Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Hawa jamaa wamejisahau mpaka wamepitiliza!
Hawajui hapo walipo ni kwa niaba ya wananchi ili kutetea maslahi ya nchi. Wanalipwa mishahara minono pamoja na posho mbalimbali kwa pesa (kodi) tunazokatwa kwenye mafuta, mishahara, mazao, madini, tozo, na ushuru mbalimbali kwa kila bidhaa inayopita mikononi mwetu.
Yote hayo tumeyakubali ili wasimamie maslahi yetu sisi wananchi. Lakini wenzetu hawa, pamoja na spika wao ambaye ni mwanasheria, wanagawa lango kuu la uchumi wetu bila hata kuonesha kwamba sisi watanzani tunapata nini cha ziada kuliko sasa?
Kwa namna wanasheria wetu wasomi na nguli; wanavyoendelea kuuchambua mkataba huo wa kinyonyaji.
Sasa natambua kwamba kwa mkataba huu wa bandari, wabunge wetu wametusaliti kwenye maeneo yafuatayo;
Mosi, kwenye uhuru wetu wa maamuzi kama nchi. Pili, Katiba yetu imesiginwa vibaya. Tatu, Kuhafifisha madaraka ya rais wa nchi aliyokabiziwa na watanzania. Nne, wametudharirisha kwamba watanzania ni watu wajinga sana. Lakini sijui watafanya kama vile msaliti mkongwe alivyofanya au vinginevyo?
"Kisha Yuda, Yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema; nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. (Mathayo 27:3)
Hakuna namna wabunge wetu wafuate nyayo za Yuda Iskariote aliyemsaliti Bwana Yesu, ili kulinusuru taifa.
Mungu ibariki Tanzania.