G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,592
- 36,008
Hawa watu sijui tuwaelimisheje. Wanakutana eti na kipengele cha kuondoa road license kwenye bajeti wanapiga makofi na kushangilia kijinga kabisa.
Wakikutana na kipengele kigumu kwao wanakaa kimya kwa muda ila kikija kizuri tu kwa sura tena hata ambacho hawakielewi wanaanza kushangiliashangilia hovyo hovyo tu.
Pale badala wangetumia muda wao kusikiliza kwa makini tena umakini mkubwa, wachambue na kuandika mambo muhimu wanabaki kupiga mayowe tu!
Baada ya kutoka weupe jana kwa kushangiliashangilia kitakachofuata ni kuchangia vitu visivyo na maana na bajeti inapita na mapungufu yake mengi tunarudi tena mwakani na ujinga ule ule wa kila siku.
Spika naye anaingia kwenye mkumbo wa ushangiliaji huku akiwa na lengo la "kuwaondoa wabunge wake wa CCM kwenye umakini kama ambavyo wanafanya siku zote" Huu ni utapeli wa kisiasa.
Inakera sana kuwaona hawa watu wakifanya mambo ya kitoto kabisa.Waliondolewa live kwenye tv kuonyeshwa vikao vyao wakashangilia na kuunga mkono hoja. Cha ajabu leo wakirejeshewa vikao vyao live watashangilia tena na kuunga mkono hoja. Yan wapowapo tu! Nachukia sana kuona bunge limekosa msimamo kuliko hata wamachinga wa kariakoo. Bunge hili ni la hovyo sana na linaenda kihovyohovyo tu. Najutia kodi yangu kulipa mshahara mkubwa majitu mizigo haibebeki inakera ipoipo kama sijui nini..Hawaeleweki wamesimamia upande gani wao ni kupelekwapelekwa tu hawajui kesho wataibukia wapi!