Wabunge wengi wamelala usingizi wa pono. Hawasemei miradi iliyotekelezwa maeneo yao

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,194
1,416
Wana JF hamjambo?

Nimeona watu wengi wanaojiita great thinkers wakizungumzia miradi inayofanyika Chato!

Hii inasikitisha sana kwa macho yootee kuangalia sehemu moja! Wabunge wengi wanafahamu nini kimetekelezwa na kinaenda kutekelezwa kwenye maeneo yao! Ila wapo kimyaaaa! Kinachofanyika Chato ni kwasababu kimepata wasemaji kwenye mitandao ya Jamii na media nyingine.

Natamani JF ingeweka utaratibu tukaona mambo makubwa yanayofanyika nchi nzima. Wekeni taarifa ya kila Wilaya, inakaa wiki nzima au siku 3 unaweka Wilaya nyingine

Mambo yaliyofanyika Chato na miradi iliyopelekwa ni michache kuliko Wilaya mbalimbali nchini! Tuache wivu na macho ya husuda!! Mkapa aliamua kujenga Lushoto sasa shida iko wapi? Kuna wengine wamenunua majumba ughaibuni nk Hata Mzee Kikwete amelisemea sana hili na yeye yalimkuta ikawa nongwaaa!

JF ni mahali Sahihi sasa tupate taarifa za Maendeleo Wilaya kwa Wilaya. Msisahau kuonesha na idadi ya watu kwenye eneo husika ili wale wa Kaskazini waone walivyopendelewa!

Sasa tuache maneno tuweke data! Mwisho mfahamu Chato wanaishi Watanzania wenzetu hivyo wakipelekewa Maendeleo ni Sawa! Acheni upotolo! "Chicken vision"! Eagle vision ndio mpango mzima.
 
Nitajie wilaya yenye project hata robo 3 ya hizi!
  • Uwanja wa kimataifa wa ndege
  • Hospitali ya rufaa ya kuhudumia kanda
  • Bandari kubwa na ya kisasa!
  • Majengo ya kisasa ya TRA,Tanesco na Bohari ya dawa MSD!
  • Taa za kuongozea magari!
  • Uwanja wa kimataifa wa mpira wa miguu
  • Chuo kikuu
Hapa achana na miradi kama maji,umeme na vituo vya afya ambayo ni common maeneo yote ikiwemo Chato!
 
Nitajie wilaya yenye project hata robo 3 ya hizi!
-Uwanja wa kimataifa wa ndege...
- Viwanja vya Ndege na bandari zimejengwa na kuboreshwa sehemu nyingi nchini. Sitaki kukutafunia umeze hebu fatilia. Pia ukumbuke lengo la uwanja wa Chato ni kuinua Sekta kubwa ya uvuvi ili Ndege za kimataifa zitue na kubeba mzigo!

- Hospitali za Rufaa jiongeze boss! Tangu Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani imejenga ngapi na Kipindi cha pili vilevile.

- Ujenzi wa Chuo kikuu hata Mikoa mbalimbali yenye viwanja hivi vipo kwenye Wilaya husika kama Chato. Ukipata kiwanja kikubwa eneo kama Chato litaibeba Kanda ya Ziwa hususan Mkoa mkubwa saana wa GEITA!

MWISHO MSISAHAU HIZI ZOTE NI AJIRA AMBAZO WATANZANIA WATAPATA
 
Mzee mmoja wa "inner circle of evil" ya CCM anasema kwa kinachoendelea,Kaskazini inabidi tujipange kitimu kutoa namba moja,wakati huo huo kanda ya kati nao wanapanga mikakati,nyanda za juu nao hawapo nyuma.

Je, hapo kuna taifa moja kama taifa kweli kwa mikakati hiyo!?

Chanzo ni nini!?

Hata mjukuu wangu wa grade 4 anashangaa kila kitu Chato,anauliza,Dodoma,DSM na Chato ni makao makuu ya nchi?
 
- Viwanja vya Ndege na bandari zimejengwa na kuboreshwa sehemu nyingi nchini. Sitaki kukutafunia umeze hebu fatilia. Pia ukumbuke lengo la uwanja wa Chato ni kuinua Sekta kubwa ya uvuvi ili Ndege za kimataifa zitue na kubeba mzigo!
Bado hujajibu swali,wilaya nyingine zinaweza kuwa na mradi mmoja au miwili kati ya hiyo niliyotaja!Nitajie wilaya yenye miradi kama hiyo kwa pamoja!

Niseme tu,watu wa Rukwa,Kigoma,shinyanga na Kagera hawana hospitali kama hiyo ya Rufaa!So watu wa ukanda huu tutakuwa tunatibiwa Bugando na Chato,hii ni sawa kweli?

