Wabunge waasi CHADEMA hawa hapa

Wabunge waasi CHADEMA hawa hapa

WABUNGE MLICHANGIA CHAMA AMA SACCOS?

Ni ukweli kuwa kuna michango ya wabunge inayopelekwa ofisi ya chama makao makuu.

Ni ukweli kuwa kumekuwepo _minong'ono_ Dodoma kuhusu michango hiyo kwamba iko wapi na inafanya nini?

Sasa kwamba Kigogo ameipata hiyo, sioni ubaya. Wala sioni ubaya yeye kuibandika jukwaani na hadharani.

Ni ukweli kwamba Kigogo si mbunge wa CHADEMA wala si mtumishi makao makuu. Kwa hiyo hana popote atakakopata taarifa hii ya siri. Lazima amepelekewa na mmoja wa wabunge. Lwa hiyo Kigogo hana kosa lolote katika hatua ya sasa. Labda hapo baadaye.

Sasa tujiulize; kama ilikuwa sahihi wabunge kuchangia chama chao hela kama shukrani kwa kuwadhamini na kukiimarisha chama kimfumo.

Nashindwa kujua ni nini makubaliano baina ya wabunge wetu na chama nyuma ya michango hiyo. Ikumbukwe kuwa michango hii ni takwa la katiba ya chama. Hakuna kwenye katiba inapoelezwa kwamba wabunge wakiisha changa watauliza iliko hela waliyochanga.

Kama kweli maelezo yanayotolewa ni kwamba walikuwa wakichangia katika mfuko wa chama kwa ajili ya uchaguzi ujao 2020, kwa nini maulizo haya yanakuja leo?

Sijui kama wabunge wetu wanachanga ili warudishiwe hizo hela ama wanachanga ili hela zitumiwe na chama kwa mujibu wa mipango yake?

Je, wabunge wanaona sadaka yao ya fedha ni kubwa kiasi kwamba haiwezi kujadiliwa ndani ya chama bali nje kulikojaa maadui zetu? Je ni kweli chama kilichowajenga na kuwapa ubunge sasa kinapokea fadhila ya kubomolewa na ninyi mlioshiba na kung'aa kwa jina la chama?

Kuna anayefikiri mnamkomoa Mbowe. Lakini niwaambie sisi wenzenu tuliofanya kazi miaka nenda rudi. Usiku na mchana tukawajengea mtandao imara ambao kwao mlikuja kushinda ubunge. Sisi tuliopoteza fursa nyingi kwa kuwa tulijitambulisha na upinzani. Sisi tuliopoteza mali nyingi kwa kugharamikia upinzani. Sisi tulionyang'anywa mali na kuhatarishwa maisha yetu kwa kuwa tumeamua kukipigania chama chenu. Sisi tuliojazwa madonda kutoka kwa watawala wanaokasirishwa na uimara wa chama chetu; leo mnaongezea pilipili kwenye madonda yetu. Hakika ukatili huu ni mkubwa sana.

Hivi wabunge wanapodai sehemu ya mshahara wao wanaouchanga kwa ajili ya chama walituambia lini sehemu inayobaki wameitumia vipi kwa ajili ya majimbo na chama katika mikoa na kanda zao.

Nilibahatika kusikia mahali kuhusu harakati ndani ya chama dhidi ya Mbowe. Harakati hizi pia zilikuwa dhidi yake kama KUB.

Wabunge wetu hawa nilinusa habari kuwa katika kikao kimoja cha kambi walisimama na kumpongeza Mhe. Zitto kwa kazi nzuri aliyofanya ya kumhudumia Lissu bila kumtaja Mbowe popote. Ilipikwa fitina dhidi ya Mbowe kwamba katika tukio la kishambuliwa kwa Lissu, Mbowe ndiye "wasiojulikana". Hii si ile propaganda ya CCM bali ni ya ndani ya chama na iliyoasisiwa bungeni.

Chama kimenyamazia wabunge hawa kwa muda mrefu. Wamejiona wafalme wa chama. Wanajua kosa la kupeleka habari za chama nje ya vikao rasmi vya chama. Je huu si uvunjifu wa kanuni na katiba ya chama kwa makusudi?

Kwa hapa walipotufikisha, Nitashangaa sana:
1. Kama tutawanyamazia. Hatuhitaji msaada wa Kamati Kuu wala Baraza Kuu. Tuwapa vidonge vyao huku huku.
2. Tuwajazie taarifa za imani yetu kwa Mbowe. Na tahadhari kwamba titawashambulia kushoto, kulia, mbele na nyuma wakiendelea na majaribio yao haya.

Waheshimiwa makamanda. Mti wenye matunda ndiyo utupiwao mawe. Hawa wabunge nani amewasikia majimboni ama katika harakati za kumaanisha za kujenga chama?

