Wabunge waasi CHADEMA hawa hapa

Wabunge waasi CHADEMA hawa hapa

WABUNGE MLICHANGIA CHAMA AMA SACCOS?

Ni ukweli kuwa kuna michango ya wabunge inayopelekwa ofisi ya chama makao makuu.

Ni ukweli kuwa kumekuwepo _minong'ono_ Dodoma kuhusu michango hiyo kwamba iko wapi na inafanya nini?

Sasa kwamba Kigogo ameipata hiyo, sioni ubaya. Wala sioni ubaya yeye kuibandika jukwaani na hadharani.

Ni ukweli kwamba Kigogo si mbunge wa CHADEMA wala si mtumishi makao makuu. Kwa hiyo hana popote atakakopata taarifa hii ya siri. Lazima amepelekewa na mmoja wa wabunge. Lwa hiyo Kigogo hana kosa lolote katika hatua ya sasa. Labda hapo baadaye.

Sasa tujiulize; kama ilikuwa sahihi wabunge kuchangia chama chao hela kama shukrani kwa kuwadhamini na kukiimarisha chama kimfumo.

Nashindwa kujua ni nini makubaliano baina ya wabunge wetu na chama nyuma ya michango hiyo. Ikumbukwe kuwa michango hii ni takwa la katiba ya chama. Hakuna kwenye katiba inapoelezwa kwamba wabunge wakiisha changa watauliza iliko hela waliyochanga.

Kama kweli maelezo yanayotolewa ni kwamba walikuwa wakichangia katika mfuko wa chama kwa ajili ya uchaguzi ujao 2020, kwa nini maulizo haya yanakuja leo?

Sijui kama wabunge wetu wanachanga ili warudishiwe hizo hela ama wanachanga ili hela zitumiwe na chama kwa mujibu wa mipango yake?

Je, wabunge wanaona sadaka yao ya fedha ni kubwa kiasi kwamba haiwezi kujadiliwa ndani ya chama bali nje kulikojaa maadui zetu? Je ni kweli chama kilichowajenga na kuwapa ubunge sasa kinapokea fadhila ya kubomolewa na ninyi mlioshiba na kung'aa kwa jina la chama?

Kuna anayefikiri mnamkomoa Mbowe. Lakini niwaambie sisi wenzenu tuliofanya kazi miaka nenda rudi. Usiku na mchana tukawajengea mtandao imara ambao kwao mlikuja kushinda ubunge. Sisi tuliopoteza fursa nyingi kwa kuwa tulijitambulisha na upinzani. Sisi tuliopoteza mali nyingi kwa kugharamikia upinzani. Sisi tulionyang'anywa mali na kuhatarishwa maisha yetu kwa kuwa tumeamua kukipigania chama chenu. Sisi tuliojazwa madonda kutoka kwa watawala wanaokasirishwa na uimara wa chama chetu; leo mnaongezea pilipili kwenye madonda yetu. Hakika ukatili huu ni mkubwa sana.

Hivi wabunge wanapodai sehemu ya mshahara wao wanaouchanga kwa ajili ya chama walituambia lini sehemu inayobaki wameitumia vipi kwa ajili ya majimbo na chama katika mikoa na kanda zao.

Nilibahatika kusikia mahali kuhusu harakati ndani ya chama dhidi ya Mbowe. Harakati hizi pia zilikuwa dhidi yake kama KUB.

Wabunge wetu hawa nilinusa habari kuwa katika kikao kimoja cha kambi walisimama na kumpongeza Mhe. Zitto kwa kazi nzuri aliyofanya ya kumhudumia Lissu bila kumtaja Mbowe popote. Ilipikwa fitina dhidi ya Mbowe kwamba katika tukio la kishambuliwa kwa Lissu, Mbowe ndiye "wasiojulikana". Hii si ile propaganda ya CCM bali ni ya ndani ya chama na iliyoasisiwa bungeni.

Chama kimenyamazia wabunge hawa kwa muda mrefu. Wamejiona wafalme wa chama. Wanajua kosa la kupeleka habari za chama nje ya vikao rasmi vya chama. Je huu si uvunjifu wa kanuni na katiba ya chama kwa makusudi?

Kwa hapa walipotufikisha, Nitashangaa sana:
1. Kama tutawanyamazia. Hatuhitaji msaada wa Kamati Kuu wala Baraza Kuu. Tuwapa vidonge vyao huku huku.
2. Tuwajazie taarifa za imani yetu kwa Mbowe. Na tahadhari kwamba titawashambulia kushoto, kulia, mbele na nyuma wakiendelea na majaribio yao haya.

