Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,719
- 5,368
Jana ungetazama jinsi wabunge wetu walivyokuwa wakishangilia Bajeti ilipokuwa ikisomwa ungesikitika sana hasa kama una "akili kidogo"!
Watu hamjakaa mkatafakari bajeti lakini kusikia tu hiki kimefutwa basi pwaaa pwaaaa na kujitoa ufahamu kabisa! Hamjui wasomi wanapoandaa Bajeti wanakupa hiki kwa mkono wa kulia na kukunyang'anya kwa mkono wa kushoto!
Mimi ni MwanaCCM lakini wabunge wetu wengi ni "Mizigo" na watia aibu sana! Wengi wao ni upupu tu hawana muda wa kuchambua mambo!
"Haya ndo Mabunge" ambayo yanapitisha sheria zinazoruhusu Wawekezaji kusafirisha Mchanga wenye madini kwa kasi ya Mwanga(Speed of light),kesho yake Rais akizuia kusafirisha Mchanga wa Madini ndiyo tena yanakuwa ya kwanza kumpongeza Rais eti ni Shujaa na Mzalendo! Vichwa vya Mbuzi kabisa!
Ebu sasa tupigieni Hesabu kwa kodi ya magari iliyofutwa na kupelekwa kwenye mafuta kwa Mwaka mwenye Gari atalipa kiasi gani na athari zingine za kiuchumi kwa kupanda kwa bei ya mafuta itakuwaje! hasa gharama za uzalishaji na usafirishaji!
Tunajua kwa sasa kazi iliyo ngumu kabisa katika Taifa hili ambayo inafanywa na watu wachache sana ni KUFIKIRI! Hata wasomi wetu walishaacha kufikiri kitambo! Eti juzi Rais kuwakejeli Wachumi wetu kwa kutofikiri vizuri kuhusu vyanzo vipya vya mapato,Eti wamachinga,mamalishe wapewe vitambulisho kwa Tshs.10,000/= na wao eti wameweka kwenye BAJETI! Hawa ni WASOMI Uchwara kabisa! Mnachukua 4% kama mrabaha kwenye Madini yetu halafu mnakuja kukimbizana na MAMALISHE na WAMACHINGA,kweli!?
Nchi hii ina kila Kitu ila laana ambayo tulipewa ni aina ya WATU tuliopo humu Nchini,Naomba tufanyiwe tafiti kuhusu "Bongo"zetu! Isijekuwa tuliwekewa Bongo za Wanyama wengine na si binadamu! Kama sivyo kwanini Watanzania sisi ni WABABAISHAJI katika kila kitu !? Kwenye Michezo,Uchumi,Siasa,Elimu ni UBABAISHAJI MTUPU!
Wabunge wa S.T.D 7 (kusoma na Kuandika na siyo hata kuhesabu) kwa sasa hawana TIJA!