Wabunge wakomaa: Ngeleja, Jairo watakiwa kuondoka; Pinda ataka mjadala uahirishwe kwa siku 21

Status
Not open for further replies.
Kwa hio hadi wiki tatu tena??? lazima waje na maamuzi ya maana, hebu ngoja nikawahi daladala za Michweni mie niende zangi kibanda maiti kwangu nikalale na giza langu, ningepata msokoto wa bangi ningefurahi sana ila naskia kuna wachunga kondoo wanauza sijui ntawapataje..ooh ok, kumbe Kiranja mkuu anawafahamu...ok very nice nahisi alikua mteja wao......hahahahaaa pombe bana haya mie nimelewa kidogo naondoka zangu, vunda moja la ziada litaniumbua.
 
Sawa bwana katika mfumo wetu huu wa kipuuzi, Waziri mkuu si picha tu, kwani ana mamlaka gani.Na wiki tatu za nini,hao si wa kufukuza tu.Bahati yao sio China,ingekuwa sio kutimuliwa tu,na risasi juu!
Wakuu,

Taarifa niliyoipata toka kwa source wetu ndani ya kikao cha CCM huko Dodoma zinashtua kidogo.

Wabunge wa CCM wamepandisha mori wakitaka Jairo (Katibu Mkuu wa Wizara) atimuliwe na wakaendelea kutishia kuwa hata Ngeleja naye anatakiwa kuachia ngazi.

Wabunge wa CCM wamemtaka Jairo ajiuzulu kutokana na kashfa ambayo imeletwa na Shelukindo juu ya Barua aliyoandika kuzitaka taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zitoe 50mil kila moja ili kupata pesa ya ku-lobby ili bajeti ipite.

Wameitaka serikali kupunguza 20% ya bajeti za 'Other Charges' na pesa zote za kujenga majengo ya Wizara ili ziende kwenye UMEME ama vinginevyo bajeti haipiti na Ngeleja atatakiwa kujiuzulu mara moja.

UPDATES:

Waziri Mkuu Mizengo Pinda kaomba mjadala uahirishwe mpaka baada ya wiki tatu ili waweze kujipanga upya. Kaonyesha kusikitishwa na kitendo cha Jairo na kasema ingekuwa ni kwa hiari yake (bila kumsubiri rais) angechukua maamuzi haraka sana
 
Amegeuza TANESCO kuwa Shirika la Mgawo wa Umeme Tanzania halafu anaongoza wizara inayotoa rushwa.

Kwani ni lini kawa waziri wa nishati na madini......Je kabla ya hapo hakukuwa na matatizo ya mgao wa umeme?....

Tatizo sio Ngeleja,tatizo ni mfumo.......Bado tuna mipango ya mwaka 47 ya ufuaji/uzalishaji wa umeme....Ngeleja amelikuta tatizo hili na ataliacha lidumu kwa miaka mingi tu endapo hakutakuwa na mipango madhubuti ya uzalishaji wa umeme(vyanzo vya ufuaji umeme)...
 
Jinsi alivyotangaza Pinda, huyo ndio kishafukuzwa. Kikwete ni kuidhinisha tu.
 
Jamani namba kuhoji nini mamla ka ya waziri mkuu kama anashindwa kumuwajibisha katibu wa wizara?kazi yake ni kuisemea serikali tu?je lowasa alipata wapi mamlaka ya kuwajibisha watendaji wa serikali?sakata la kuanguka ghorofa lowasa alimfukuza kazi engineer mkuu wa wilaya.sasa pinda anashindwa nini?
 
Wakati nchi iko kwenye matatizo rais anaenda south africa kula bata hatuna sina president.
 
Duh hii ni kali huyu Jairo hana chake tena kimewaka tayari!me nadhali suala ni namna kujua tatizo litakwisha vp na si malumbano!
 
Kibonde katoa taarifa hiyo.tena chanzo chake ni hii post ya JF...Mhm kumbe anasoma vya humu ndani
 
Hureeeeeeeeeee, Ola la laaaaaaaaaaaaaaaaaaa

pesa ipo BOT, Fumueni foreign reserve ibakie ya miezi3.
 
Hizo hela wamegawana kamati ya kina February,
may be mwenyekiti alitoswa mgao
 
Kawa waziri mkuu hana mamlaka makubwa ya kuteua na kumwajibisha mtu,je anamamlaka gani makubwa zaidi ya kuwa analidanganya bunge na kulialia tu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom