo Mwaka 1992 ndipo walipotumwa Wachungaji wao wa awamu ya kwanza waliotokana na Msingi wa Neno kwamaana alisema kati ya wale 13 ndio sasa ni Maaskofu wakuu wa Majimbo wa Kanisa hilo kote Tanzania ambao katika wote hakuna aliyeokoka au kupatikana kwa msingi wa Maombezi na ndio wanaolifanya kanisa hilo kuwa imara hivyo lilivyo pamoja na makelele na vita vyote vya serikali na makanisa mengine wanaoipinga huduma hiyo
Askofu Kakobe alisema kutokana na Uzoefu alioupata na shule ya Roho mtakatifu aliyomfundisha katika utumishi wake kwa muda wote alieleza kuwa Tangu aanzishe huduma hizo za maombezi mwaka huo 1991 ndipo kanisa lilipoaanza kuwa dhaifu na ndipo wote waliozaliwa baadae kwa msingi wa maombezi ndio hao ambao walikuja kulitesa kanisa na ndio walikuja kutikishwa hata kupeperushwa na upepo na mafuriko yaliyokuja kulipiga kanisa , na kwasababu walijengwa juu ya Mchanga si juu ya mwamba.Hivyo ndipo alipofundishwa na Roho mtakatifu kuwa MAOMBEZI HUZAA KANISA DHAIFU
Hivyo Askofu Kakobe aliwataka Watumishi wote wa Mungu, Mitume na manabii wote ambao walimfuata nyuma yake katika huduma au katika utumishi kupenda Kujifunza juu ya mapito walioyopitia watangulizi wao katika huduma ili wao wasije wakapita katika makosa yale yale waliyopitia wao {AYUBU 8:7-10}.Hivyo aliwataka wawe wanyenyekevu na kukubali Kufundishika kutoka kwake kama Baba yao aliyewafundisha juu ya huduma hizo za maombezi ili waweze kurudi kwenye Msingi Imara Kwa kuwajenga watu kwenye neno badala ya Maombezi
Hivyo sasa ndipo Askofu kakobe akaanza Kueleza sifa za watu ambao wamejengwa juu ya Maombezi jinsi ambavyo wasivyoweza kustahimili kuendelea kukaa katika imani hasa pale wanapopitishwa katika majaribu na mazingira ya MAUDHI,ADHA, MATESO, MAGONJWA NA SHIDA MBALIMBALI.Alieleza kuwa watu wa maombezi Hawezi kutoa bali ni mtu wa kupokea na vile vile ni watu ambao hawawezi kuomba mwenyewe bali ni watu wanaosubiri kuombewa na SUPERMAN Fulani Mtumishi Fulani maarufu, mwenye Upako maalum wa kuombea
Askofu kakobe aliendelea kukazia sana juu ya msingi mbovu unaojengwa na hao mitume na manabii katika maombezi yao ambayo yanawafanya watu kuamini juu ya vitu tangible kama Mafuta ya Upako ,maji ya Upako n.k ambavyo vinauzwa ambapo watu wanaaminishwa vitawaponya pale wanapojipaka na kunyunyiza badala ya kuwajenga juu ya Yesu Kristo na kujiombea wenywe badala ya kutegemea kutumia vitu hivyo kwa namna ile ile ya waganga wa kienyeji
Vile vile Askofu huyo alikemea zaidi tabia ya Mitume na manabii hao wanaowajengea watu wanaombewa kuwa wao(watumishi) ndio Superman Fulani ambaye ndiye Mungu anamsikiliza sana kuliko wengine.Kakobe alisema huo ni uongo maana Hakuna Mtumishi Fulani special, maarufu ambaye eti Mungu anamsikiliza kuliko wote bali alisema sisi sote ni watoto wa Mungu na ahadi ya Mungu inasema Kila atakayemuamini Yesu basi ISHARA NA MIUJIZA NA MATENDO MAKUU YATAFUATANA NAE
Hivyo Askofu aliendelea kusema Kanisa halipaswi kujengwa juu ya mtu Fulani kama Superman ambaye yeye tu ndiye anasikilizwa na watu wote waende kwake kutafuta ufumbuzi wa matatizo bali kanisa linapaswa kujengwa juu ya Yesu na kumuinua Yesu zaidi kuliko majina ya watumishi hao maana si kwa jina la Mtumishi Fulani mkubwa bali kwa jina la Yesu, sisi kama watoto wa Mungu tukiomba tunapokea
Vile vile Askofu Kakobe aliwataka Watumishi wote wanaojenga makanisa kwa msingi wa maombezi kufuata kielelezo cha Yesu Kristo ambaye alilijenga Kanisa chini ya misingi ya mitume na manabii ambao ni wale wanafunzi 12 ambao hakuna aliyepatikana kwa maombezi maana wote walijengwa kwa misingi ya Neno isipokuwa Yuda ambaye ndiye alimsaliti ili kutimiza unabii wa maandiko. Katika hao 12 wa Yesu ndio haowalioweka msingi wa kanisa la kwanza
Zaidi sana Askofu huyu alielezea katika LUKA 12:1 Kuwa pale Watumishi wa Mungu wanapojenga kanisa kwa msingi wa maombezi basi linakuwa halitengenezi wanafunzi wa Yesu bali linajaza umati wa makutano mengi ndani ya kanisa ambayo sio kazi au agizo walilopewa na Yesu Katika MATHAYO 28:18-19 la kwenda kuwafanya Mataifa kuwa wanafunzi badala ya kuwafanya kuwa makutano ambao wanakusanyika makanisani kutafuta maombezi ambao wasipopona au kutendewa Miujiza wanayohitaji basi hawataweza kuendelea na imani hiyo
Aliendelea kukazia kuwa wale wote waliojengwa juu ya neno badala ya maombezi ndio wale hata walipopita katika Mazingira magumu kiasi gani Kama Petro aliyesulubishwa kichwa chini miguu juu na kama Tomaso aliyechomwa mkuki ubavuni kule india kwani walikuwa wanafahamu kuwa imewapasa kuingia mbinguni kwa njia ya dhiki nyingi MATENDO 14:19-22
Askofu kakobe aliwapa siri moja wahubiri wote kuwa hawapaswi kuangaika juu ya maombezi na kufanya kanisa kuwa kituo cha maombezi kama hospitali bali Wanapaswa Kulihubiri neno kama lilivyo na kuwaeleza watu juu ya habari ya Toba na ondoleo la dhambi kwa mataifa LUKA 24:47.Alieleza kuwa watakapolihubiri Neno kama lilivyo ndipo Mungu sasa hulithibitisha lile Neno kwa ISHARA NA MAAJABU NA MIUJIZA {MARKO16:20}.Na neno litakapohubiriwa ndilo linalowaponya magonjwa yao maara baada ya kuliamini maana Neno ni Roho tena ni uzima
Askofu kakobe aliendelea kusisitiza kuwa kinachomtisha shetani sio mafanikio yetu tunayoyapata kwa maombezi ila ina mtisha pale anapoleta majaribu ya namna zote Ila mtu hateteleki wala haikani imani.Na akasema kinachomfanya mtu akaweza kusimama hata katika Mazingira magumu ni lile neno lililojaa ndani yao. Na akasema ndio maana Kanisa lake la FGBF kwa muda mrefu sana sasa wameachana na maombezi hayo bali wanadamu kulifundisha Neno kwa masafa marefu lakini bado umati wa watu wanaendelea kukaa na hakuna watu wadhaifu wala wanaumwaumwaovyo na hata wakiumwa wamefundishwa Kumuomba Mungu wao na hivyo kanisa linazid ikukua kwa kasi na kuongezeka kwa neno
Hivyo kwa msingi huo aliwataka wahubiri wale wote ambao ni wanyenyekevu na kumuheshimu kama mzee wao aliyewatangulia katika huduma hizi za maombezi Kuachana na mfumo huu wa kuyafanya makanisa kuwa VITUO VYA MAOMBEZI,MAKANISA YA MAOMBEZI AU HUDUMA ZA MAOMBEZI ambapo yanawafanya watu na kanisa kwa ujumla kuwa dhaifu sana katika imani bali Wajenge kanisa katika kuwafundisha watu Neno la usafi na utakatifu ili kanisa lizidi kusafishwa zaidikwa Nneno maana Yesu yupo malangoni kurudi kulinyakua kanisa hivyo watakatifu wanapaswa kukamilishwa kwa Neno si maombezi. MUNGU AKUBARIKI
Na mwandishi :Shujaa Charles Richard Mwaisemba (CRM)
0712-054498/0759-420202
stnnwaisembac@gmail.com
 
Back
Top Bottom