Wacha niseme hili wazi

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,576
2,000
Wacha niseme hili wazi
Kwenu
Najua wakaka mtanuna ila bora
Mnune kidogo ili niwaponye
Mabinti zangu
Iko hivi 😍🤔
Asilimia kubwa ya wanaume wanataka kuishi na wanawake bila kufunga ndoa ili ikitokea siku wakaachana hakuna kugawana mali, wengi wanaamini hivyo na ni kweli kugawana mali na mtu ambaye hamjafunga ndoa ni ngumu kidogo ingawa kuna ile sehemu katika sheria inasema kuwa mkikaa kwenye ndoa miaka miwili mfululizo basi inahesabika kama ndoa. Sasa kama mwanaume unaishi naye kashakutolea hata na mahari kwaninia sikuoe kama sikuwa hataki kugawana hicho kidogo alicho nacho!

Hili si tatizo tatizo nikuwa wadada mnapobembelezea ndoa mnakua na vile vimbelembele vyakutaka kuolewa, kujifanya mnajua kushauri mambo ya maendeleo, kujifanya mnataka mfanye mambo kwa mpamoja na hapo ndiyo mnaishia kutapeliwa! Iko hivi kama hajakuoa ndoa ikatambulika si mume wako, fanya mambo ya maendeleo kivyako kwani hakuna upendo hapo, ach aujinga wa kumuamini kila kitu na jina lake wakati yeye hata kukuamini kukuoa hawezi!

Kama ukikutana na mwanaume akakuambia kuwa hataki muoane kwanza unatakiwa kujua kuwa sbabau zanazokupa kuwa hana pesa, kwa wakati huo wakatio anajenga, hajajipanga sijui nini ni uongo. Ishu ni kwamba anapenda kuishi na mwanamke lakini anataka urahisi wa kuachana na wewe, kwamba anataka kuishi na wewe lakini kashajiandaa kukuacha, hivyo ukijitia kiherehere cha kubeba mimba na kulazimisha akajitambulishe sijui nini hayo ni yako yeye hana mpango huo!


WEKA KICHWANI HII NA CHUKUA HATUA NA PIA TAMBUA KUWA
Mwanaume anapoishi na wewe bila ndoa hua anakuchukulia kama unajaa tu ya maisha, hunamalezi ndio maana wazazi wako wamekuruhusu, huna namna imebidi uishi naye tu ili siku ziende, hivyo anakuchukulia kama mtumwa wake tu, hata kama akikucheat anaamini utamuvulia kwani we upo kwa ajili ya kufadhiliwa maisha yako hivyo kwa ufupi hutakua na heshima yoyote..
Ufanyaje?
Ujinasuaje?
 

Pazi na Jogoo

Senior Member
Aug 12, 2016
152
250
Kwanini uishi na mtu kwa lengo la kuachana baadaye, huoni kama unapoteza muda na ikiwa ndo umezalishwa ndugu uwe makini maana saiv wanaume hatutaki ujinga wa kuoa mwanamke aliyezalishwa na kuachwa na mumewe wa awali maana hapo usaliti ni nje nje!!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ezekiel Mbaga

Verified Member
May 28, 2018
5,497
2,000
mali nitafute mwenyewe kwa jasho langu halafu ety kisa ndoa mali nigawane na mwanamke.! labla kama nae alizihangaikia na sio amekalisha makalio tuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom