Wabunge wengi wamelala usingizi wa pono. Hawasemei miradi iliyotekelezwa maeneo yao

Nitajie wilaya yenye project hata robo 3 ya hizi!
  • Uwanja wa kimataifa wa ndege
  • Hospitali ya rufaa ya kuhudumia kanda
  • Bandari kubwa na ya kisasa!
  • Majengo ya kisasa ya TRA,Tanesco na Bohari ya dawa MSD!
  • Taa za kuongozea magari!
  • Uwanja wa kimataifa wa mpira wa miguu
  • Chuo kikuu
Hapa achana na miradi kama maji,umeme na vituo vya afya ambayo ni common maeneo yote ikiwemo Chato!
Kwa hiyo ulitaka vijengwe wapi?
 
Yaani huoni aibu kabisa?Watu wa Kigoma,kagera,Shinyanga na Rukwa waende wakatibiwe Chato?Wakati huo huo kuna Bugando mwanza ambapo si umbali mkubwa kutoka Chato,kwanini hospitali hiyo ijengwe Chato?Kwanini isingejengwa hata Nyakanazi ambako ni rahisi kufikika na mikoa hiyo minne niliyotaja na watu wa Chato wakatumia Bugando?Kwanini uwanja wa ndege basi usingejengwa Kahama,mji uliokua kwa kasi sana kibiashara na badala yake ukajengwe Chato!
Yaani uwanja wa mpira wa pili kwa ukubwa nchini ukajengwe Chato,game za taifa stars nyingine zikachezewe Chato,hivi kweli hamuoni tatizo hapo?Kuna miradi kama maji,barabara na vituo vya afya,hivyo hatuwezi kuhoji maana ni miradi ya muhimu kila mahali!Hii mingine hapana!
Nitajie wilaya moja tu nchini yenye miradi Mingi kwa pamoja kama Chato!
Uwingi wa miradi hiyo Chato,hauna uhusiano wowote na Rais kuwa mzawa wa Chato?Hilo ndilo swali la msingi zaidi!
Acheni kupofushwa na mahaba yenu,jambo hili halina afya kwa ustawi wa nchi yetu na umoja wetu!
Kuna kila dalili kila mtu kumchagua mtu kwa kabila lake huko mbeleni kama hali hii haitakomeshwa!
Yaani wabongo mna nongwa, kwani uwanja mkubwa ukijengwa Chato Kuna shida gani? Taifa stars ikichezea Chato Kuna shida gani? Kwani Mikoa mingine hakujengwi viwanja? Chato siyo Tanzania?

Kahama iko mkoa wa Shinyanga ambako Aiport ya Shinyanga inapanuliwa na itakuwa na uwezo wa kupokea ndege kubwa Kama dreamliner. Chato iko mkoa wa Geita, kwa hiyo Aiport ya Chato ni ya mkoa wa Geita.

Kuhusu Hospitali za Kanda nimefafanua vya kutosha wanapoweka location ya Hospitali lazima wafanye tathimin namna gani itanufaisha pande zote. Pia Cha kuongezea location ile itavutia hata medical tourism kwa nchi jirani Kama Uganda na Kenya.
 
Uwanja unaojengwa Chato ni wa pili kwa ukubwa baada ya ule wa Mkapa!Umewaza ingekuwaje kama Mkapa angeenda kujenga huo uwanja alikozaliwa?
Wilaya gani nyingine nchini ina neema ya kupata uwanja wa kimataifa wa mpira wa miguu kama Chato?
Kuhusu hospitali ya rufaa,nimesema hata kijiografia hospitali haikupaswa kuwa Chato kama lengo ni kuhudumia Kigoma,Rukwa,Kagera na Shinyanga!Walau ingejengwa nyakanazi!Mtu kutoka kigoma itabidi apige KM zaidi ya 600 kwa barabara kufika Chato,huo ni uungwana?Vp mtu kutoka Rukwa?Acheni siasa za rejareja!
Eti utalii wa hospitali,mtu atoke Nairobi au Kampala ambako kuna hospitali kubwa na za kisasa aje kushangaa hospitali Chato?Are you serious?Kabisaa?
Kama ni Airport basi ilipaswa kuwa makao makuu ya Mkoa yaani Geita na si huko Chato!Mtu ni bora akashukia Mwanza na kuja Geita kwani ni karibu kuliko kushukia Chato halafu aitafute Geita ambako kunakuwa mbali zaidi!

Punguzeni mahaba na muwe wakweli kwa nafsi zenu!
 
Angekuwa anafanya hiyo miradi Chato pekee na sehemu nyingine pamesimama hapo ungepata sababu ya msingi kulalamika.

Ukianza na Hospitali za Kanda, Kanda ya ziwa haina Hospitali ya Kanda inayomikikiwa na serikali, Hospitali kujengwa Chato ni sahihi ili mikoa jirani Kama Kagera na kigoma iweze kunufaika na Hospitali hiyo.
Kanda ya kusini inajengwa Hospitali ya Kanda huko mtwara. Kanda ya Nyanda za juu kusini Kuna Hospitali ya Kanda Mbeya. Kanda ya kazikazini Kuna Hospitali ya Bombo Tanga, Kanda ya Kati kuna Hospitali ya Benjamini Mkapa, Kanda ya mashariki ndo usiseme.

Ukija kwenye viwanja vya ndege kila mkoa viwanja vya ndege vinapanuliwa na kuboreshwa zaidi. Mkoa wa Geita haukuwa na kiwanja Cha ndege, ndio hicho kilichojengwa Chato.

Viwanja vya mpira kila mkoa vitajengewa/kuboreshwa viwanja vilivyopo.

Maofisi ya serikali na taasisi zake kila wilaya yanajengwa. Vyuo vya Veta vinajengwa karibu kila wilaya.

Miradi ya barabara ndo usiseme, nitajie wilaya hata moja ambayo barabara hazijengwi.

Kwa hiyo ukiangalia miradi mingi inayofanyika Chato mkoani Geita haina tofauti na miradi inayofanyika mikoa mingine. Chato nako Kuna watu wanahitaji maendeleo Kama yanayofanyika sehemu nyingine.

Ni kwa sababu tu Rais anatokea kule basi wapinzani wasiokuwa na hoja Kama akina Lisu wanaona ni kete za kuwainua na wanapata washabiki wasiongalia Mambo kwa upana wake.
Again why chato na sio muleba au kasulu?

Ishu hpo ni coincidence ya magufuliMagufuliMagufuliMagufuli
Hii inaonyesha kbsa kuna kitu hakipo Sawa ila kwa kuwa watanzania unafiki ishakuwa ni sehemu ya maisha yetu ndyo maana tunaona hii ni Hali ya kawaida.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Angekuwa anafanya hiyo miradi Chato pekee na sehemu nyingine pamesimama hapo ungepata sababu ya msingi kulalamika.

Ukianza na Hospitali za Kanda, Kanda ya ziwa haina Hospitali ya Kanda inayomikikiwa na serikali, Hospitali kujengwa Chato ni sahihi ili mikoa jirani Kama Kagera na kigoma iweze kunufaika na Hospitali hiyo.
Kanda ya kusini inajengwa Hospitali ya Kanda huko mtwara. Kanda ya Nyanda za juu kusini Kuna Hospitali ya Kanda Mbeya. Kanda ya kazikazini Kuna Hospitali ya Bombo Tanga, Kanda ya Kati kuna Hospitali ya Benjamini Mkapa, Kanda ya mashariki ndo usiseme.

Ukija kwenye viwanja vya ndege kila mkoa viwanja vya ndege vinapanuliwa na kuboreshwa zaidi. Mkoa wa Geita haukuwa na kiwanja Cha ndege, ndio hicho kilichojengwa Chato.

Viwanja vya mpira kila mkoa vitajengewa/kuboreshwa viwanja vilivyopo.

Maofisi ya serikali na taasisi zake kila wilaya yanajengwa. Vyuo vya Veta vinajengwa karibu kila wilaya.

Miradi ya barabara ndo usiseme, nitajie wilaya hata moja ambayo barabara hazijengwi.

Kwa hiyo ukiangalia miradi mingi inayofanyika Chato mkoani Geita haina tofauti na miradi inayofanyika mikoa mingine. Chato nako Kuna watu wanahitaji maendeleo Kama yanayofanyika sehemu nyingine.

Ni kwa sababu tu Rais anatokea kule basi wapinzani wasiokuwa na hoja Kama akina Lisu wanaona ni kete za kuwainua na wanapata washabiki wasiongalia Mambo kwa upana wake.
Kwanini atangulize kwake, alafu kwingine kutajengwa?
Hapo ndipo tunaona kunipendelea.
Zamani wazazi hasa wakiume, unatengwa wali kwa nyama, mtoto hakuruhusiwa Kula nyama mpk aruhusiwe na baba.

Huyo baba atashambulia nyama baadae atasema kuleni na nyama! Wababa wengine waligawa vibande kwa Kila mtoto, vitakavyobaki vinamuhusu yeye. JE HAUKUWA UROHO NA ULAFI?

NDIVYO ALIVYO HUYU KWENYE KEKI YA TAIFA.

Angekuwa mcha Mungu angetanguliza mikoa wilaya zingine.
Ndivyo neno la mungu linavyoagiza.
 
- Viwanja vya Ndege na bandari zimejengwa na kuboreshwa sehemu nyingi nchini. Sitaki kukutafunia umeze hebu fatilia. Pia ukumbuke lengo la uwanja wa Chato ni kuinua Sekta kubwa ya uvuvi ili Ndege za kimataifa zitue na kubeba mzigo!

- Hospitali za Rufaa jiongeze boss! Tangu Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani imejenga ngapi na Kipindi cha pili vilevile.

- Ujenzi wa Chuo kikuu hata Mikoa mbalimbali yenye viwanja hivi vipo kwenye Wilaya husika kama Chato. Ukipata kiwanja kikubwa eneo kama Chato litaibeba Kanda ya Ziwa hususan Mkoa mkubwa saana wa GEITA!

MWISHO MSISAHAU HIZI ZOTE NI AJIRA AMBAZO WATANZANIA WATAPATA
Acha kukwepa,hebu jibu moja kwa moja.
Unaifahamu Geita?Kwa uelewa wako unadhani mkoa wa Geita ni wa kubebwa na mji mdogo wa Chato kimapato?Tembelea mkoa wa Geita uuone, Don't be an armchair thinker!
 
Kwanini atangulize kwake, alafu kwingine kutajengwa?
Hapo ndipo tunaona kunipendelea.
Zamani wazazi hasa wakiume, unatengwa wali kwa nyama, mtoto hakuruhusiwa Kula nyama mpk aruhusiwe na baba.

Huyo baba atashambulia nyama baadae atasema kuleni na nyama! Wababa wengine waligawa vibande kwa Kila mtoto, vitakavyobaki vinamuhusu yeye. JE HAUKUWA UROHO NA ULAFI?

NDIVYO ALIVYO HUYU KWENYE KEKI YA TAIFA.

Angekuwa mcha Mungu angetanguliza mikoa wilaya zingine.
Ndivyo neno la mungu linavyoagiza.
Huwa Kuna msemo fulani hivi, kwamba ukileta machungwa nyumbani,halafu unaishi na watoto ambao sio wa kuzaa wewe;Basi anza kuwapa watoto wasio wa kuzaa wewe,ili wawakatie vipande watoto wako wa kuzaa.Msemo huu una maana kubwa sana.Nashangaa wanaojiita wapenzi wasema kweli wanashindwaje Kutumia busara Kama hizi.
 
Nitajie wilaya yenye project hata robo 3 ya hizi!
  • Uwanja wa kimataifa wa ndege
  • Hospitali ya rufaa ya kuhudumia kanda
  • Bandari kubwa na ya kisasa!
  • Majengo ya kisasa ya TRA,Tanesco na Bohari ya dawa MSD!
  • Taa za kuongozea magari!
  • Uwanja wa kimataifa wa mpira wa miguu
  • Chuo kikuu
Hapa achana na miradi kama maji,umeme na vituo vya afya ambayo ni common maeneo yote ikiwemo Chato!

Kule bungeni sasa hivi ni kazi ya kuoneshana status za whatsup tu

Spika wa bunge nae ndio kinara wa pasia simu
 
Bado hujajibu swali,wilaya nyingine zinaweza kuwa na mradi mmoja au miwili kati ya hiyo niliyotaja!Nitajie wilaya yenye miradi kama hiyo kwa pamoja!

Niseme tu,watu wa Rukwa,Kigoma,shinyanga na Kagera hawana hospitali kama hiyo ya Rufaa!So watu wa ukanda huu tutakuwa tunatibiwa Bugando na Chato,hii ni sawa kweli?

Uwanja wa mpira wa pili kwa ukubwa Tanzania unaenda kujengwa Chato,uwanja wa ndege wa kimataifa,tunamdanganya nani?
Hivi mpaka ifanyike miradi kiasi gani ndio mtaona upendeleo wa wazi Chato?
Kanda ya ziwa haina uwanja wa michezowa kisasa kanda ya ziwa. Ajabu kabisa!
 
Back
Top Bottom