Wabunge wanashuhudia utiaji saini ujenzi daraja la Busisi Mwanza

Hongera sana JPM...................Wewe ni mzalendo..............piga kazi baba
 
Wapinga maendeleo na serikali kwa ujumla wapo uvunguni mwa kitanda wameziba masikio

Mkuu hiyo computer image ndio inayokuchanganya nini? Hivyo vyote vilikuwepo huko Afrika Kusini lakini Mandela na weusi wenzake hawakuvisujudia.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Nashauri hilo daraja liwekewe sehemu ambapo Meli kubwa zinaweza kupita....! Mfano, wanaweza kuweka sehemu ambapo linafunguka kupisha meli kubwa kupita na kisha kujifunga/kufungwa kwa matumizi ya upitaji magari...kama kulirefusha juu sana itakuwa tatizo.

Nawasilisha hoja.
 
Myonge myongeni tu lakini haki yake mpe! Mbali na kwamba bado hali ya maisha huku mtaani ni NGUMU lakini Serikali ya hawamu hii ya tano, kwakweli kazi wanafanya. Tuweke masuala ya siasa pembeni, Mh Rais Magufuli na wasaidizi wake binafsi nawapongeza kwa baadhi ya masula ya kimaendeleo. Tutakosoa kwa nia njema na kumtia moyo, tutafanya kazi kwa ajili ya taifa letu pamoja pia kushauri panapohitajika na tutapongeza pia kwa mazuri. Kwa hill napongeza pia.
 
Mkuu hiyo computer image ndio inayokuchanganya nini? Hivyo vyote vilikuwepo huko Afrika Kusini lakini Mandela na weusi wenzake hawakuvisujudia.
Hiv wewe chadema wanakupaga Nini mpaka uwe unapinga kila Jambo zuri linalofanywa na serikali?
 
Hiv wewe chadema wanakupaga Nini mpaka uwe unapinga kila Jambo zuri linalofanywa na serikali?

Mkuu unaweza kunionyesha nimepinga wapi hapo hayo maendeleo kwenye hiyo post yangu au wapi nimeponda kila kitu cha serikali? Inaonekana wewe ni wale wafuata mkumbo hivyo hujisimamii kwa akili yako ndio maana huna uwezo wa kupima hoja iliyotofauti na kusikia sifa tu.
 
Hatimaye historia imeandikwa nchini Tanzania kwa kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza lenye urefu wa kilometa 3.2, ambao utagharimu jumla ya fedha za kitanzania Bilioni 592.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja hilo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe, amesema mradi huo utatekelezwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania bila kutegemea fedha za wafadhili.

Waziri Kamwelwe alisema mradi wa Kigongo Busisi kama ilivyo miradi mingine ya kimkakati ulipigwa vita sana na baadhi ya watanzania na hata wahisani, amesema hata baadhi ya wanasiasa waliupinga wakidai ni mradi mkubwa sana kwa taifa na hauna tija kwa wakazi wa maeneo hayo na nchi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom