Kenya kuna mtu anaitwa Andrew Kibe.
Huyu jamaa alinitoa kwenye ujinga mpaka kuwa
kataa ndoa sugu.
huyu jamaa ana nondo, wachokonozi wamwite babu kwa nondo alizokua nazo.
Jamaa alikua anaishi states, alikua anatema nondo mpaka youtube wakafuta akaunti yake.
Kuna kipindi alimshukia rais WILLIAM RUTO, mpaka akapigiwa simu na ikulu ya kenya afute video.
View: https://youtube.com/shorts/SpDnaIbuTGE?si=GtXLQQtdipbSlZXm
Siku hizi video zake ni chache sana zinapostiwa na watu wengine.
View: https://youtube.com/shorts/UlIaRtbLogc?si=3iGhdyPYBRBg0gnU
Jamaa alikua na consistently ile mbaya,kila baada ya dakika chache ana upload video youtube.
Mchizi ndio alikua content creator number moja Africa, na alikua anaingiza pesa ndefu youtube kuliko content creator yeyote.
Walipomfungia youtube alirudi kenya, akaiwekeza hela yake yoote kwenye project ya kuanzisha youtube yake lakini mpango ukafeli hivyo akapoteza hela nyingi sana, lakini bado anapambania.
Wakati sisi watanganyika tukihangaika na upuuzi, wakenya wenzetu miaka 3-4 watakua na youtube yao.
Mastaa wote wa kenya wanamhanya, huwa anawatandika fact tu. Hata diamond anampaga za uso
Nimeanza kumfuatilia tangu yupo kenya vipindi vyake vya rooftop miaka ya 2020 kisha akaja akaenda states, akapiga sana hela ila youtube walipomfungia akaunti yake akarudi kenya.
Huyu jamaa amenifundisha mengi sana
View: https://youtube.com/shorts/COXFroX5zPg?si=FDG9bOYm9XJ6u6f3
Kibongo bongo namuona DUDUBAYA anaweza akafuata nyayo za huyu jamaa kama atatuliza kichwa huyu jamaa.
Mlio karibu na dudubaya mshaurini aache kuhangaika na interview za tu TV twa youtube, thamani yake ni kubwa kuliko hata hivyo vi TV aisee, dudubaya ni almasi iliyo mchangani, ila bado hajajishtukia.
Kizazi kilichopo mtandaoni kwa sasa kina hela nyingi sana ya kumpa dudubaya
Nasema hili nikiwa na uhakika wa asilimia 100%, dudubaya akiwa seriously kwenye podcast yake, anaweza kuwa anaingiza mkwanja mrefu kuliko aliokuwa anaingiza kwenye muziki.
Dudubaya afanye kama alivyokuwa anafanya andrew kibe, jamaa alikua anaenda live youtube hata lisaa lizima, akiongea mambo mbalimbali, kijamii, kuhusu mastaa, anaweza akachukua video iliyopostiwa mtandaoni akaijadili, lisaa lizima unakuta kaongea mambo kibao.
Wakati mwingine anapokea simu na kuulizwa maswali na fans.
Halafu anavikata vipande vidogo vidogo vya dk 1, au mbili, kulingana na vi mada vidogo vidogo alivyoongelea.
Huyo jamaa anaweka number yake live kwenye screen anaanza kumwaga madini(ukiguswa unatoa chochote kupitia MPesa.
Asee kama kuna mtu ana hela, anataka kuwekeza mtandaoni, nenda kajifunze alichokua anafanya andrew kibe halafu wekeza kwa dudubaya utanishukuru.