Waheshimiwa makamanda. Mti wenye matunda ndiyo utupiwao mawe. Hawa wabunge nani amewasikia majimboni ama katika harakati za kumaanisha za kujenga chama?

Mbowe kwa ajili yetu na taifa amepitia madhila mangapi? Mali zake zilizoharibiwa ni za bei gani? Akaunti zake zilizofungwa ni za thamani gani? Amepoteza vingapi ili kutufikisha hapa tulipo.

Kwa nini wabunge wetu wachague kumlipa fedheha badala ya fadhila kwa harakati zote alizofanya hadi kufikia hapa tulipo!

Naogopa kumadress Mbowe katika hili. Ila nitawashanga mkiwanyamazia wabunge hao wanaoiona sadaka yao kuwa ni kubwa kuliko za watu wengine ambao hawajalipwa mishahara na posho za kibunge kama wao.

Hivi mimi nimekuwa katibu wa mkoa kwa miaka 10. Sijawahilipwa mshahara miaka yote hiyo. Je sadaka yangu hii ambayo niliitoa ili wapatikane wabunge nani alitakiwa ailipe? Mmeniletea lini mafuta pipa moja la kufanya ziara mkoani kwangu. Aje hapa Katibu mwenzangu yeyote wa mkoa aonyeshe anavyolipwa fadhila na wabunge aliowapigania.

Nasema semeni yote muyatakayo, fanyeni yote muyawezayo, nendeni popote mtakako:

Mwenyekiti wetu ajaye ni FREEMAN AIKAEL MBOWE.

Update 2:

Anaandika Halima James Mdee (Mb), Mjumbe Wa Kamati Kuu CHADEMA.

Sisi wabunge tunaochangia PESA na ambao ni WAJUMBE wa KAMATI KUU tunaopata fursa ya kupata taarifa za MAPATO na Matumizi ya CHAMA TUNATHIBITISHA hakuna hata 100 iliyoliwa na MTU..Wakongwe katika hiki CHAMA tunajua kila mwaka wa UCHAGUZI ukifika kuna CHOKOCHOKO nyingi zinazohusu FEDHA. Najiuliza tu, hivi kama hizo pesa za UMMA zinapigwa na WATU kwenye CHAMA namna hiyo mbona SERIKALI ya CCM tena MAGUFULI anavyotuchukia ASITUFUNGULIE MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI??

Hivi MNAVYOONA SHUGHULI za CHAMA zinaendelea NCHI nzima yenye ukubwa wa sQuare KM 945,087 mnadhani pesa inatoka wapi? Mnavyoona Pikipiki zinakwenda nchi NZIMA sio mara moja au mbili mnadhani pesa zinatoka wapi? Mnapoona M4C mpya zinanunuliwa mnadhani pesa inatoka wapi?? Sasa hivi CHAMA kiko kwenye Chaguzi NCHI nzima mnadhani pesa zinatoka wapi? Mnajua gharama za Matibabu ya KAMANDA wetu mpaka sasa hivi IMEGHARIMU kiasi GANI na CHAMA kimeshatumia KIASI gani ??Mnataka SASA tuanze kurusha Twitter AU INSTAGRAM au kwenye HIZI groups???mapato na matumizi ya chama?? Wenyeviti na MAKATIBU wa KANDA zenu WAJUMBE wa KAMATI KUU, wanajua TAARIFA zote za FEDHA. Wafuateni KWENYE ofisi zao wawape Ufafanuzi wa jambo lolote mnalodhani linahitaji ufafanuzi. Ni kweli kuna wabunge ambao UTEKELEZAJI wa TAKWA la KATIBA la KUCHANGIA chama umekuwa ukiwauma SANA.

Hawajawahi kutaka toka awali, hawa ndio walienda kulalamika kwa NDUGAI na Hawa ndio wanafanya kazi na CCM Bungeni kuumiza au kuwachonganisha wabunge wenzao na MHIMILI. Miaka yote kabla 2015, tumekuwa tukichanga kwa kukatwa moja kwa moja na ofisi ya katibu ya Bunge.

