Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Kizitto Noya, Dodoma
KAMATI ya Bunge ya Miundombinu imeitaka serikali kutoa tamko kuhusu tuhuma zinazomkabili mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Ephraem Mrema kwamba mkataba wake wa kazi umekwisha.
Mbunge wa viti maalum (CCM), Joyce Masunga, akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo Mohammed Missanga, alisema tuhuma hizo zinaathiri ufanisi na utendaji wa Tanroads.
Masunga alisema hayo alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu katika makadirio ya matumizi ya Wizara ya Miundombinu.
Kamati yangu inasikitishwa sana na malumbano yanayoendelea kwa muda mrefu sasa kuhusu mtendaji mkuu wa Tanroads kwamba mkataba wake wa ajira umekwisha, alisema Masunga.
Lakini wakati malumbano hayo yakiendelea, serikali imekaa kimya bila kutoa ufafanuzi na ukweli wa madai hayo yanayoandikwa magazetini siku hadi siku. Kamati ingependa serikali ieleze ukweli wa madai hayo kwani yanaathiri ufanisi na utendaji katika wakala huo.
Alisema katika kulipatia ufumbuzi suala hilo, kamati iliwakutanisha watendaji wakuu wa wizara, bodi ya Tanroads na Mrema kubaini kama kulikuwa na tatizo, lakini bado mijadala na malumbamo hayo haijakwisha.
Katika mikutano hiyo, Masunga alisema, kamati ilibaini kuwapo kwa makundi yaliyokuwa yakichagizwa na wafanyakazi waliokuwa Tanroads na ambao wamesimamishwa kazi au kumaliza muda wao wa utumishi na wengine hawakuridhika na kuenguliwa kwao katika nafasi zao za uongozi.
Kamati yangu kwa kutumia busara na ili kuepusha malumbano yasiyo na tija katika kipindi kinachopaswa kukamilisha miradi, iliishauri wizara kukaa pamoja na bodi ya Tanroads na watendaji wake wakuu kujadili masuala yanayowahusu, hasa yale ya mchakato wa kujaza nafasi za watendaji, alisema.
Kamati ilishauri kuwa ili miradi isisimame wakati mchakato huo unaendelea, mtendaji mkuu awateue wale wote wanaoshilikia nafasi hizo wakaimu hadi watakapopatikana wa kujaza nafasi hizo kulingana na muundo mpya wa wakala ambao ulishakamilika na kuridhiwa na idara kuu ya utumishi.
Katika hatua nyingine kamati hiyo ya miundombinu imeelezea kuridhishwa kwake na utendaji wa mkurugenzi huyo kwa kila ilichoeleza kuwa amefanya kazi nzuri tangu aingie madarakani Juni mwaka 2007.
Wakati anaingia madarakani wakala ulikuwa na miradi 10 tu lakini, sasa kuna mikataba zaidi ya 40. Mabadiliko yalianza kuonekana kwa kasi ikilinganishwa na mtendaji aliyepita, alisema.
Mrema alipoanza kazi kulikuwa na mikataba 18 iliyokamilika, miradi 4 alianza nayo yeye na kuikamilisha ambayo ni Kigoma- Kidahwe, Usagara- Sengerema na Masasi- Mangaka, alisema.
Masunga alitaja miradi mingine iliyokamilika katika kipindi cha uongozi wa Mrema kuwa ni barabara 18 , miradi 10 aliyoirithi kutoka kwa mtangulizi wake na miradi minne kutoka wizarani
Leo hii ni miradi zaidi ya miradi 54 ya barabara za kitaifa ambayo ameisimamia pamoja na miradi ya madaraja na vivuko kama vile vya Busisi, Kigamboni, Pangani, Kilombero, Utegi na vingine.
Awali Spika wa Bunge Samuel Sitta alimpa pole mtendaji mkuu huyo wa Tanroads na kumtia moyo kwamba aendelee kuvumilia katika kipindi hicho kigumu cha tuhuma katika utendaji wake wa kazi.
Wabunge wamkalia kooni bosi Tanroads
HAWA WANA WAZIMU? wanahoji na hapo hapo kupongeza!!!!! Huu uchaguzi utatufanya watu tubebeshwe makapi watu wanatafuta fedha za uchaguzi.... Jamani Mwenyekiti Mohamed Misanga, ana gari jipya kabisa!!!!!