pappilon
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 3,192
- 3,556
Waheshimiwa wapenda nchi tuwe wakweli. Wakati mwingine nakubaliana na watu wanaposema kwamba pamoja na sifa zote njema za mwalimu mkuu, the great Julius Kambarage Nyerere, mwenye sifa njema nyingi na utu usio mashaka kwetu sote kama mwanadamu (MUNGU amrehemu), pia yeye hakuwa Malaika kwamba kila alichosema kilikuwa sahihi , japo moyo wake ulikuwa kwa ajili ya Tanzania na watanzania zaidi.
Pili, yeye mwenyewe katika nyakati tofauti alitamka wazi kwamba hakuwa malaika na pia alikiri kwamba alifanya makosa mengi. Mwalimu hakuwa na uwezo wa kuona ndani ya yaliyojificha ndani ya miyoyo ya watu. Hilo ni la MWENYEZI pekee. Kwa mfano:
1. Mwaka 1985 alimpigania Rais mh. Ali Hassan Mwinyi sana kama mtu mpole, mwenzetu nk nk. Sawa. Lakini, na kwa uchacke mwisho wa siku, legacy yake (Mwinyi) huwezi kuitenganisha na ubaguzi wa kidini, kuuza ardhi ya Loliondo kwa waarabu, kujaribu kubadilisha katiba apate term ya tatu kama Nkurunzinza, kuharibu uchumi kiwango kikubwa kabisa, kuvunjwa kwa azimio la Arusha na mwanzo wa kupulizwa kipenga kwa viongozi kuwa mafisadi, wezi, wafanya biashara, yaani ruksa kuu.. Kwa uchache . kiasikwamba ilimbidi kuandika kitabu cha Hatima ya Tanzania na kuwafukuza kina Kolimba na Malecela John. kama mwl huyo huyo asingekuwepo, basi nchi hii ilishasambaratika kipindi cha Mwinyi.
2. Mwaka 1995 ambao wengi tunaukumbuka zaidi, mwalimu alimpigania Mh. Rais Benjamin W Mkapa kama mtu safi mr clean. Hii ni baada ya kusema asingeweza kumpigania mgombea wa kusafisha kwanza ili ndio aanze kimwombea kura. Hizi ndizo kauli mnazozitaja humu. Sawa. Lakini majuzi mkapa akiwa london, akizungumzia awamu ya tano alinukuliwa akisema, ccm imtafute mgombea anayekubalika kwa wanachama wengi ambae yupo anajulikana kwa historia ya maamuzi yake magumu lakini ccm wakiendele kunangania kashfa mfu za huyo mgombea, watamwacha wataishia kupata anayeitwa clean aunde serikali legelege na chama legelege ambacho mwisho wa siku hataweza kuongoza nchi na serikali yake itaanguka. Lakini pia sote tunajua pamoja na u clean wa mkapa mwalimu aliotuelezea, legacy ya mkapa inahusishwa na nini kuuzwa kwa mashirika ya umma, kuuzwa na hatimaye kuuwawa kwa viwanda vyote vya uma vikubwa karibu 20, yeye mwenyewe na wenziwe kujiuzia mgodi wa serikali kiwira kwa bei poa, kuvunjwa na kuuzwa kwa benki zetu kubwa za nbc na nmb katika mazingira tata kabisa (asante bunge la tazania kuwazuia hawa genge likijumuisha pia yona daniel, basil mramba na sumaye frederic)., kuletewa kwa nguvu makaburu wa net solutions na kufukuza wazalendo tanesco kina luhanga nk nk. Tunaambiwa ndio epa, kagoda, meremeta, deep green, kashfa ya ndege ya rais, kashfa ya rada ya kijeshi, kuua shirika l ndege na reli huyu ndie aliye m betray mwalimu nyerere japo tuliambiw ni clean na mwalimu huyo huyo!
3. Mwaka huo huo wa 1995, tuliaminishwa kwamba mwalimu alisema mh. Jakaya Kikwete aangaliwe kama mboni ya jicho .japo sijui alikuwa na maana gani, inatosha kusema kwamba legacy yake itahusishwa na uswahiba, udini, kulindana, kiongozi aliyefukuza/ondoa mawaziri zaidi ya 60, serikali mbili kuwajibishwa na bunge, wizi mwingi mkubwa na mdogo kama escrow, epa, kashfa ya richmond , mabehewa feko ya reli, utata bandarini, kujaribu kulindika maendeleo bagamoyo kama bandari, kiwanda cha matunda huku tanga ndio watoa matunda, lami, kiwanda cha sukari (bahati mbaya wafadhili walijitoa), kushindwa kupitisha katiba pendekezwa, na sitashangaa kujaribu kurefusha muda w kutawala au kupigana kuf na kupona kuweka mtu wake kujaribu kuilinda familia yake! Dalili tayari ziki wazi.
4. Kuna huyu mtu anaeitwa Mzee Kasoli, tarishi wa mwalimu miaka hiyo. Nakereka na kuna mtu alisema , hivi bado unakuwa tarishi wa mtu aliyefariki? Kwa kifupi wanaomjua mzee huyu kwanza ni mlevi tu wa kawaida (sidhani kama alikuwa analewa wakati mwalimu yupo (mnafiki tu wa siasa na chuki binafsi). Kuna wakati alilewa pombe akaanza kutishia watu na bastola aliyorithishwa na dr. Julius nyerere polisi wakamnyanganya. Leo anataka tuamini kwamba naye katumwa atuchagulie watanzania kiongozi? Aende akanye pombe zake atulie.
kwa kuhitimisha niseme kwamba kila kitabu na enzi zake. Tusimtumie mwl nyerere kauli zake zote kwa sababu hata yeye hakuweza kujua kilicho ndani ya watu aliowatetea sana, wakafeli baade na ni failure ya mwalimu nyerere pia. Kwa maneno mengine, waacheni wananchi waamue kiongozi wanaomtaka kwa utashi wao maana ni wazi kwamba sasa tunacheza pata potea. Wanasiasa wengi kabisa wamepotoka. Mwacheni mh. Edward Ngoyai Lowassa aje uwanjani ajitambulishe, wampime kama hiyo ndio wish ya watanzania majority. Acheni kura ziamue ili watanzania na tazania isije kumlalamikia mtu yoyote kama ambavyo post moterm ya wagombea wa mwl nyerere inavyodhihirisha ku fail kwa hali ya juu. Nawasilisha.
Mkuu nimekupenda bureeeeeee