Baada ya 2015 tumeendelea kukatwa mpaka hao WAPUUZI wanaojulikana hawajaenda kwa ADUI yetu kumwambia CDM haitetereki sababu wabunge tunachangia na kwamba AKIZUIA CHAMA kitasota, na KWELI YULE PIMBI akazuia. Kumbe wabunge WALIOPELEKA HUO uzushi wamesukumwa na UBINAFSI wao wa KUKOPA mpaka kupitiliza... mpaka kufikia hatua ya kuona MCHANGO HALALI wa KIKATIBA ni HISANI kwa CHAMA.

Wamesahau na SISI huko nyuma tukiwa WACHACHE tulichanga kwa UAMINIFU MKUBWA ndio maana WAO wakapatikana. Tuna wabunge WAFIA CHAMA, lakini pia tuna wabunge MASLAHI . Ni ukweli mchungu!! Tukiimarishe CHAMA , tupate WAWAKILISHI wanaotanguliza MASLAHI ya UMMA na CHAMA kabla ya MASLAHI yao BINAFSI. Nashukuru MUNGU MAGUMU tunayoyapitia MSIMU HUU yanatukomaza na kutufanya TUJUANE ZAIDI.
Asante Mheshimiwa Mdee ingawa watu wa aina hiyo wapo hata CCM na hata mbinguni walikuwepo malaika waasi. Kinachotakiwa ni kuwatambua ili mjitenge nao mapema kabla hawajawa 'malucifer' wakamatwe kuharibu mtaji wa wanachama waliopo.
Kwa sisi wakereketwa wa mageuzi ya kweli inauma sana kuona mlikaa muda mrefu na wasaliti hadi wakafikia hatua ya kutuvua nguo baada ya kukaribishwa hadi jikoni - akina Waitara kwa mfano. Chukueni hatua mapema kabla hawajafanya uharibifu mkubwa kwenye upinzani wa kweli.
 
Vibaraka wa Mbowe wanatumia nguvu nyingi sana kutafuta uungwaji mkono
 
Uchaguzi 2015,japokua chadema ilipata kuranyingi nakupelekea ruzuku kubwa kupishana naccm kidogo mgao waruzuku kwamwezi toka serikalini,mamluki walikua wengi nambowe alikengeuka nakuwaamini.naamini waliopo kuazia wabunge ninjaa ndo imewaweka ila sio chadema nambowe ajue hilo
 
Halima Mdee aache kuzingua yaani taarifa za mapato na matumizi ya chama mpaka watu wakaulize wajumbe wa kamati kuu?
Ni kwenye kipengele gani cha katiba wajumbe wa kamati kuu wana kazi ya kutoa taarifa za mapato na matumizi ya chama?

Hapa uongozi wa Chadema ueleze, pesa zinazopatikana zimetumikaje?
Kama ni kwenye kumtibia Lissu iwekwe wazi, kama ni kazi za chama iwekwe wazi!

Ziko wapi taarifa za auditor wa matumizi ya pesa za chama?

Lazima CHADEMA ionyeshe utofauti, siyo kutaka Transparency serikalini wakati nyinyi wenyewe si wawazi
 
Mungu ibariki Chadema
Anaibariki vipi wakati ni majizi?? Msikie hapa kigogo (yule unayeamini taarifa zake kwa sasa)
IMG_20190920_180858.jpg
 
Yaleyale ya ccm, Leo membe anaandamwa kisa kutumia haki yake kama mwanachama kuwaomba wanachama wenzie wampe ridhaa ya kupeperusha chama chao imekuwa nongwa.hivi chadema hawajifunzi hayo? Hawajawaona wenzao Kule marekani democrat? Wagombea 10 wanachuana? Haya mavyama Ni shida.

Mfano wako fake. Nchi inaongozwa na TRUmp. RP. Kama wangekuja wagombea toka Republican ndo hoja yako ingekuwa na mshiko
 
Kazunguka weee, lakini hitimisho ni mwenyekiti ajaye ni freeman mbowe. Kwa aina hii ya siasa, mtu akijitokeza kum-challenge mbowe mtu huyo atakuwa salama?!
Salama salimini, huku hawezi kutishwa kama Membe maana Chadema haina dola ukitishwa nenda polisi waliokutisha washughulikiwe.
Kama watu wakivaa tuu T-shirt mnawakamata mtashindwa kumkamata anayetishia maisha? Si atakuwa anasindikizwa na defender!
 
Salama salimini, huku hawezi kutishwa kama Membe maana Chadema haina dola ukitishwa nenda polisi waliokutisha washughulikiwe.
Kama watu wakivaa tuu T-shirt mnawakamata mtashindwa kumkamata anayetishia maisha? Si atakuwa anasindikizwa na defender!
Mkuu Chakaza, hii kauli ya Molemo haijakaa sawa. "Nasema semeni yote muyatakayo, fanyeni yote muyawezayo, nendeni popote mtakako:

Mwenyekiti wetu ajaye ni FREEMAN AIKAEL MBOWE."
 
Nimewahi kusema ukiona kiongozi yoyote hasa wa kiafrika anakaa madarakani zaidi ya miaka 10 tegemea mauzauza. Kama pesa inachangwa, kuna ubaya gani wachangiaji kuhoji matumizi yake? Kupewa nafasi na chama kuwa mbunge isiwe ndio kiziba mdomo cha kuhoji matumizi yenye kutia shaka. Sasa kama pesa zenu wenyewe mna matumizi yenye kuacha shaka, mtawezaje kuhoji za umma, ni wapi mtapata huo uhalali?

Mleta uzi unasema iwe isiwe mwenyekiti wa cdm ni lazima awe Mbowe, sasa mnaitisha uchaguzi wa nini wakati mwenyekiti atakuwa Mbowe? Hivi Mbowe amekaa madarakani zaidi ya miaka 15, ni kweli mnataka tuamini huko cdm hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuwa mwenyekiti zaidi ya Mbowe!? Katika mazingira ambayo mnaaminisha watu kuwa Mbowe pekee ndio anafaa kuwa mwenyekiti, hamuoni kuwa kuna kikundi kinachofaidika na madaraka ya Mbowe na hicho kikundi ndio hasa kinachofuja hizo pesa zenye utata hivi sasa?

Hivi mnaamini wengine wote hatujui chama na thamani ya kukilinda chama ni ipi, mpaka mfiche uhuni wa matumizi mabovu ya pesa kwa kisingizio cha chama kitayumba? Kama uimara wa chama ni kufumbia macho matumizi mabaya ya pesa za taasisi, si bora hicho chama kife tu? Kwa kosa tu la kumkaribisha Lowasa chamani na kumpa nafasi ya kugombea urais, huku akiwa hana mapenzi wala kujua lolote kuhusu chama, kulitosha kabisa Mbowe na uongozi wake wote kujiuzulu. Sisi wengine tuna imani na cdm na sio uongozi wa Mbowe tena kwenye makosa ya wazi hivi.
 
Kwa kosa tu la kumkaribisha Lowasa chamani na kumpa nafasi ya kugombea urais, huku akiwa hana mapenzi wala kujua lolote kuhusu chama, kulitosha kabisa Mbowe na uongozi wake wote kujiuzulu.
Wangekuwa hata na chembe ya uungwana wangewaomba wanachama na mashabiki wao wote radhi kwa kosa kubwa walilofanya lakini wamejaa kiburi na kubatiza usaliti kila anayeliona kosa lile.
 
Mfia chama naona leo maji shingoni. Nilishawahi kusema humu, CDM wanaweza kuwa wabaya kuliko CCM, Angalia wanavyotokwa na povu kumlinda Mbowe, halafu hawataki Makonda and the CO walinde wanapopata ugali wao. Mbu.r.u.r.a kweli hawa watu!
Hatari, hata Tanzania Daima Zitto alisema lilianzishwa kwa pesa ya chadema. Mkono na Rostam wakatoa pesa ya kusaidia chadema Mbowe akadai ni pesa yake amekikopesha chama. Jambazi sugu hili.
 
Binadamu wameumbwa kuwa wabinafsi katika maisha, wanataka mambo mazuri yawe upande wao peke yao hawataki upande wa pili, lakini pia hawako tayari kuruhusu kuumia kwa muda fulani ili baadae wacheke kwa pamoja, kwa sasa asilimia kubwa ya wawakilishi wetu bungeni wapo kwa ajili ya matumbo yao na siyo maslahi ya chama kikichowapa dhamana, ikitokea ya kwamba ameenguliwa kwenye nafsi yake atatembea usiku na mchana kueneza maneno machafu lengo tu aendelee kuonekana mwema machoni pa wengi. Kwa sasa makumbano siyo mazuri, kikubwa vyama vya upinzani vinatakiwa kukaa chini na kuangalia namna ambavyo wanaweza kuleta ushindani katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni
 
Back
Top Bottom