Wabunge wapimwe akili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wapimwe akili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Faddy, Nov 21, 2011.

 1. F

  Faddy Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nilichokishuhudia katika mchakato wa kuchangia mswada wa katiba mpya .kunahaja ya kufanya yafuatayo:

  1. Wabunge kupimwa akili kila siku kabla ya kuingia bungeni
  2. Kuwa wanaandikiwa na wananchi kile wanachotakiwa kukichangia
  3. Kuwa na utaratibu wa kuwauliza na kuwawajibisha kutokana na jinsi walivyo tekeleza yale tuliyowatuma siyo kusubiria miaka mitano
  4. Mishahara yao iwe inalipwa kuendana na ufanisi wao na wawe wanapokelea majimboni kwao kwani wengine huwa hawaendi huko.

  Kwani kwa kilichotokea inaonyesha hawa jamaa tunaowaita wawakilishi wetu niwawakilishi wa fikira zao wenyewe, vyama vyao na interest zao na za rafiki zao. Haiwezekani wapewe nafasi ya kuchangia mswada wa kitu muhimu kama katiba wao wanaishia kuongea kuhusu chadema halafu mwishoni wanaunga mkono hoja. Au chadema ndo ulikuwa muswada wenyewe?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Unategemea nini toka kwa wabunge wanaohonga kuingia bungeni?

  Unataka usikie nini toka kwa wabunge wa viti maalum?
   
 3. K

  KIBONGOMKUTI JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 1,415
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Faddy ki-ukweli naungana na hoja yako kuhusu hawa wabunge wetu utaratibu wa hii domo-krasia ya wao kutusemea HAIKUBALIKI.

  Mtazamo wangu Wabunge wangekuwa wanapimwa kwa ufanisi wao kila robo mwaka, endapo Mbunge hawezi kutekeleza majukumu na ahadi zake anapigwa chini kisha anachukua nafasi alie kuwa mshindi wa pili.

  Pia iwe ni lazima kufika kazini kwa maana ya kuweka sahihi na kutoa huduma kwa wananchi katika ofisi zao za majimbo.

  Cha kushangaza na kusikitisha asilimia kubwa ya wabunge wetu wanaishi na kuponda raha jijini Dar, huku shamba wanakuja kwa ajili ya uchaguzi.

  Elimu ndogo na duni ya watu wetu pia na ulimbukeni wa ki-siasa tunaacha kuchagua Mbunge tunachagua chama. Hii inasikitisha sana, daima nimekuwa na mtazamo kuwa Mbunge anapomaliza vikao mjengoni ni LAZIMA arudi jimboni atoe mrejesho wa shughuli aliyotumwa na wapiga kura wake.
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  wengine hawaitaji kupimwa maana ni hata kuku anaweza kumjua ni chizi kabisa like mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde.
   
 5. c

  cr9 Senior Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Faddy mi nakubaliana na wewe 100%. hawa jamaa hawana akili haiwezekani utumie 90% ya muda wako kuelezea chama kingine na 10% kuzungumzia hoja iliyo mezani.

  haya ni madhara ya vikao vya siri vyakuawaambia wabunge wote waseme kitu kimoja kupinga upinzani lakini wajue wananchi wanaangalia na hukumu yao ipo karibu sana
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wazo lako ni zuri na ninaliunga mkono. Kwa vili nina hakika hakuna mbunge aliyechaguliwa na kulipwa posho na mishahara ili akimbie mijadala na kuwanyima nafasi wawakilishi, basi wabunge wa chama chenye tabia ya kususa susa wawe wa kwanza kwenye foleni ya kupimwa akili ili tujiridhishe kama kweli tulichagua watu wanaoweza kusema au ni mabubu? Hili lianze na kiongozi wa upinzani bungeni na mnadhimu wake.
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na ghadhabu za wananchi zitaanzia na wale mataahira wanaokimbia kimbia mijadala.
   
 8. O

  Obesity Senior Member

  #8
  Jan 29, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwingira ashauri wagombea wapimwe akili

  KIONGOZI wa Kanisa la Efatha nchini, Mtume Josephat Mwingira ametaka kila anayegombea uongozi wa umma sharti apimwe akili.
  Hayo aliyaeleza jana asubuhi wakati akihubiri katika ibada ya kwanza kwenye makao makuu ya Kanisa hilo, jijini Dar es Salaam.

  "Hali ni mbaya, malalamiko ya wananchi dhidi ya wizi wa rasilimali za Taifa kwenda nje yamekuwa mengi,'' alisema.
  Alisema tabia ya mfumo wa uchumi nchini ya kuthamini wawekezaji kutoka nje ya nchi kuliko wa ndani siyo nzuri na kwamba ni moja ya vyanzo vya kudorora kwa uchumi wa taifa.

  "Mimi nimewahi kuchimba madini ya Tanzanite, ikanipa kipato kizuri tu lakini nilinyang'anywa wakapewa wawekezaji wakubwa, siasa zisizoona tatizo hata kudhulumu wananchi wake ni siasa chafu," alieleza Mtume na Nabii Mwingira.

  Akifafanua juu ya hali ilivyo nchini, alitoa mfano wa familia yenye kumiliki ardhi kubwa lakini isiyoendelezwa akisema, "wanakuja watu kutoka nje kuomba wapatiwe ardhi hiyo ili waiendeleze kwa kilimo na ufugaji na baba wa familia husika ambaye anawaruhusu kwa kusema, ‘tumieni tu hamna taabu'.

  Kiongozi huyo mwanzilishi wa Kanisa la Efatha alieleza kuwa wageni hao wanapohoji kuhusu malipo, wanaelezwa na baba wa familia husika kuwa hakuna tatizo waendelee na shughuli zao kwanza, baada ya miaka mitano ndipo wataamua walipe kitu gani.

  Alisema wakati wakulima hao wakivuna mazao na kuuza na mengine kuhamishia kwenye nchi zao, wanafamilia inayomiliki mashamba hayo wanakabiliwa na uhaba wa chakula kiasi cha wengine kufa kwa kukosa chakula, hali inayosababisha baba wa familia husika kuchota fedha za familia, kwenda kwenye nchi za wale wanaolima mashamba yake kuomba misaada.

  "Hii si sawa, kuna umuhimu kila mtu atakayetaka kuongoza umma wa Watanzania hata kama ni ngazi ya mbunge, akapimwe akili yake kwanza ili kujiridhisha na uwezo wao wa utendaji kiakili,"

  chanzo:gazeti la mwananchi
   
 9. m

  mugayasida JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2013
  Joined: Nov 3, 2012
  Messages: 482
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa ndugu yangu Mwingira umeongea point ila sisi tunajua CCM hawana akili kwahiyo kwenda kuwapima ni kupoteza za walipa kodi kama vile wao wanavyozifisidi...Waliokosa hoja na uliowashika pabaya watakuja na nyimbo za kukukashifu mara oooh unachapa wake za watu mara oooh umetapeli ardhi na halafu kuna kijidini fulani cha ibilisi kinauadui na ukristo kina vihoja mufilisi kweli tusubiri sasa hivi wataingia
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2013
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  CCM wakapimwe akili
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2013
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huyu NABII aka MTUME Mwingira hajui kwamba katiba yetu bado ina dentetion act na deportation.
   
 12. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2013
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,848
  Likes Received: 4,223
  Trophy Points: 280
  'Mwenye masikio na asikie'
   
 13. O

  Obesity Senior Member

  #13
  Jan 29, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tusichanganye dini na siasa...kamwe havitachanganyana
   
 14. j

  joely JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2013
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  nafikiri huelewi misingi ya kutenganisha dini na siasa, tumia muda mwingi kusoma ili uelewe.
   
Loading...