Wachina wanavyowanyanyasa Watanzania

Wachina wanavyowanyanyasa Watanzania

Kwema wana jukwaa leo nimekuja na hoja jinsi wajina wanavyowanyanyasa wazawa ambao wamewaajiri katika kampuni za ujenzi
Kuna kampuni moja inaitwa Chicco inajenga mto ng'ombe unaopita mitaa ya Sinza, Mtogole mpaka Mkwajuni. Mradi ambao uko chini ya Manispaa ya Kinondoni.

Lakini mwanzoni mwa wiki hii J.tatu waliwasimamisha wafanyakazi wao ambao no mafundi ujenzi kwa miez miwili wakidai wamewapa lay-off bila kuwapa stahiki zao kama pesa ya likizo.

Mbali ya hayo wachina hawahawa wanajeuri ya kuwaambia nendeni kokote mkashtaki. Yaan watu wakihoji kukatwa overtime unafukuzwa.

Sasa wako wapi viongozi wa wawanyonge
wenyewe kwa wenyewe pia tunanyanyasana sana tu
 
ukiamua kufanya kazi kwa wachina kubali yoyote, wana jeuri kwa sababu wana backup nzuri kutoka juu, ni kweli huna pa kuwashtaki
 
Wachina hata kufanya nao biashara ni changamoto sana. Kwa mfano unaweza ukaingia mkataba na makampuni yao ya ujenzi kuwauzia mchanga, kokoto au hata matofali. Kwanza wanakubana sana kwenye bei huku wakihakikisha unaleta vitu quality

Wakati mwingine unalazimika kukubali ukijua kwamba kutokana na volume/quantity wanayokupa basi utatengeneza faida kidogo. Changamoto ni pale anapokuja mtu mwingine akapunguza bei kidogo anaachana na wewe na hawaheshimu mikataba kabisaaa!
 
Kuna siku moja nilikuwa kariakoo.. kwenye duka nililokuwepo pembeni kulikuwa na duka la wachina lenye wafanyakazi waswahili...nakumbuka yule kaka mswahili aliomba ruhusa kwa mchina anajisikia vibaya arudi nyumbani..jibu la mchina alimwambia akitoka pale na kazi Hana..dah!!..yule kaka alitia huruma akataka na kumpigia mchina magoti..bahati nzuri duka la pembeni nilipokuwa Mimi wenye duka waswahili wakorofi wakamwambia mchina ..huyu jamaa anaenda home kupumzika Sasa ole wako kesho umfukuze kazi..mchina alinywea kwa ule mkwara..vijana wafanyao kazi kwa wachina wanatiaga huruma Aisee.
Wabongo bwana ila kwenye siasa mpaka mnauwana na kutiana vilema, tena kwa malipo ya buku 5 mpaka 10 tuu. Huku kwa wachina mnalia lia...
 
Back
Top Bottom