Mbowe kwa ajili yetu na taifa amepitia madhila mangapi? Mali zake zilizoharibiwa ni za bei gani? Akaunti zake zilizofungwa ni za thamani gani? Amepoteza vingapi ili kutufikisha hapa tulipo.

Kwa nini wabunge wetu wachague kumlipa fedheha badala ya fadhila kwa harakati zote alizofanya hadi kufikia hapa tulipo!

Naogopa kumadress Mbowe katika hili. Ila nitawashanga mkiwanyamazia wabunge hao wanaoiona sadaka yao kuwa ni kubwa kuliko za watu wengine ambao hawajalipwa mishahara na posho za kibunge kama wao.

Hivi mimi nimekuwa katibu wa mkoa kwa miaka 10. Sijawahilipwa mshahara miaka yote hiyo. Je sadaka yangu hii ambayo niliitoa ili wapatikane wabunge nani alitakiwa ailipe? Mmeniletea lini mafuta pipa moja la kufanya ziara mkoani kwangu. Aje hapa Katibu mwenzangu yeyote wa mkoa aonyeshe anavyolipwa fadhila na wabunge aliowapigania.

Nasema semeni yote muyatakayo, fanyeni yote muyawezayo, nendeni popote mtakako:

Mwenyekiti wetu ajaye ni FREEMAN AIKAEL MBOWE.

Update 2:

Anaandika Halima James Mdee (Mb), Mjumbe Wa Kamati Kuu CHADEMA.

Sisi wabunge tunaochangia PESA na ambao ni WAJUMBE wa KAMATI KUU tunaopata fursa ya kupata taarifa za MAPATO na Matumizi ya CHAMA TUNATHIBITISHA hakuna hata 100 iliyoliwa na MTU..Wakongwe katika hiki CHAMA tunajua kila mwaka wa UCHAGUZI ukifika kuna CHOKOCHOKO nyingi zinazohusu FEDHA. Najiuliza tu, hivi kama hizo pesa za UMMA zinapigwa na WATU kwenye CHAMA namna hiyo mbona SERIKALI ya CCM tena MAGUFULI anavyotuchukia ASITUFUNGULIE MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI??

Hivi MNAVYOONA SHUGHULI za CHAMA zinaendelea NCHI nzima yenye ukubwa wa sQuare KM 945,087 mnadhani pesa inatoka wapi? Mnavyoona Pikipiki zinakwenda nchi NZIMA sio mara moja au mbili mnadhani pesa zinatoka wapi? Mnapoona M4C mpya zinanunuliwa mnadhani pesa inatoka wapi?? Sasa hivi CHAMA kiko kwenye Chaguzi NCHI nzima mnadhani pesa zinatoka wapi? Mnajua gharama za Matibabu ya KAMANDA wetu mpaka sasa hivi IMEGHARIMU kiasi GANI na CHAMA kimeshatumia KIASI gani ??Mnataka SASA tuanze kurusha Twitter AU INSTAGRAM au kwenye HIZI groups???mapato na matumizi ya chama?? Wenyeviti na MAKATIBU wa KANDA zenu WAJUMBE wa KAMATI KUU, wanajua TAARIFA zote za FEDHA. Wafuateni KWENYE ofisi zao wawape Ufafanuzi wa jambo lolote mnalodhani linahitaji ufafanuzi. Ni kweli kuna wabunge ambao UTEKELEZAJI wa TAKWA la KATIBA la KUCHANGIA chama umekuwa ukiwauma SANA.

Hawajawahi kutaka toka awali, hawa ndio walienda kulalamika kwa NDUGAI na Hawa ndio wanafanya kazi na CCM Bungeni kuumiza au kuwachonganisha wabunge wenzao na MHIMILI. Miaka yote kabla 2015, tumekuwa tukichanga kwa kukatwa moja kwa moja na ofisi ya katibu ya Bunge.

Baada ya 2015 tumeendelea kukatwa mpaka hao WAPUUZI wanaojulikana hawajaenda kwa ADUI yetu kumwambia CDM haitetereki sababu wabunge tunachangia na kwamba AKIZUIA CHAMA kitasota, na KWELI YULE PIMBI akazuia. Kumbe wabunge WALIOPELEKA HUO uzushi wamesukumwa na UBINAFSI wao wa KUKOPA mpaka kupitiliza... mpaka kufikia hatua ya kuona MCHANGO HALALI wa KIKATIBA ni HISANI kwa CHAMA.

