Paul dybala
JF-Expert Member
- Jul 30, 2023
- 553
- 2,266
Aisee wakuu,...ndugu yenu saivi yapata siku ya nne silali kwa amani kabisa.
Siku ya jana nikiwa tayari nimesinzia nilishtushwa na kitu ambacho kilikuwa kinanitambaa mkononi kinaanzia kwenye vidole hadi begani.,bhasi nikashtuka nikarusha shuku,nikajipangusa kwa kiwewe huku naweweseka,,nikawaza hichi kinini au naota?
Mda wote huo ni kiza,..nikapata wazo labda nimende au panya nikakimbilia simu huku napapasa bila mafanikio ya kuishika simu,,nikaona tena kitu kama sponchi kinanigusa,,,aisee nilichomoka mbio nikavuta mlango huku nikiwa na boksa hadi sebuleni usiku wa manane nikipiga mayowe,,.
Mimi nimepanga kwenye nyumba ambayo naishi na familia ya mwenye nyumba,kwa hio nipo kwenye chumba Cha ndani humohumo
Wakatoka masister wa mle ndani,, sister mkubwa akawasha taa na kunihoji kunanini? aisee,,nikawaambia Kuna kitu kinanitambaa...Daah yaani taharuki wazee, familia nzima ikaamka ikabidi wote wanisindikize kukagua chumba ...sijapata usingizi kabisa..
Saivi natafuta dalali aisee