Wacha nimpe darasa kidogo Mzee Jakaya Kikwete

Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

Kikwete ambaye marehemu Askofu Getrude Lwakatare alikuwa mbunge kupitia chama chake CCM na hakuwahi kuitoa kauli kama hiyo anayoitoa sasa. Kikwete ambaye Askofu Gwajima anayezunguka kuhubiri nchi nzima huku akitumia madhabahu kumnadi Rais Samia, wabunge na madiwani kwenye madhabahu na Kikwete alichagua kunyamaza. Kikwete ambaye Sheikh Mkuu wa Dar es laam Sheikh Walid Alhad aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Malezi wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Dar es laam, Kikwete alichagua kukaa kimya. Nini kinamtoa pangoni sasa?

Kwanza, upo uwezekano kuwa yumo kwenye scandal ya bandari kupewa waarabu so anatetea mkate wake wa kila siku.

Pili, anaona CCM chama chake kinaenda kuanguka kwa kukosa ushawishi kiasi kwamba sasa wanaogopa nguvu ya maaskofu katika ku speedup anguko la CCM kutokana na uovu wao.

Tatu: Unafiki.

Sasa wacha nimpe Darasa.

Mzee JK akimuona askofu ajue huyo askofu ameshirikishwa Ukuhani, Unabii na Ufalme wa Kristu. Leo nitazungumzia unabii tu na nitatolea mifano ya manabii wawili, Nabii Samweli na Nabii Nathani.

Zamani Mungu aliwatumia manabii kuwapaka watu mafuta ili wawe wafalme rejea 1 Samweli 9:17 "Huyu ndiye mtu niliyekwambia habari zake! Yeye ndiye atakayewatawala watu wangu". Hapa Nabii samweli anaambiwa amsimike mfalme Sauli kuwa nabii wa Israeli. Hii hata nchini kwetu huwa tunafanya, wakati wa kumuapisha Rais viongozi wa dini wanaalikwa ili washuhudie ama kushiriki kumsimika Rais mteule.

Hata katika kumkataa mfalme Mungu hutumia manabii Rajea 1 Samweli 16:1-7 "BWANA akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israel?". Samweli aliyetumika kumsimka Sauli kuwa nabii, Samweli yuleyule anatumiwa tena kuambiwa kuwa Mungu amemkataa Sauli.

Nafikiri unaweza ona namna dini na siasa zilivyokuwa zikihusika tangu Mwanzo katika kuwaweka na kuwaondoa wafalme.

Wakati fulani mfalme Daud alimchungulia mke wa mwanajeshi wake akioga yule mwanajeshi alikuwa akiitwa Huria. Akamtamani akalala na yule mwanamke, mwanamke akapata mimba, Daud akaagiza mumewe arejeshwe kutoka jeshini ili amlishe, amnyweshe na amuache akalale na mkewe ili ionekane ile mimba ni yake (Deception)

Mwanajeshi akarudi kweli akala na kunywa ila kwa kuwa alikuwa akijua miiko ukiwa vitani huruhusiwi kulala na mkeo hakwenda kulala na mkewe. Mfalme akakasirika akaagiza apelekwe kwenye mapambano makali vitani ili apigwe afe. Kweli akauawa vitani, mfalme Daud akamchukua mke wa yule jamaa.

Mungu akakasirika akamtuma nabii Nathani aende kumuonya mfalme Daud Rejea 2 Samweli 12:1-25 Mfalme Daudi akalia akatubu akisema, “Nimetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu.” Mungu akamsamehe akaendelea kutawala Israel.

Nataka kusema nini?

1. Kama Nabii Nathani (wa dini) alimuonya mfalme Daudi (wa siasa) dhambi iko wapi maaskofu kumkemea Rais Samia?

2. Kama Mfalme Daudi alijua makosa yake akanyenyekea na kutubu na kuacha njia yake mbaya, kwa nini Rais Samia asitazame nyuma na kuachana na mkataba ovu wa Bandari. Ili aendelee kutawala kwa amani bila pressure kutoka kwa umma wa anaowaongoza?

Nafikiri Rais bado anayo nafasi, asimsikilize Kikwete bali aangalie wapi kajikwaa, apige chini mkataba wa bandari, asimame tena asonge mbele akiwa na uhakika kuwa kama kuna mahali alifanya vibaya kwa hila, rushwa ama upendeleo Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema na Neema atamsamehe na kumuimarisha tena maana hatujakamilika huo ndiyo ubinadamu wetu.

La! akishupaza shingo maneno haya yatamuhusu. Arejee Daniel 5: 24-28 Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

Wasalaam
John Pambalu
Pretoria - Afrika Kusuni
21.08.2023
Bro we ni hadhina, umeongea yaliyopo kwenye mioyo ya wengi,
 
Wewe unayetaka kumpa somo JK tuambie uzoefu wako kwenye mambo ya siasa, diplomasia, serikali nk

JK ni mwanajeshi, mwanadiplomasia, mwanasiasa, mbunge wa zamani na waziri wa zamani , rais mstaafu

Naomba na wewe uweke wasifu wako tuwalinganishe halafu utaendelea kumpa somo mzee mwenzako
 
Back
Top Bottom