Magufuli 05
JF-Expert Member
- May 7, 2023
- 942
- 1,986
Wabunge wetu mnawawakilisha wananchi wapi? Mbona mmeshindwa kuwawakilisha dukuduku lao la bandari? Je, mlichaguliwa kwenda kumsifu chifu tu? Hivi walioeleza dosari za mkataba ule wote walikuwa na nia ovu kweli?
Kwanini katika bunge la kujadili mkataba/makubaliano hayo hamkujadili issues badala yake mkajikita kushambulia (personalities)
Wabunge wetu nani mnamuwakilisha? Mnasikitisha sana. Nani aliwatuma kwenda kumsifu chifu tu? Kwanini hamhoji mambo ya msingi? Mbunge unaitisha press unatamba weee, nina ndege, nina magari ya bei ghali. Sisi inatuhusu nini? Utajiri ni wako, nchi ni ya kwetu sote.
Yaani kila mbunge anayesimama anasifu tu, ana sifu tu. Kwani chifu ni malaika? Yeye hakosei? Matumbo yenu na uoga wenu ndiyo unaleta yote haya.
Nani kwenye kikao cha bunge maalumu la kujadili mkataba huo aliingia na mkataba whether kwenye hard copy au soft copy walau akasoma hata kipengele kimoja ambacho hakina maslahi kwa taifa letu ili kirekebishwe?
Je, mnadhani wenzetu walioanzisha kampuni hiyo ya usimamizi wa bandari, wana bunge na wabunge kama nyingi?
Wabunge wetu mnasikitisha. Aibu yenu mmehalalisha maoni yenu na si ya wananchi. Kama mkataba huu utaiingiza nchi kwenye hasara kubwa huko mbeleni tutawasaka mmoja mmoja tuwahoji na Watanzania watawapiga mawe.
Mwisho, kama mlichohalalisha jana kina manufaa kwa nchi na hakiidhulumu, Mungu awabariki. Ila kama hamkujali maslahi ya nchi na uzalendo mkawa wazalendo wa matumbo yenu, nawashtaki kwa Mwenyezi Mungu 2025 mkashindwe nyingi wote na chama chenu chote. Narudia mkashindwe kabisa.
Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