Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,382
Habari zenu wapendwa,
Ni siku chache tu zimepita tangu kuibuka kwa zogo kama sio mzozo nchi nzima kufuatia kutimuliwa kwa watoto, ndugu au wadogo zetu waliodahiliwa kusomea stashahada maalumu ya ualimu katika masomo ya sayansi na hisabati. Moto huu ulichochewa zaidi na Mh. Rais pale alipowadhalilisha vijana wetu hawa kwa kuwaita vilaza jambo lililoibua mjadala nchi nzima kiasi cha hata wengine "kufukunyua matokeo halisi ya binti wa mfalme ambaye naye yupo chuo hichohicho cha UDOM wala sio kwa stashahada kama wale "Vilaza" bali shahada kabisa tena kwa udahili wa fasta fasta kwani hivi sasa anaufukuzia mwaka wa tatu na wa mwisho wakati kanuni na hatua za kimasomo nchini kwetu hazikubali. Matokeo ya huyu binti mfalme yanaonyesha alipata divisheni foo tena ile ya mteremkoni kabisa kuelekea kule kwa akina sendeka. Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Jesika!
Cha ajabu bunge letu limekubali hoja hii izimwe kabisa! watoto wetu hawa ambao tunaambiwa walipiga zile makisi zenye akili waliamua kusitisha mipango yao ya kuendelea kidato cha tano wakakubali kuwa washika chaki wala sio "makapeni" ni ile chaki yenyewe nyeupe pee na vumbi lake. Tunaambiwa hoja ilipelekwa bungeni, lakini naibu wa sipika yule ambye HAJATULIA aliamua kuipiga roba na kuinyongelea mbaaali! ebo! ina maana hapo ndo mwisho wa mchezo? msiniambie wabunge wote yaani wa CCM na upinzani mmekubali hoja hii ife kifo cha mende? haiwezekani! Hivi mnaweza kunyamaza kweli kwa kile kilichowapata wadogo zetu hawa?
Lakini sitashangaa sana maana hivi karibuni mfuko wa PPF umesitisha mafao ya kujitoa lakini sijaona hoja hii ikijadiliwa bungeni ili kuwanusuru mamilioni ya watanzania maskini wanaodhalilika na kuporwa jasho lao waziwazi baada ya ajira zao kukoma. Sasa hawa wanyonge wakimbilie wapi? ikiwa serikali imewageuka na bunge halijali kuwatetea? Ndio maana nasema sitashangaa sana hata hawa wadogo zetu waliofukuzwa UDOM wakikosa utetezi thabiti wa bunge.