Wabunge wanapoenda Bungeni leo wakiwa hawajui wanachoenda kufanya huko tuwaeleweje?

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
3,142
5,634
Katika hali isiyo ya kawaida jana wakati naangalia taarifa ya habari ITV, Mh. Mnyaa alikuwa akilalamika kuwa wabunge wanaelekea katika kikao cha bunge kinachoanza leo wakiwa hawajapewa muhtasari wa nini wanachoenda kufanya.

Katika hali isiyo ya kawaida tu unaweza kukutana na mtu kabeba mabegi anasafari na kumuuliza unaelekea wapi na kukujibu sielewi. Na huku ni kupoteza uelekeo.

Wabunge kuelekea bungeni bila kupewa muhtasari wa nini wanachoenda kufanya ni kuonyesha kabisa kuwa wanaelekea huko ili mradi tu kukamilisha ratiba na hii inaonyesha ni namna gani huu mhimili muhimu wa Serikali ulivyokosa muelekeo.
 
inasikitisha sana kufikia katika hali kama hii, shame on Mama Makinda

Hivi kuna lolote zuri la kuonekana au kusikika ambalo bunge tunalolijua limewahi kulifanya kwa ajili ya waliowachagua?

Nasikia ya kuwa Tanzania sio nchi masikini duniani bali ni nchi fukara.

Tembelea shule, mahospitali, na kwengineko ujionee shida wajameniii.

Kumbuka madini ya Mwadui toka Babu wa mababu alisikia yalivyo kuwa yahasifika. Leo tembelea Shinyanga utajionea ufukara wa kutisha.

Ila nakubali ya kuwa Tanzania ni tajiri wa maneno na uwoga. Na bunge wana maneno sana na waoga wa kutimiza matakwa ya wengi walio watuma huko Dodoma.

Hivi ngoja niulize nje ya mada. Kwanini wasihamie kabisa Dodoma? au Makao Makuu ndio bado yapo Dar?
 
Back
Top Bottom