Wamesahau na SISI huko nyuma tukiwa WACHACHE tulichanga kwa UAMINIFU MKUBWA ndio maana WAO wakapatikana. Tuna wabunge WAFIA CHAMA, lakini pia tuna wabunge MASLAHI . Ni ukweli mchungu!! Tukiimarishe CHAMA , tupate WAWAKILISHI wanaotanguliza MASLAHI ya UMMA na CHAMA kabla ya MASLAHI yao BINAFSI. Nashukuru MUNGU MAGUMU tunayoyapitia MSIMU HUU yanatukomaza na kutufanya TUJUANE ZAIDI.
Huyu bundi wa sasa ni mwekundu. Mkuu Molemo pole sana naona CDM ipo hospitali na ugonjwa wake ni Ebola na kwa hakika Mungu ataipenda zaidi. Hakuna namna zaidi ya kuanza kuandaa mapambio ya kuiaga CDM. Lakini siku ya kusoma wasifu wasifu tutakuwa na mengi ya kusema kuhusu mafanikio ya CDM wakati akiwa hai hapa dunia.
 
Wabunge wetu hawa nilinusa habari kuwa katika kikao kimoja cha kambi walisimama na kumpongeza Mhe. Zitto kwa kazi nzuri aliyofanya ya kumhudumia Lissu bila kumtaja Mbowe popote. Ilipikwa fitina dhidi ya Mbowe kwamba katika tukio la kishambuliwa kwa Lissu, Mbowe ndiye "wasiojulikana". Hii si ile propaganda ya CCM bali ni ya ndani ya chama na iliyoasisiwa bungeni.
LOooo, mbona mmechanganyikiwa hivi!
Kuyasoma haya hata yakitajwa tu toka kwa watu walioko ndani ya chama..., kunatia matumaini hapa?

Ngoja niendelee kuisoma njozi hii, inayosikitisha .
 
Naona kigogo kawanyuka, hana rafiki siyo ? Maana wengi walikua mashabiki wake
 
Kitu kingine ni kwamba hata sisi wananchi tunalipa kodi na tuna haki ya kuhoji zinavyotumika, sembuse wabunge wanaokatwa mishahara yao unataka wasihoji zinavyotumika?
Nimesoma bandiko ulilosoma wewe.
Mimi sijaona mahala popote linaposema "wabunge wanaokatwa mishahara wasihoji."
Au kuna bandiko jingine tofauti ulilosoma ambalo mimi bado sijalisoma?
 
Huyu bundi wa sasa ni mwekundu. Mkuu Molemo pole sana naona CDM ipo hospitali na ugonjwa wake ni Ebola na kwa hakika Mungu ataipenda zaidi. Hakuna namna zaidi ya kuanza kuandaa mapambio ya kuiaga CDM. Lakini siku ya kusoma wasifu wasifu tutakuwa na mengi ya kusema kuhusu mafanikio ya CDM wakati akiwa hai hapa dunia.
Nimekuzoea kwa porojo miaka nenda rudi.Sikushangai
 
Asante Mheshimiwa Mdee ingawa watu wa aina hiyo wapo hata CCM na hata mbinguni walikuwepo malaika waasi. Kinachotakiwa ni kuwatambua ili mjitenge nao mapema kabla hawajawa 'malucifer' wakamatwe kuharibu mtaji wa wanachama waliopo.
Kwa sisi wakereketwa wa mageuzi ya kweli inauma sana kuona mlikaa muda mrefu na wasaliti hadi wakafikia hatua ya kutuvua nguo baada ya kukaribishwa hadi jikoni - akina Waitara kwa mfano. Chukueni hatua mapema kabla hawajafanya uharibifu mkubwa kwenye upinzani wa kweli.
Kwa Taarifa za uhakika nilizopewa hatua zitachukuliwa
 
Chadema ni kama mradi mkuu. Kumpokea Lowassa na kumfanya kuwa mgombea urais ilikuwa ni kiashiria cha kwanza cha kile kinachoitwa 'biashara ya siasa'. Ilitazamwa pesa kwanza na misingi ya chama ikatupwa huko.

Sidhani kama kuna mtu mwenye akili anayetaka washike dole,wengi tunataka wawe na nguvu(wengi bungeni) ili waweze kupiga kelele serikali inapofanya mambo ya hovyo.

Huko chamani mtu akihoji matumizi ya pesa anaitwa msaliti, kuna tofauti gani na hawa wanaoita watu wasaliti wa taifa pale wanapohoji matumizi ya pesa za umma?
​

Hujui usemacho.Pole
 
Waitara kapata wafuasi, lakini kabla hawajahama wanataka kukiua au kukifarakanisha chama na wafuasi, Mkiwa makini mtaliona hilo.
Wamesha ahidiwa au kulipwa pesa na ccm, kinachofanyika ni kulitifua tu, kisha wao wana exit kupitia emergency door.
 
Waitara kapata wafuasi, lakini kabla hawajahama wanataka kukiua au kukifarakanisha chama na wafuasi, Mkiwa makini mtaliona hilo.
Wamesha ahidiwa au kulipwa pesa na ccm, kinachofanyika ni kulitifua tu, kisha wao wana exit kupitia emergency door.
Ubavu wa kusambaratisha CDM hawana.Watasambaratika wao.Hilo nakuhakikishia
 
Back
Top Bottom