Wachina wajenga maabara MBINGUNI!!!!

Nzowa Godat

JF-Expert Member
Jun 15, 2011
2,759
794
Baada ya kuwapeleka wanaanga wake kwenye safari
za anga ya juu na wanaanga kutembea kwenye anga ya juu
kwa mafanikio, China imepiga hatua nyingine muhimu katika juhudi zake za kutafiti anga ya juu, kwa kurusha maabara yake ya kwanza Tiangong-1 kwenye anga ya juu.

Tofauti na satelaiti au vyombo vya safari za anga ya juu
vilivyorushwa na China hapo kabla, maabara hiyo Tiangong-1 haitabaki angani peke yake, bali itaweza kuunganishwa na vyombo vingine.

Imefahamika kuwa China inatarajiwa kurusha chombo cha safari ya anga ya juu Shenzhou No 8 baada ya mwezi mmoja, chombo hicho kitaunganishwa na maabara
hiyo.

Zaidi ya hayo, katika kipindi cha miaka miwili ijayo, China itarusha vyombo vingine viwili ambavyo pia vitaungana na maabara hiyo. Mambo hayo!
 

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,770
6,521
sasa hawa watawala wapya wa dunia wamebakisha nini ambacho hawajafanya..
 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,973
8,965
ndio ni mbinguni, inategemea ubongo wako unauendesha wewe au umeamua kumpa padre, shekhe au rabi aufinyange anavyotaka! eti mbinguni au angani,malaika,kuzimu, teteteteee!

Nenda waego wachina sisi wazungu na waarabu walifuta hard disk za mibongo yetu,tunatumia theory zao kuishi na sasa tunauna kwa ajili ya maslahi yao.
 

G. Activist

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
482
125
Inawezekana tu, maana Mungu alivomuumba Adam alimuambia nakupa uwezo wa kutawala Anga, Nchi na Bahari!! Kama ukiweza kutawala huwezi shindwa kuunganisha maabara..,.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom