Wabunge wetu tunaomba mtusaidie wahitimu tafadhali,

mumak

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,069
668
Naomba nilete ombi langu humu kwa matumaini ujumbe wangu utawafikia wawakilishi wetu,naomba wabunge wetu mtusaidie kuikumbusha serikiari sisi wahitimu wa vyuo hususana kada ya elimu tupo shidani sana kwani tangu tumemaliza chuo ni miaka miwili inaenda mitatu sasa tumekua mtaani bila ajira,

Serikali imekua kimya wala hatujui uelekeo ,wengine wamefikia kupoteza haiba ya ualimu kwa kuathiliwa na maisha ya mtaani,tumeona bajeti nyingi zinapangwa kwa kusema wataajiri lakini wapi,ualimu ni tofauti na taaluma nyingine kusema watajiajiri au kuomba kazi katika shule nyingine kwani idadi ni kubwa kuliko shule za binafsi,

Pia lazima itambulike kwamba asilimia kubwa ya wanaosoma ualimu ni watoto wa masikini kupata mtaji inakua ngumu pia mahalifa ya ujasiliamali hakuna chuo kilichowaandaa wanafunzi kwa ajili hiyo, na mwisho naomba waishauri serikali kama haina tena uhitaji wa walimu ni bora isitishe kudaili kozi hizo kwani vijana watapoteza mda na serikali itapoteza pesa kwa watu ambao hawaajiriwi ambapo baaadae wanakua wahanga wa wanasiasa.
 
duh naona ajira za ualimu zitakuwa unamaliza 2017 alafu ajira 2o21 maana naona kundi la tatu linakuja mtaani ssa hizo ajira hawawezi toa za graduates wa miaka mitatu waajiriwa wa 2015 alafu wengine wanavuta muda
 
Back
Top Bottom