Wabunge wanne wajiunga na ACT - Wazalendo

Wabunge wanne wajiunga na ACT - Wazalendo

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,175
Reaction score
11,573
Kwa mujibu wa Naibu Katibu mkuu wa ACT- Wazalendo akiongea na Clouds Fm Amesema wabunge hao hatawataja kwa majina mpaka watakapopokelewa katika majimbo yao.

Pia Naibu Katibu mkuu huyo amesema Kuhusu Moses Machali aliyekuwa mbunge NCCR mageuzi tayari amejiunga rasmi na chama hicho.

Wakati Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikivuna maelfu ya wanachama wa chama tawala CCM, uku hali siyo shwari ndani ya NCCR - MAGEUZI chama ambacho kinaunda muungano wa UKAWA.

Ni jana tu aliyekuwa mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali na Naibu katibu mkuu bara pamoja na aliyekuwa M/kiti wa Vijana Taifa Deo Meck walijiunga na ACT.

Leo imesemekana kuwa vigogo wengine wa chama hicho watakiama na kutimkia ACT vigogo hao ni mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila, Mkosamali Mbunge wa Muhambwe na Nicolas Clinton M/kiti wa vijana jimbo la Nyamagana Mwanza.
 
Hawa ACT wawaache tu, sisi tuko busy kugombea nafasi ya urais tu, mbowe kishatuzunguka kavuta mpunga kwa lowassa amuuzie chama, kweli siasa za kibongo hazina maana kabisa

Ha ha ha ha niliwahi kuandika humu siku moja kwamba mchaga yeyote huwa hafanyi biashara kichaa! Mbowe ni mfanyabiashara ya siasa, wacha avute mkwanja aendelee na maisha na wakati huo huo wale misukule wanaojiita wafia chama mtabaki mmevimba macho kwa kushangilia mikutano ya chadema kwenye mavumbi kibao na wengine kuishia kuvunjwa vichwa na miguu kwenye maandamano haramu!
 
Hawa ACT wawaache tu, sisi tuko busy kugombea nafasi ya urais tu, mbowe kishatuzunguka kavuta mpunga kwa lowassa amuuzie chama, kweli siasa za kibongo hazina maana kabisa

Hii imekaaje, ACT wakiwachukua wabunge kutoka vyama vya upinzani mnashangilia, ati ACT waache tu, lakini UKAWA wakitaka kumchukua Lowassa inakuwa Mbowe keshatuzunguka na kuchukua mpunga. Ama kweli kutawaliwa na akili ndogo ni shida. Lowassa ana watu wanaomuunga mkono si chini ya milioni mbili na wabunge wa CCM zaidi ya mia na hamsini. Unamkataaje mtu mwenye mtaji wa wapiga kura zaidi ya milioni mbili na wabunge zaidi ya mia na hamsini. Ukimkataa mtu wa jinsi hiyo utakuwa kichaa.
 
Lowassa fisadi mbowe fisadi sishangai Hapo, mchukueni tu mbona mnapiga ramli wiki nzima sasa?
 
Walisema 60, siyo 50. Pia wakasema Lowassa anajiunga nao. Namsikitikia Moses Machali kama amejiunga na wasaliti ACT, amechagua garasa. Bora Shibuda kaenda tawi lingine la CCM, yaani TADEA, kawaepuka ACT na Ayatollaak wao Zitto.

Hata wewe utakuja tu,sasa utakubali kubaki pekee yako kwenye hiyo Saccos coz wengine wameshaanza xafari kutoka misri kwenda nchi ya ahadi
 
Back
Top Bottom