Uwanja wa mpira wa pili kwa ukubwa Tanzania unaenda kujengwa Chato,uwanja wa ndege wa kimataifa,tunamdanganya nani?
Hivi mpaka ifanyike miradi kiasi gani ndio mtaona upendeleo wa wazi Chato?
 
Mzee mmoja wa "inner circle of evil" ya CCM anasema kwa kinachoendelea,Kaskazini inabidi tujipange kitimu kutoa namba moja,wakati huo huo kanda ya kati nao wanapanga mikakati,nyanda za juu nao hawapo nyuma.
Miradi ya Dodoma, Dar, Arusha huioni?
 
Viwanja vya Ndege na bandari zimejengwa na kuboreshwa sehemu nyingi nchini
Weka data usilete maneno ya jumlajumla.

Andika hapa wote tusome.

Mfano kijiji cha zinga Bagamoyo kuna uwanja wa ndege kama chato unajengwa au umeshakamilika nk.

Pia ukumbuke lengo la uwanja wa Chato ni kuinua Sekta kubwa ya uvuvi ili Ndege za kimataifa zitue na kubeba mzigo!
Kwa maana hiyo kila penye shughuli za uvuvi magufuli atajenga uwanja wa ndege kuinua uvuvi?

Kwanini ujenzi uanzie chato kijijini alipozaliwa magufuli na siyo nyamisati ambapo pia kuna shughuli za uvuvi

Huu tukiita upendeleo tutakua tunakosea?

- Hospitali za Rufaa jiongeze boss! Tangu Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani imejenga ngapi na Kipindi cha pili vilevile
Kanda ya ziwa tayari kuna hospitali ya rufaa ya bugando.

Hakukua na ulazima wa kujenga hospitali ya rufaa chato tena magufuli anasisitiza ijengwe haraka haraka ikamilike wakati kuna kanda kama ya maghribi hakuna hospitali ya rufaa.

Ujenzi wa Chuo kikuu hata Mikoa mbalimbali yenye viwanja hivi vipo kwenye Wilaya husika kama Chato.
Hapo lumumba hamfundishwi communication skills?

Ulichoandika hakieleweki.
 
Hakuna mbunge ambaye jimbo lake limepata miradi mingi ya kama jimbo la Chato.

Na mbunge wa Chato anaona aibu kutaja miradi aliyopewa maana ni kufuru kulinganisha na walichopata wenzake.
 
Wakati WILAYA nyingine wanachangishwa kwa nguvu kwa ajili ya madarasa CHATO mabilioni yanamiminka kwa miradi isiyona tija
 
- Viwanja vya Ndege na bandari zimejengwa na kuboreshwa sehemu nyingi nchini. Sitaki kukutafunia umeze hebu fatilia. Pia ukumbuke lengo la uwanja wa Chato ni kuinua Sekta kubwa ya uvuvi ili Ndege za kimataifa zitue na kubeba mzigo!

- Hospitali za Rufaa jiongeze boss! Tangu Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani imejenga ngapi na Kipindi cha pili vilevile.

- Ujenzi wa Chuo kikuu hata Mikoa mbalimbali yenye viwanja hivi vipo kwenye Wilaya husika kama Chato. Ukipata kiwanja kikubwa eneo kama Chato litaibeba Kanda ya Ziwa hususan Mkoa mkubwa saana wa GEITA!

MWISHO MSISAHAU HIZI ZOTE NI AJIRA AMBAZO WATANZANIA WATAPATA

Bora umejitokeza ww, wasifiaji wanasema serikali ya awamu ya tano imejenga hospitali za rufaa 67 nchi nzima, na hospitali na vituo vya afya 370+. Nimekuwa nikiulizia watuwekee jedwali likionyesha hospitali ilipo, mkoa wilaya na kijiji/tarafa ilipo. Hakuna yoyote anayefanya hivyo kiasi kwamba tunaona ni uongo. Ila kwakuwa na ww ni msifiaji, hebu weka hiyo list ili tujiridhishe. Ukiweza weka na bei ya hospitali au kituo cha afya husika ili tukate mzizi wa fitina.
 
Kuna mbunge mmoja wa jimbo la Ukonga Jerry Slaa aliyeingia kwa kazi kwa kutoa matumaini kwa wana Ukonga,wengine tulipata wakati mgumu kuamua kuchagua upinzani au huyu Slaa,Du!! najutia kura yangu ilivyopotea, Kama alivyokuwaa mtangulizi wake Mwita Waitara naona na yeye kaingia mitini huku akiacha barabara za mitaani zikigeuka mitaro..... Hovyo kabisa. 🤔 :oops:😡
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom