Wachezaji kuishi keko,kutibiwa mwananyamala......

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,063
115,462
Sijui ni mimi peke yangu ninaeshangaa
inakuwaje club kubwa kama simba na yanga
unakuta wachezaji wanatibiwa mwananyama hospitali
wanaishi keko ....
na wengine wa kutoka nje wanaishi mahoteli ya bei rahisi hadi wanaibiwa pesa zao
na kadhalika na kadhalika....

nimesoma sehemu simba walipata almost mil 200 mevhi ya mwisho na ubingwa
bado na udhamini na kadhalika....

achilia mbali kuendesha magari mabovu hadi wanaptwa na ajali......

kuna mtu mwingine labda anaona hii ni sawa?
 
The Boss,
Tatizo siyo kuishi Keko,
Tatizo ni aina ya nyumba wanapoishi.

Kukaa Keko nadhani ni kwasababu ni karibu na viwanja vyao vya mazoezi as well as uwanja wa Taifa.
 
Last edited by a moderator:
The Boss,
Tatizo siyo kuishi Keko,
Tatizo ni aina ya nyumba wanapoishi.

Kukaa Keko nadhani ni kwasababu ni karibu na viwanja vyao vya mazoezi as well as uwanja wa Taifa.

mkuu mimi nina ndugu weengi wanaishi keko
nyumba hata iweje keko ni keko naijua
kwani tandale hakuna nyumba nzuri?

utulivu na amani unaletwa na mazingira pia
keko yote karibu ni surveyed area.....hapa choo hapa kichochoro na kadhalika
 
Keko wanatakiwa waishi kina nani?

sizungumzii siasa hapa
wala wananchi wa kawaida
nazungumzia mchezaji wa timu inayopata milioni 150 na zaidi kwa mechi moja na yenye udhamini.....wa pesa nyingi
kama bahari beach zipo nyumba za dola 1000 kwa mwezi
tuna haki ya kuuliza kwa nini timu iwapangie nyumba keko...
 
mkuu mimi nina ndugu weengi wanaishi keko
nyumba hata iweje keko ni keko naijua
kwani tandale hakuna nyumba nzuri?

utulivu na amani unaletwa na mazingira pia
keko yote karibu ni surveyed area.....hapa choo hapa kichochoro na kadhalika
Kwa hili naona nipingane na wewe, Keko kuna maeneo mazuri sana. Siyo kila sehemu ni uswazi.

Naona tunajidili ni nini kinawafanya waishi Keko, ni kwasababu ya ukaribu na eneo la kazi yao au ni kwasabu ya financial constraints?
 
Tuwekee mchanganuo wa mapato na matumizi ya hizi club halafu utuambie kama kweli mapato yao yanatosha kuendesha hizi club kama unavyotaka. Mechi zinazoingiza Tshs 200 million ni kati ya watani wa jadi na sidhani kama mechi kama ya Simba na Polisi Dodoma inaweza kuingiza kiasi hicho.

Ajali aliyopata mchezaji wa Simba haikutokana na ubovu wa gari. Ajali ni ajali hata gari mpya inaweza kupata ajali.

Hizi kasumba za kuona Keko, Temeke, Mbagala sio sehemu nzuri za kuishi ni mbaya sana.
 
sijasema keko hakufai kushi
nimesema kwa wachezaji ambao timu zao zina mapato ni sawa?

halafu mada inazungumzia pia matibabu
je ni halali kutibiwa mwananyala hospitali?

kama keko kunafaa je rage anaishi keko au mbagala au temeke?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom